Muuza simu used
JF-Expert Member
- Aug 23, 2017
- 4,393
- 7,074
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha!kuna kaukweli kwa mbaaali hayo majamaa yanayojali maisha yao yana maendeleo mazuri sana kuliko wale wanaogawana na wenzao kidogo walicho nacho.Ni hapo swali langu linakuja kwa nn baraka ziende kwa limtu linalojijali lenyewe na familia take tu kuliko wale walio na moyo wa kusaidia ndugu zao na hats watoto wa jirani?Pasco Mayalla njoo utusaidie huku hivi ile karma huwa haiwaoni watu wanaosaidia wenzao?mbona hawana maisha mazuri licha ya kuwa wanajitoa sana kusaidia ndugu na jamaa zao?Roho mbaya (Protestant ethics):
Postpone enjoyments, be selfish, be frugal, invest, make more profits. Give good education to children. Focus on yourself na usitapanye pesa.
Roho nzuri (Christian values):
Toa ndugu, toa ndugu, toa ulicho nacho, kwani bwana ana kuona mpaka moyoni mwako. Usiwe na wasiwasi, kwamba utakula nn mezani kwa bwana Kuna chakula Cha uzima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama umeamua kujiunga na kamati ya roho mbaya jiunge tu kelele za nini ! Blueface[/U
Sent using IPhone X
[/QUOTE]
Hahaha!Sio hivyo mkuu!Mimi binafsi nimechukua roho ya kujitoa ambayo nimerithi kwa baba ambaye maisha yake ni ya kawaida japo kasaidia sana ndugu.Wasiwasi wangu naogopa nisijeishia maisha kama yake.Lakini kila nikikaza roho nipunguze kusaidia inashindikana yani ndugu akipata matatizo automatiki najikuta nasaidia tu!ndo mana nikauliza hilo swali
Hahaha!hapana malipo ya karma huanza hata bado ukiwa hai
Roho mbaya haikufikishi mahali popote mwisho wako utapasuka mara sabini, nimeelewa point ya kuweka akiba , lakini usi justify roho mbaya kwamba ina matunda mazuri, muhimu kwenye maisha tumia akili na moyo kwa pamoja.Japo sijatajwa kwenye uhenga hapo acha nijipendekeze tu.
Mwenye roho nzuri ni sawa na tenga la nyanya hata ulipeleke baharini au ziwani kuchotea maji haliwezi kujaa. Roho nzuri yao inawadidimiza hawaweki akiba.
Mwenye roho mbaya mbinafsi ni sawa na ndoo ukikinga maji yanajaa. Hawa mara nyingi wana uwezo mkubwa wa kuweka akiba. Wahenga walishasema akiba haiozi.
Sijapata jibu bado mkuu!Baraka za hawa watu wanaosaidia wenzao huwa zinaenda wapi?Kwa nn wabaki na maisha Yale ya kawaida halafu fun enough baadhi ya waliosaidiwa wanatoka nyuma na kua na maisha mazuri kuliko aliyewasaidia?Hivi kadiri unavyosaidia si ndo unabarikiwa au?Fikiria hata mfano wa Tanzania, nchi ilizozisaidia kupigania Uhuru zimetoka nyuma zimeipita kiuchumi kwa nn zile baraka zisingetufanya tuwe matajiri kuliko wao?kuna tatizo gani kwenye kusaidia?Maji ya mto humomonyoa miamba milaini tu. Same happens kwa watu nice. Watu wakishakujua
tu uko soft, basi hata shida ambazo wangetatua wenyewe wanakutwisha wewe.
Matokeo yake unabaki hapo hapo kuwa daraja la watu kupita na wakipita hawageuki nyuma.
Ndivyo tulivyo wanadamu. Kumbuka wale kenda walioponywa wakasepa zao akarudi 1 tu
kushukuru.
Hapo ulipo unajua kabisa nani ulimpitia simu anaweza akakupa hela na nani hawezi.
-better late than never, but never late is better-
Sawa kiongoziHakumaanisha utajiri wa fedha alimaanisha kujihesabia haki, soma biblia tangu Mwanzo hadi ufunuo utangundua Yesu hakufanya Kazi na maskini hata mmoja, pia kwenye agano la kale yeyote alieandikwa hakua maskini wote walijitosheleza kiuchumi ila walikua na kiu ya kumtumikia Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii mada imenifikirisha sana.. Thanks for a tagHili jambo nimekua nikilifikiria kwa miaka mingi bila majibu.Hata wewe hapo ulipo jaribu kuangalia katika familia au ukoo wenu. Unaweza kuta katika ukoo au familia ndugu yenu mwenye roho mbaya ndiye mwenye uwezo kifedha kuliko nyie wenye moyo wa kutoa. Katika jamii tunazoishi yaani wale watu wenye huruma na moyo wa kujitolea kwenye matatizo ya wenzao huwa na maisha magumu au ya kawaida sana.
Labda ungetegemea kwa kadiri mtu anavyosaidia wenzake ndo na yeye mambo yake yanyooke lakini inakua tofauti.Wapo watu wengi waliofirisika kwa kusaidia ndugu au marafiki mwisho wa siku wakajikuta wameishiwa kabisa. Mbaya zaidi wale waliosaidiwa huanza kuwacheka na kuwakejeli. Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.
Upande wa pili ukiangalia watu wenye roho mbaya na wabinafsi huwa wanafanikiwa sana pamoja na roho zao mbaya. Hawa ni wale watu ambao hawatoi msaada hata kama mtu anaumwa labda kwenye msiba ndo utawaona wanatoa misaada ya sifa.Kwa nini iko hivyo wakati tunaambiwa kwenye dini kadri unavyotoa ndivyo unapata zaidi? Kwa nini mwenye roho ngumu ndo afanikiwe kuliko mwenye roho nzuri? Majibu yenu tafadhali. Pascal Mayalla, Mshana Jr na wahenga wengine, nahitaji busara zenu huku.
Hahaha!Kaka mshana tusaidiane kupata majibu!Hii mada imenifikirisha sana.. Thanks for a tag
Jr[emoji769]
Nitakuja kamiliHahaha!Kaka mshana tusaidiane kupata majibu!
Sawa kaka nakuaminia najua ukizama chimbo utakuja na majibuNitakuja kamili
Jr[emoji769]
Naona unavunjika mbavu mkuu!Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app