Kwa wahenga tu: Kwanini watu wengi wenye roho nzuri huwa na maisha magumu au ya kawaida tu?

Kwa wahenga tu: Kwanini watu wengi wenye roho nzuri huwa na maisha magumu au ya kawaida tu?

Zuri au baya utakalowafanyia watu litakurudia kwa namna ambayo huwezi kutegemea.

Mwisho wa siku (alama utakayoacha kwa jamii) watu hawatakukumbuka kwa uzuri wa sura yako au umbo lako bali watakukumbuka kwa moyo wako na roho yako nzuri.

Tabia yako nzuri na matendo yako mazuri yataendelea kukufuata kokote uendapo katika dunia hii.
 
Zuri au baya utakalowafanyia watu litakurudia kwa namna ambayo huwezi kutegemea.

Mwisho wa siku (alama utakayoacha kwa jamii) watu hawatakukumbuka kwa uzuri wa sura yako au umbo lako bali watakukumbuka kwa moyo wako na roho yako nzuri.

Tabia yako nzuri na matendo yako mazuri yataendelea kukufuata kokote uendapo katika dunia hii.
Sawa mkuu ila swali langu ni kwa nn hao watu wenye roho nzuri na kujitolea huwa wengi wao wanamaisha magumu au ya kawaida tena wengine wanafirisika kwa kusaidia?Je wanavyotoa huwa hawapati baraka za kubadilisha maisha yao?
 
Hata mimi imenitokea hadi nikabadilisha namba ni sister yangu pekee ndio huniokoa nami pia nampiga tafu hata nikiwa na Hali mbaya... yaani kuna watu wapo tu kwa kusaidiwa ndio sababu kubwa... kwao hawajui kitu kusaidia utapigwa chenga za Messi hadi akili ikukae sawa.
Hahaha!
 
Sasa kwa nn tunahizwa kusaidia mkuu?

Hahaha!umeua mkuu!Sasa tutafanyaje mana Dino zinataka tusaidiane kiasi kwamba aliye na nguo mbili ampe moja jirani yake sasa ukiwa selfish INA maana uko nje ya dini.Jambo la ajabu hao wasiofuata hayo maagizo ya kusaidiana ndio wanawin maisha.Hapo ndo kichwa kinauma kiasi cha kuuliza hilo swali kwa nn watu wengi wenye roho nzuri hawawin kama wale wenye roho mbaya au ngumu?
Usifuate dini inayofundisha kile isichokiishi.

Niambie kanisa au msikiti gani unaojitoa kwa sehemu kubwa kuwasaidia waumini wake kifedha? Wengi wanataka mtoe nyie ila wao ni wagumu sana kuwapa wahitaji.

Mimi mimeshaamua nitakupa kile unachonipa. Ukinipa maombi nitashukuru na kukuombea pia.
Ukinipa mali na fedha nitajitahidi fadhira yangu pia ionekane kwa njia hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna msemo unasema, "tenda wema nenda zako usingoje shukrani" lakini nakumbuka kwa nyakati tofauti, nimewahi kuwasaidia watu wangu wa karibu pale walipokuwa wamekwama.

Kikaja kipindi fulani nikapitia Majanga makubwa kila nilipopiga hodi kuomba Msaada niliambulia ahadi tu. Niliteseka sana lakini hakuna ambaye alinyosha mkono wake kunisaidia

Nilijitutumua mwenyewe, nashukuru Mungu alinipigania.

Kwanini watu wengi wanaotoa msaada kwa upande wao hua ngumu sana kupata msaada wakiwa na shida?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mitihani tu ya maisha ndg

Kila mmoja hupitia katika maisha haya ili kukufunza jinsi ya kuishi na kumtegemea Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu ila swali langu ni kwa nn hao watu wenye roho nzuri na kujitolea huwa wengi wao wanamaisha magumu au ya kawaida tena wengine wanafirisika kwa kusaidia?Je wanavyotoa huwa hawapati baraka za kubadilisha maisha yao?
Tafsiri ya maisha mazuri ipo tofauti kwa mtu na mtu, mwengine mpaka awe na pesa, mtoto, gari, shamba na nyumba (pesa kiasi gani?, watoto wangapi?, magari mangapi au gari la aina gani? shamba heka ngapi? nyumba ngapi au nyumba iwe sehemu gani au nyumba yenye ukubwa gani? majibu yatatofautiana kwa sababu binadamu hatufanani kama vidole vya mkono.

