Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

watanzania gani waliumia wewe.wananchi tulio wengi tuliishi maisha ya kawaida tu kama tunavyoishi sasa.labda ninyi mabepari wakwepa kodi ndo mdai mliumizwa.afu msipende kuzungumzia maumivu yenu wachache kuwakilisha umma mkubwa wa watanzania
 
"Watu wabaki na n'nyaaaa yao nyumbani??!!",----- Hivi kweli Magu kama Rais alifikia hatua ya kutamka maneno hayo kuwaambia Watu au mnamsingizia tu kwa kuwa hayupo???? Looo siamini !!!.[emoji32]
Pole mkuu maana nia yangu sio kukuaminisha wewe, nimeongea what i feel.

Alaf mimi na Magu hatukuwahi kujuana personally kiasi cha kuanza kumsimgizia vitu kama hivi. Ukiwa mfatiliaji, haya yote yalifanyika hadharani, na wala sio siri. Utayajua tu
 
Mazingira ya kutaka kusifiwa kinafiki aliyetengeneza yeye. Hizo ni sifa za dictators wote.
sasa mpaka amekufa bado uhisi watu wanamuogopa!!!!

huoni kama una tatizo la kufikiri???
 
Nakubaliana na wewe Mkuu. Hili jambo linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee. Na wale watu wasiojulikana waliokuwa wakishirikiana na Jiwe kuwatesa kuwauniza na hata kuwatowesha wengine Duniani, nao wanapaswa kuomba radhi peke yao kwani wao yawezekana bado wako hai.

Wasiwe na hofu kwani ni wazi kuwa walikuwa na utii kwa mwenye Mamlaka.
waombe radhi kwanini!!!

kwani walifanya kwa kumuonea mtu!!kwa sasa bado hayo mambo yapo sana tu.mtaanza kuyasikia tena ili muelewe aina ya jambo mnalopigia kelele.
 
nimeongea what i feel.

Umeongea what you feel or what you believe he said with evidence ??!🤔

Maana yangu ni hii: tumlaumu mtu kwa matendo aliyoyatenda tusimlaumu kwa kitu ambacho hakutenda, hiyo ndio haki.
 
Umeongea what you feel or what you believe he said with evidence ??![emoji848]

Maana yangu ni hii: tumlaumu mtu kwa matendo aliyoyatenda tusimlaumu kwa kitu ambacho hakutenda, hiyo ndio haki.
Niliposema "what i feel" nilikuwa namaanisha kulingana na msamaha ambao jamaa amemuombea, mm nimecomment kulingana na ninavyojiskia kutokana na yaliyofanywa na Magu.

Tukirudi kwako, Sitaki kuamini kama ni kweli hukuwahi kuiskia hii kauli ya Magu alivyojibu hadharani bila kupepesa macho.

Anyway, tafuta uzi unaosema utamkumbuka Magu kwa kipi, mule ndani nahisi kuna mtu aliweka ile clip.

Jamaa alikuwa na kauli za kejeli na dharau sana. Huo ndio ukweli
 
Hii ishu ni rahisi tu, 'you can mark bads out of goods' na wewe utakuwa sawa tu ama pia unaweza 'kumark goods out of bads' wewe pia upo sawa tu kwa sababu binadamu walio wengi ama ni optimistic au ni pesmistic kulingana tu na namna alivyokuwa na mazingira aliyopitia mpaka kuwa mtu mzima. Mtihani uliopo hapa ni kujua wewe ni binadamu wa namna gani hasa ili uweze kuiendana na wenzako ambao wengine si wa namna yako.
Hoja yangu hapa ni kwamba, kunamtu anataka kusema kwamba JPM amefanya mengi mazuri (pengine hata kwa mifano hai) lakini mwingine anasema hapana hayati JPM kafanya mabaya mengi tena kwa mifano pia.
Mimi kama nygax nakubaliana kabisa kwamba yapo mazuri yaliyofanywa na mabaya pia. Swali ni je, kati ya mazuri au mabaya ni yapi yamekuwa na uzito mkubwa kwa taifa? ili tuweze ama kuiona au kutokuiona legacy ya hayati JPM.
Niungane na mtoa uzi hapa kwamba kwa Yale aliyokosea tumsamehe lakini Mimi niongeze kwa kusema kwa Yale mazuri aliyoyafanya basi pia tuyaone maana yeye yupo udongoni lakini inawezekana mpaka muda huu kunawatu wananeemeka na angalau 'kakitu' alikokaacha.
Asanteni.
 
sasa mpaka amekufa bado uhisi watu wanamuogopa!!!!

huoni kama una tatizo la kufikiri???

