Kwa video hii, a boy from Tandale lazima ifungiwe

Wakinizengua nahamia kabisa kenya maana nshapewa na kiwanja kabisa na mkinizengua zaidi nabadili na uraia kabisa,shubaàaaàmit!
 
Huo wimbo mbona sio wa huko Tanzania ni wa huku Kenya, na kwa huku ruksa tu
 
Kama vipi Mondi ahamie tu nchi za nje awe anatuletea madude makali kama haya. Dunia ya leo mnapiga kelele na kichupa cha Mondi wakati wadada wa watu mnawachojoa kila siku na wengine mnachojolewa kama hamna akili nzuri. Kwanza maadili halisi ya Kiafrika ni wasichana vigoli kuacha matiti wazi na kuvaa kikamba tu kiuononi.
 
Video you tube imewekwa Age restricted,na sidhani kama Diamond kaipeleka hiyo video media yoyote ya Bongo maana anajua utafungiwa.

Huwezi shindana na utandawazi,huwezi zuia ndani wakati uchafu wa nje unaingia ndani.
 
Aaaaah jamani kama mumesoma vizuri kabla ya kuplay wimbo kuna maelezo yanajitoshereza na ndoo maana nyimbo iko YouTube tu
 
Anajiharibia local fanbase na bado ataendelea kulalamika ooo media za bongo hazipigi nyimbo za wasafi,Mbona nyimbo ya SIKOMI haina mbwembwe nyingi lakini hata views inazozaidi ya mil 11 alafu collabo na rickross hata mil 6 haijafika. jiongeze kaka unajiharibia mashabiki utaona kiba nyimbo atakayotoa haitakuwa na mbwembwe nying za wadada wakaa uchi na itapata air time kweny media,Alafu kweny hiyo nyimbo mpya kaharibu content kweny upande wa culture kwani masuala ya uchi sio ubeauty wa mdada wa kiafrika kama inavyotambulika,hayo mambo mwachie Jason na treysongz
 
Umenena,kwa level ya Diamond tusitegemee aimbe ngoma za kigogo au kinyakyusa ambapo mwanamke amevaa mavitenge kama anaenda kwa wakwe zake
 
Nipe tafsiri ya ujinga kijana?
Clubing song ulitaka wavae madela na ukizingatia umefanywa na mtanzania ila kwa watu wa dunia ambako huku kuonekana hivyo ni jambo la kawaida.
labda anataka avae mayenu na wadada wavae magauni marefu makubwaa na ushungi halafu wawe wamekaa kwenye viti wakiimba hizo rnb songs
 
Wakinizengua nahamia kabisa kenya maana nshapewa na kiwanja kabisa na mkinizengua zaidi nabadili na uraia kabisa,shubaàaaàmit!
bongo wachawi tupo tumejaa tele sema hatuna mavifaa tu kama maungo ya kurukia tunatafuta kwa udi na uvumba kumshusha mtu kimaisha tupate la kusema mitandaoni
 
Halafu huo wimbo ni wa Kenya na huko duniani sio Tanzania ambako kiongozi wake anafurahia wananchi wake kuishi kama mashetani....
 
Awe anaandika sasa specifications kuwa hii ni ya wabongo na hii kwa ajiri ya watu wa mataifa mengne ya nje (abroad)
Ujinga tu ndo mnaoendekeza maadili mmeyajulia wapi uhuni mnafanya gizani mnakuja malizia hasira zenu kwe sanaa fasihi hainaga matusi na hiyo ni aina ya kujieleza mbwembwe nyingi kufungia wasanii basi muwafungie na wa nje basi watu wanashusha kwe net
 
Mimi nampenda sana Diamond lakini huu wimbo kwakweli amepitilizanhata kama hategemei soko la nchini lakini si kweli uchi na utupu ndio vinauza zaidi hii video ina shida kabisa
 

Acheni uwongo na kuwa na fikra hasiii kiasi hcho "" mbona kuna video nyingi tu toka huko huko ulaya na amerca ambazo hazina viashiria vya ngono na nyimbo zao ziko hit mnooo ""


Hebu nionyeshe wimbo wowote wa eddy sheran ambao video yake inamaudhui ya wanawake waliokaa uchi "" au video zake naye ameziandaa kwaajili ya kuzionyesha afrivmca tu peke yake vipi kuhusu ile ngoma ya manya ya wizkid mbona hamna wacheza uchi mule au video imepangwa kuonyeshwa tanzania tu pekee"" vipi kuhusu fia ya davido..vipi kuhusu " loyalty ya kendrick vipi kuhusu humble ya kendrick .

Aiseeee ifikie hatua watu tubadilike na hizi fikra hasi kuwa kukaa uchi ndio uzungu sijui ustaa wakati hapo hapo tumeona huyo omarion video yake ameifanyia south africa tena eneo kubwa la shooting likiwa limefnyika mbugani na hakuna aliyekaa uchi vipi kuhusu french montana aliykuja kufnya video uganda na nyimbo yke kuwa hit pasipo kuwa na mademu walio uchi .


Serikali ikiwafungia mnadai kuwa mnaonewa ..kwanini msijikite kwenye kuwa mnaiga mambo mazuri tu pekee na yasiyo na faida mkaachana nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…