Mwengine tafsiri yake ya maisha mazuri ni kuishi maisha yenye upendo, utulivu, amani, afya na utajiri wake ni maisha yanayompendeza Mungu pamoja na kusaidia watu.

Unaweza kuyaona maisha yake ni ya kawaida kulinganisha na maisha ya mtu mwengine. Lakini watu wanaishi kutokana na malengo waliyojiwekea na maisha ambayo wameamua kuishi.

Binadamu tunategemeana, huwezi kuishi bila binadamu wenzako. Wewe unamsaidia huyu na yeye anaweza akakusaidia wewe kama malipo au atamsaidia mwengine mbele ya safari yake
 
Ebu fanya utafiti wako vizuri maana kuna wengi tu wenye mioyo ya kusaidia na wamefanikiwa na bado wanasaidia wengine.

Mimi ni mfano mzuri wa mmoja wapo wenye moyo ya kusaidia na pia nimefanikiwa.

Sidhani kama ukiwa na roho ngumu ya kuto kusaidia watu ndiyo utafanikiwa. Pengine uwenda hizo pesa unazo save na kuacha kusaidia watu ukatumia pabaya zaidi labda kunywa pombe au starehe zingine lakini kama ni uwekezaji basi ntasema iyo myth iko sahisi kwa mantikiya kubana pesa na kuwekeza.

Nawasihi wahenga tusaidiane jamani hapa duniani tunapita tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli dunia ina mitihani mengi. Kuna nyakati bila kushikwa mkono maisha yanakua machungu sana.

Tujitahidi kufanya kazi ili tupate chetu bila kulazimika kuwapigia watu magoti kwani manyanyaso ya kuomba uumiza sana.

Ila tukikwama , usiche kutoka na kupaza sauti kwa ndg na rafiki kuomba msaada. Mungu utumia watu kujibu mahitaji yetu.

Kumbuka ukiona mtu hajakusaidia usimulaumu, usipokufa yuko aliyeandaliwa kukutoa kwenye janga hilo. Subira na uvumilivu ni nguvu amabayo kila mja anapaswa kuwa nayo.

Kwa upande mwingine, kujenga tabia ya kusaidia ni njema sana kwani unaweza usitambue ila ni moja ya huduma kubwa sana kupunguza maumivu ya maisha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli tenda wema nenda zako.

Kama ukiwa unataka return kwa ulio watendea basi wewe ukuwa unasaidia ulikuwa una wekeza.

Mara nyingi au zote ulio wasaidia siyo wao watakao kuja kukusaidia watakao kusaidi ni wengine tofauti.

Kwahiyo ukiwa na shida usi walilie wale ulio wahi kuwasaidia tafuta mtu tofauti kabisa na atakupa msaada.

Mdau mimi naamini hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vyema ndg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vyema ndg

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini ndugu hata dini inatushauri tuwekeze kwa Mungu kupitia sadaka na matendo mema.Sikumbuki ni injili ipi ila kuna mstari YeNsu anasema palipo hazina yako ndipo roho yako itakua tena tuweke akiba zetu kwa Mungu ambapo nondo na wezi hawafiki?Sasa kwa nn unasema kumsaidia mtu sio kuwekeza?waswahili wanasema wema hauozi maana yake nn?Natoa wito wale mliosaidiwa mnawajibu wa kimaadili kuwakumbuka waliowasaidia
 
Nimekupata mkuu!Ila nilitaka kujua kwa kadiri ya mafundisho ya Dini na kijamii tunafundishwa unaposaidia ndo unapata baraka nyingi ila naona watoaji wengi maisha yao yapo kawaida tu nikadhani wale wenye uwezo wasiotoa watapata laana wafilisike wawe maskini lakini kadiri wanabyokuwa wabahili na roho mbaya ndo Mali zao zinaongezeka!
Kwenye dini kuna mawili kwa watu wenye taswira ya watoaji wa sampuli uliyotolea mfano.
-Awe na subira Mungu hadanganyi kwenye ahadi zake.
-Arekebishe usaidiaji wake.
•Kuna wengine ni rahisi kusaidia lakini anasaidia kwa masimango
•Asisaidie kwa majivuno kuwa ona mimi ndiye msaidiaji.
•Asisaidie kwa kutaraji aonekane mwema kwa watu.
•Asisaidie mkono wa pili ujue.

Afanye hivyo, ataona mabadiliko.

Mambo ya pesa na mali kuongezeka yana mengi. Kila mtu na siri yake.
 
