Kwa wahenga tu: Kwanini watu wengi wenye roho nzuri huwa na maisha magumu au ya kawaida tu?

Hahaha!kuna kaukweli kwa mbaaali hayo majamaa yanayojali maisha yao yana maendeleo mazuri sana kuliko wale wanaogawana na wenzao kidogo walicho nacho.Ni hapo swali langu linakuja kwa nn baraka ziende kwa limtu linalojijali lenyewe na familia take tu kuliko wale walio na moyo wa kusaidia ndugu zao na hats watoto wa jirani?Pasco Mayalla njoo utusaidie huku hivi ile karma huwa haiwaoni watu wanaosaidia wenzao?mbona hawana maisha mazuri licha ya kuwa wanajitoa sana kusaidia ndugu na jamaa zao?
 
Maji ya mto humomonyoa miamba milaini tu. Same happens kwa watu nice. Watu wakishakujua

tu uko soft, basi hata shida ambazo wangetatua wenyewe wanakutwisha wewe.

Matokeo yake unabaki hapo hapo kuwa daraja la watu kupita na wakipita hawageuki nyuma.

Ndivyo tulivyo wanadamu. Kumbuka wale kenda walioponywa wakasepa zao akarudi 1 tu

kushukuru.

Hapo ulipo unajua kabisa nani ulimpitia simu anaweza akakupa hela na nani hawezi.

-better late than never, but never late is better-
 
Roho mbaya haikufikishi mahali popote mwisho wako utapasuka mara sabini, nimeelewa point ya kuweka akiba , lakini usi justify roho mbaya kwamba ina matunda mazuri, muhimu kwenye maisha tumia akili na moyo kwa pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijapata jibu bado mkuu!Baraka za hawa watu wanaosaidia wenzao huwa zinaenda wapi?Kwa nn wabaki na maisha Yale ya kawaida halafu fun enough baadhi ya waliosaidiwa wanatoka nyuma na kua na maisha mazuri kuliko aliyewasaidia?Hivi kadiri unavyosaidia si ndo unabarikiwa au?Fikiria hata mfano wa Tanzania, nchi ilizozisaidia kupigania Uhuru zimetoka nyuma zimeipita kiuchumi kwa nn zile baraka zisingetufanya tuwe matajiri kuliko wao?kuna tatizo gani kwenye kusaidia?
 
Ni siyo roho nzuri wala mbaya...

Pale unapotoa je wewe mwenyewe unabakiwa na akiba...

Kama hapana, je baada ya kutoa itakuchukua muda gani kujirejeshea tena... Hapa sasa ndipo linapokuja swala la kufulisika...


Cc: mahondaw
 
Sawa kiongozi
 
Nasikia wanasema moja ya mbinu za utajiri ni ubahili.
 
Hii mada imenifikirisha sana.. Thanks for a tag

Jr[emoji769]
 
Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unavunjika mbavu mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…