Kwa wadada zangu ambao waume zenu wakimya/wapole msiwafanye na kuwaona wajinga

Duu jamaa hakutaka kumuumiza mkewe physically bali alitaka kumuumiza kihisia,tena huyo binti kushika mimba ni kitu ambacho kitamtesa sana mkewe,daah ila mwana..............
Mwana kaanzisha familia mpya kisa kisasi..
 
Vizuri kama unasoma biblia. Kwa hiyo huyo mwanaume alichokifanya yeye ndo amepatia? Ndo katumia hekima?
 
Vizuri kama unasoma biblia. Kwa hiyo huyo mwanaume alichokifanya yeye ndo amepatia? Ndo katumia hekima?
Mimi sikusema alichokifanya ni vema, mimi nimezungumzia kitendo chenu chakupenda dramas na maswaibu pamoja na ubabe ilihali amani ni kitu chema. Pili sikumjibu mtoa mada bali nimekujibu point yako, kwanini uende mbali kuanzisha ugomvi ili mwisho wa siku mwanaume aje afanye kitu kibaya ili ukae njia sawa. It's pure stupidity!
 
kuna mzee moja alimwambia mkewe usiutumie upole wangu vibaya uvumilivu una mwisho wake
Dada zangu wengi hawajui ila wanaume ambao ni wapole wakipenda kweli kabisa, yani wanahakikisha mkewe anapata mahitaji yake yote ya msingi ila mara nyingi huwaga wana potezaga hizi bahati.

Washazoea kuzibuliwa kila mara,mitusi kila siku ,kufokeana, halafu baadae utawasikia "wanaume wote mbwa.......".
 
Hakika, kila jambo inabidi like Kwa kiasi kisicholeta Madhara kwa upande wowote ule
 
Kisasi kiko poa tu, hata angempa mwanamke wa nje ni poa tu coz ishu sio kumuumiza huyo jamaa anaekugongea. Hapo mpumbavu ni mke sio muuza duka.

Ukianza kudeal na anaochepuka nao utadeal nao mara ngapi kama mkeo ni kicheche.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…