Kwa video hii, a boy from Tandale lazima ifungiwe

Sikio la kufa halina dawa,anaweza kujihisi anapanda chati kwa haraka lakini hajui kuwa anguko lake litakuwa nalo la haraka vilevile..
 
Tatizo BASATA inaishi nyakati tofauti na muziki wanaofanya vijana hawa....
 
ndo maana domo anatusua mond ni mnyamwezi yan macheni,mapete nn pamba Kali kwa sana sio ka yule mjinga anachanganya mziki na dini eti "nimezaliwa kwenye familia inayozingatia misingi ya dini"
 
ifungwe ili iweje mbona si wabongo wanafiki eti maadili maadili what a ****??basi zifungieni na za mamtoni!!fungieni mitandao ya ngono!kamateni Malaya wote tz!kamateni mademu woote wanaovaa vibaya barabarani...
Msanii ni kioo cha jamii, yeye ndo anayetakiwa kuibadilisha jamii kutoka kwenye uovu kuipeleka kwenye maadili. Sasa inapotokea msanii mkubwa kama Diamond kuanza kupromote ujinga wa kushusha maadili, hatuwezi kufumbia macho ujinga kama huwo.
 
Wimbo mzurii ..video ya kibabe hii ndo mwaga mboga nimwage kande
 
Msanii ni kioo cha jamii, yeye ndo anayetakiwa kuibadilisha jamii kutoka kwny uovu kuipeleka kwny maadili. Sasa inapotokea msanii mkubwa kama Diamond kuanza kupromote ujinga wa kushusha maadili, hatuwezi kufumbia macho ujinga kama huwo.
maadili gani bwana wewe??maadili bongo??mnazingua bwana mwacheni dogo afanye yake...!!maadili kitu gani??
 
Hivi kuonesha matiti nje kwa wanawake si ndo utamaduni wetu hasa wa Kiafrika? Ama maadili yetu ni ya wapi?
 
Hata Mond anajua Nyimbo itafungiwaa sema Ashazoeaaa maana BASATA ndo kazi wanayowezaaa kufungia nyimboo tuu...!! Mondi ni[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Hivi diamond ndo kuna Msikiti alikua anawajengea waislam kutokana kazi yake hii si ndio wandugu au?
 
Ndio maana uzinduzi kaenda kuufanyia Kenya[emoji3] [emoji3] [emoji3] muda si mrefu mtaanza kulia lia pale wakenya watakapoanza kusema Diamond ni msanii kutoka Kenya.

BASATA mfungieni huyo Mkenya[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
BASATA walete sababu za msingi za kufungia nyimbo za wabongo kwa kudai hazina maadili wakati hakuna sehemu wamewahi sema maadili ni yapi na kwa mtazamo wa nani. Video za nje full makalio wazi na zinapigwa kwny TV zetu. Kama kuweka nudity kwny video sio maadili wapige ban na video za nje.
Tulikubali utandawazi na haya ndo matokeo yake. Kama tunataka kuishi kama watanganyika ban video za nje zote af unaruhusu unazoona za bongo zina hayo so called maadili.
 
Kichupa kimesimama vizuri. .hongera kwake kijana.
 
Hivi kwenye dunia ya leo lipi jipya?....unafiki na roho mbaya.

Maadili ni parsonal issue na ni jambo mtambuka sana,fasihi haina mipaka na haina kazi ya kuleta au kubomoa maadili.
Unafikiri yeye akivaa mabwanga wewe nafamilia yako ndo mnapata maadili.

Mbona hayo matako na matiti tunayaona kila siku mitaani kwetu na hakuna kipya.... unafiki!
Kama unategemea diamond akusaidie upate maadili umechelewa sana....!!!
 
Msanii ni kioo cha jamii, yeye ndo anayetakiwa kuibadilisha jamii kutoka kwenye uovu kuipeleka kwenye maadili. Sasa inapotokea msanii mkubwa kama Diamond kuanza kupromote ujinga wa kushusha maadili, hatuwezi kufumbia macho ujinga kama huwo.
Unategemea msanii akuetee maadili....jiongoze mwenyewe acha kutegemea mtu akusaidie kuishi.

wabongo bwana.....eti hawaishi maisha yao bila kucopy kwa msanii au mtu maarufu....ni uzembe wa akili na kufikiri
 
Video ina mawazo finyu sana. Hivi, african beauty ni matiti na makalio ya wasichana tu?
Vipi mandhari za kuvutia kama ngorongoro, mlima kilimanjaro, maporomoko ya mto limpopo huko zimbabwe nk sio african beauty hiyo?
 
Si nilisikia ikifunguwa Audio na video pia na ikiwa video na audio zote ban. lakini si yuko mlezi wa group au sikusikia vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…