Hili jambo nimekua nikilifikiria kwa miaka mingi bila majibu.Hata wewe hapo ulipo jaribu kuangalia katika familia au ukoo wenu. Unaweza kuta katika ukoo au familia ndugu yenu mwenye roho mbaya ndiye mwenye uwezo kifedha kuliko nyie wenye moyo wa kutoa. Katika jamii tunazoishi yaani wale watu wenye huruma na moyo wa kujitolea kwenye matatizo ya wenzao huwa na maisha magumu au ya kawaida sana.

Labda ungetegemea kwa kadiri mtu anavyosaidia wenzake ndo na yeye mambo yake yanyooke lakini inakua tofauti.Wapo watu wengi waliofirisika kwa kusaidia ndugu au marafiki mwisho wa siku wakajikuta wameishiwa kabisa. Mbaya zaidi wale waliosaidiwa huanza kuwacheka na kuwakejeli. Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.

Upande wa pili ukiangalia watu wenye roho mbaya na wabinafsi huwa wanafanikiwa sana pamoja na roho zao mbaya. Hawa ni wale watu ambao hawatoi msaada hata kama mtu anaumwa labda kwenye msiba ndo utawaona wanatoa misaada ya sifa.Kwa nini iko hivyo wakati tunaambiwa kwenye dini kadri unavyotoa ndivyo unapata zaidi? Kwa nini mwenye roho ngumu ndo afanikiwe kuliko mwenye roho nzuri? Majibu yenu tafadhali. Pascal Mayalla, Mshana Jr na wahenga wengine, nahitaji busara zenu huku.
Mwenye roho mbaya anafanya lolote ili afanikiwe, mcha Mungu hathubutu
 
Lakini ndugu hata dini inatushauri tuwekeze kwa Mungu kupitia sadaka na matendo mema.Sikumbuki ni injili ipi ila kuna mstari YeNsu anasema palipo hazina yako ndipo roho yako itakua tena tuweke akiba zetu kwa Mungu ambapo nondo na wezi hawafiki?Sasa kwa nn unasema kumsaidia mtu sio kuwekeza?waswahili wanasema wema hauozi maana yake nn?Natoa wito wale mliosaidiwa mnawajibu wa kimaadili kuwakumbuka waliowasaidia
Unaposaidia lengo ni kuondoa kizingiti kinachomzuia mtu kufikia sehemu fulani, ni kumuwezesha pasipo kutaraji malipo.

Ukiwekeza ni kuwa unataraji ulichokiwekeza kikuletee faida zaidi. Hii ni biashara tayari.

Ulichoambiwa ukifanye hapo juu ni kuwekeza kwa Mungu. Ni kufanya biashara na yeye mwenyewe Mungu. Biashara yenyewe ni kufanya wema. Maadamu yeye ndiye muwekezaji mkuu faida utaipata kutoka kwake.

Wewe usihangaike na bidhaa (binadamu) ulipowekeza pesa zako. Hangaika na uliyoingia naye ubia. Faida utaipata kutoka kwake yeye maadamu ndiye aliyekuambia iwe hivyo wekeza kwake.

Ukihangaika na bidhaa (binadamu) itakushughulisha hii bidhaa ina mengi! Utajawa na ghadhabu, chuki na unaweza ukawa na kisasi.

Lakini biashara ni mapatano. Ni muhimu kuyaelewa na yule unayeingia naye ubia ili ufaidike naye.
 
Japo sijatajwa kwenye uhenga hapo acha nijipendekeze tu.

Mwenye roho nzuri ni sawa na tenga la nyanya hata ulipeleke baharini au ziwani kuchotea maji haliwezi kujaa. Roho nzuri yao inawadidimiza hawaweki akiba.

Mwenye roho mbaya mbinafsi ni sawa na ndoo ukikinga maji yanajaa. Hawa mara nyingi wana uwezo mkubwa wa kuweka akiba. Wahenga walishasema akiba haiozi.
Kula kongole. Nimekupenda bureeeeeh. Chukua kinywaji nakuja kulipia.
Kutaka kupendwa na kila mtu ni njia ya kupoteza.
Angalia dereva yule yule taxi ya muhindi akikosa hesabu anakopa apeleke. Kama bosi mswahili basi anakwenda na maneno kibao. Agressiveness ina nafasi muhimu sana kwenye baadhi ya biashara. Ila wale wakucheka cheka wabaki reception na customer services.
 
Back
Top Bottom