Amekufa miaka 200 iliyopita au ni mwezi uliopita? Hivi ukipata kidonda kovu linaisha ndani ya mwezi?
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Sisi wengine tunamshukuru tu Mungu kwa kutuondolea udhia nchi hii. Hallelujah!
 
Kwani ametukosea nini sisi Watanzania? Kwa level ya Taifa sioni kosa lake labda kwa level ya mtu binafsi. Kama ni hivyo, basi ni jukumu la familia yake. But sisi kama Wananchi, we are proud of him and we would had wished him to live longer.

R.I.P JPM

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Huwezi kuona kosa kwa Level ya Taifa kwa Sababu aliku Brainwash, ni Level ya Watu Binafsi aliofanikiwa kuwa Brainwash na wale aliokuwa anaiba nao kama Bashite, Sabaya and the like ndio wako Proud nae, ila sio Wananchi
 
Marehemu asemwi vibaya ila jiwe alipokufa watu mioyo yao ilishangilia.

Kufa wote tutakufa ila insue nani anatangulia?

Jiwe kanitesa binafsi ila nishamsamehe muda sana.
Mi bado sijamsamehe aisee. Ametutesa sana watu wa kaskazini. Yan kutoka Arusha iliyokuwa inasifika kwa maisha bora mpaka ukapuku. Alihakikisha vyanzo vyote vya mapato vinavyowainua watu wa Arusha anavivuruga na kuvibana, alihakikisha biashara na Kenya haifanyiki, matajiri wa migodi ya Tanzanite wanachukuliwa hela zao kwenye akaunti kwa kodi za kubambikiwa, wengine wanashtakiwa ili washindwe tu kuendeleza uchimbaji, makampuni yaliyokuwa yanaendesha biashara ya mbogamboga na maua wakavurugwa hadi wakahamia kenya, utalii ukavurugwa kwa kuongeza kodi za ajabu ajabu, mikutano ya kimataifa ikapigwa zengwe isifanyikie Arusha, kisa tu watu wa kaskazini ni wapinzani. Sasaiv majority ya watu wa Arusha wanapitisha mchana bila kula daily, usiku nayo imekuwa kula ni majaliwa! Toka Geneva ya Africa mpaka ukapuku! Lakin ukienda kwao kanda ya ziwa full kujiachia! Hakuna kitu kimeguswa
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Umetumia kigezo cha kumwomba msamaha jpm,JE na familia zilizopoteza watu wao wakimlilia jpm kwa mapenz makubwa? Na kundi kubwa la waombelezaji,JE kuna watu waliandamana kufurahia kifo chake?!,usiwe mnafiki,bora ujiombee wewe mwenyewe,naamini wewe ukifa hakuna hata mmoja atakae kulilia wala kufa kwa ajiri yako,bora hai waharifu wasimsamehe magu,
 
waombe radhi kwanini!!!

kwani walifanya kwa kumuonea mtu!!kwa sasa bado hayo mambo yapo sana tu.mtaanza kuyasikia tena ili muelewe aina ya jambo mnalopigia kelele.
Mkuu wewe ni miongoni mwao nn?? Kumbuka kila alitendalo binadamu gizani Mungu huliweka nuruni.
 
Mkuu wewe ni miongoni mwao nn?? Kumbuka kila alitendalo binadamu gizani Mungu huliweka nuruni.
ya Mungu apewe mungu na kaisari apewe kaisari.

kama umeamua kukinzana na kaisari ukitarajia mungu aingilie kati unajichanganya.
 
Sasa wale waliokuwa wanaimba mapambio ya kuwa kaletwa na Mungu, haijawahi kutokea na wengine wakadiriki kumpa jina la shujaa wa Africa sijui na wao wana mtazamo kama wako au la!!
 
watanzania gani waliumia wewe.wananchi tulio wengi tuliishi maisha ya kawaida tu kama tunavyoishi sasa.labda ninyi mabepari wakwepa kodi ndo mdai mliumizwa.afu msipende kuzungumzia maumivu yenu wachache kuwakilisha umma mkubwa wa watanzania
Wacha uwongo wewe. Hata mama Janet Magufuli mwenyewe alikuwa anateseka sasa hivi ndiyo tunaiona smile yake baada ya Mwendazake kufariki, sembuse ya wewe unyakudongo ??

Usiwasemee Watanzania, jisemee nafsi yako
 
Back
Top Bottom