Acheni tamaa na maisha ya purukushani, kama kuoa kunahitaji purukushani zisizona msingi basi haina maana. Kwelikweli unatamani purukushani maishani na kuanzisha maswaibu bila msingi, basi ni vema nikakaa pembeni nikuangalie tu. Sikuoa mtoto bali mtu mzima mwenzangu nikijua ni mtulivu ila ghafla unataka dramas, nivema nikatafute amani yangu. Wajua majukumu yako namimi nayajua yangu ila ghafla ukajigeuza akili, ni mpumbavu tu ndio awezaye kuyatenda hayo. Nahasira ya mtu mpole na mtaratibu ni mbaya sana, maana uchungu wake ni Mungu tu ajuaye ndani ya moyo wake. Usingemuigizia upole na utaratibu kipindi cha uchumba jua kwamba kamwe asingekuoa, ila mnaigiza baadae mwaja kubadilika, hiyo ni asili ya shetani. Ishi kwa amani na watu wote. Utulivu wangu wa akili (my peace of mind) ni bora zaidi kuliko ngono, maana ndicho kitaniwezesha kutunza wazazi wangu na kulea familia yangu kwakiwango kinachostahili. Ndio maana usifikiri single moms wataisha bali itaongezeka kwakuwa wanawake hutafsiri kuwa ubabe na kurukaruka ndio uanaume, mtazidi kuwaharibia hata vizazi vijavyo. Soma sana biblia, hili jambo limezungumziwa na madhara yake kutolewa.
Sent using
Jamii Forums mobile app