Kwa wadogo zangu wa kike na wakina dada kwa ujumla, tabia ya kujiachia mbele ya ndugu wa kiume tuwaachie Wazungu

Kwa wadogo zangu wa kike na wakina dada kwa ujumla, tabia ya kujiachia mbele ya ndugu wa kiume tuwaachie Wazungu

Kumbuka mwanaume anashawishika sio kwa hisia, bali kwa macho. Unavyovaa ndivyo chances za kuzidi kimvutia Me zitaongezeka au kupungua.

Mavazi kwa watoto ni muhimu yaangaliwe, hasa kunapokuwa na halaiki ya watu, tuwafunze kuvaa kwa stara. Hivi unavaaje chupi na khanga unapita mbele za watu?
Mtoa mada kaongelea nyumbani, watoto wa kike wavae sijui kujifunika mwili mzima.
Mimi kusema ukweli mwanaume hawezi nichagulia, aina ya vazi gani nivae. Sivai kwasababu yake navaa kwaajili yangu.
Ikiwa wewe kaka hapo nyumbani, ukanitamani dada yako mirembe inakuhusu.
Nimevaa hiyo khanga moja sana tu home, vigauni vifupi na sijabakwa sababu nilioishi nao wana akili timamu.
 
Mavazi siyo sababu ya mwanaume kubaka, kumnyanyasa kijinsia mtoto wa kike.
Acheni kupotosha na tamaa zenu, kwenye maonyesho moja ya unyanyasaji wa kijinsia, kuliwekuwepo na nguo ya mtoto wa miaka 2.

Wakasema wazi mtoto wa miaka 2, anahamasishaje mwanaume kuweza kumbaka? Kuanzia nguo na maumbile yake?
Ikahitimishwa nguo siyo kigezo, ni akili za mwendawazimu tu ndiyo anaweza kubaka.
Upande wangu navaa navyojisikia, nitakavyopenda. Ukishawishika utajijua mwenyewe mimi kwa raha zangu...
Hatuzumgumzii kubaka watoto hata wanaume wapo wanaolazimishwa na wanawake kufanyangono, kimaadili haijakaa sawa sema tu ni tunaamua kma ulivohitimisha lakini sio kusema ndo iwe uhalali wa mtoto wa kike kuvaa nusu uchi kimaadili haipo na wanaoongea ni wanaume wenye maumbile Yao sie sijui tunabisha nn 😀

Uthamani wa mwanamke pamoja na mwili wake mfano pika chakula acha wazi kutwa nzima na pia chakula kifunike kipo kinaonekana kina usalama Kwa walaji ndo uhalisia wa mwili wa mwanamke 🙏
 
Mtoa mada kaongelea nyumbani, watoto wa kike wavae sijui kujifunika mwili mzima.
Mimi kusema ukweli mwanaume hawezi nichagulia, aina ya vazi gani nivae. Sivai kwasababu yake navaa kwaajili yangu.
Ikiwa wewe kaka hapo nyumbani, ukanitamani dada yako mirembe inakuhusu.
Nimevaa hiyo khanga moja sana tu home, vigauni vifupi na sijabakwa sababu nilioishi nao wana akili timamu.
Mkuu, unaona kawaida coz ndivyo mlivyolelewa, yaani makuzi yenu yaliruhusu wewe kuvaa kanga au vigauni vifupi ukiwa na kaka zako, wazazi/walezi wako hawakuona kuwa ni tatizo lakini hilo ni tatizo kubwa sana, nisiwaseme vibaya waliohusika na malezi ila najua tu wazazi tunakosea sana. Kwa vile hakuna baya lililokukuta haimaanishi kuwa ulichokuwa unafanya ni sahihi, kwa vile uliolelewa nao waliizoea hali hiyo haimaanishi kuwa ni sawa.

Lakini kimakuzi na malezi kwa mtazamo wa wengi sio sawa.
 
Exactly
Mkuu, unaona kawaida coz ndivyo mlivyolelewa, yaani makuzi yenu yaliruhusu wewe kuvaa kanga au vigauni vifupi ukiwa na kaka zako, wazazi/walezi wako hawakuona kuwa ni tatizo lakini hilo ni tatizo kubwa sana, nisiwaseme vibaya waliohusika na malezi ila najua tu wazazi tunakosea sana. Kwa vile hakuna baya lililokukuta haimaanishi kuwa ulichokuwa unafanya ni sahihi, kwa vile uliolelewa nao waliizoea hali hiyo haimaanishi kuwa ni sawa.

Lakini kimakuzi na malezi kwa mtazamo wa wengi sio sawa
 
Back
Top Bottom