supermarket
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 7,453
- 10,952
Sawa mkuu ila swali langu ni kwa nn hao watu wenye roho nzuri na kujitolea huwa wengi wao wanamaisha magumu au ya kawaida tena wengine wanafirisika kwa kusaidia?Je wanavyotoa huwa hawapati baraka za kubadilisha maisha yao?Zuri au baya utakalowafanyia watu litakurudia kwa namna ambayo huwezi kutegemea.
Mwisho wa siku (alama utakayoacha kwa jamii) watu hawatakukumbuka kwa uzuri wa sura yako au umbo lako bali watakukumbuka kwa moyo wako na roho yako nzuri.
Tabia yako nzuri na matendo yako mazuri yataendelea kukufuata kokote uendapo katika dunia hii.
Hahaha!Hata mimi imenitokea hadi nikabadilisha namba ni sister yangu pekee ndio huniokoa nami pia nampiga tafu hata nikiwa na Hali mbaya... yaani kuna watu wapo tu kwa kusaidiwa ndio sababu kubwa... kwao hawajui kitu kusaidia utapigwa chenga za Messi hadi akili ikukae sawa.
Usifuate dini inayofundisha kile isichokiishi.Sasa kwa nn tunahizwa kusaidia mkuu?
Hahaha!umeua mkuu!Sasa tutafanyaje mana Dino zinataka tusaidiane kiasi kwamba aliye na nguo mbili ampe moja jirani yake sasa ukiwa selfish INA maana uko nje ya dini.Jambo la ajabu hao wasiofuata hayo maagizo ya kusaidiana ndio wanawin maisha.Hapo ndo kichwa kinauma kiasi cha kuuliza hilo swali kwa nn watu wengi wenye roho nzuri hawawin kama wale wenye roho mbaya au ngumu?
Mitihani tu ya maisha ndgKuna msemo unasema, "tenda wema nenda zako usingoje shukrani" lakini nakumbuka kwa nyakati tofauti, nimewahi kuwasaidia watu wangu wa karibu pale walipokuwa wamekwama.
Kikaja kipindi fulani nikapitia Majanga makubwa kila nilipopiga hodi kuomba Msaada niliambulia ahadi tu. Niliteseka sana lakini hakuna ambaye alinyosha mkono wake kunisaidia
Nilijitutumua mwenyewe, nashukuru Mungu alinipigania.
Kwanini watu wengi wanaotoa msaada kwa upande wao hua ngumu sana kupata msaada wakiwa na shida?
Sent using Jamii Forums mobile app
Tafsiri ya maisha mazuri ipo tofauti kwa mtu na mtu, mwengine mpaka awe na pesa, mtoto, gari, shamba na nyumba (pesa kiasi gani?, watoto wangapi?, magari mangapi au gari la aina gani? shamba heka ngapi? nyumba ngapi au nyumba iwe sehemu gani au nyumba yenye ukubwa gani? majibu yatatofautiana kwa sababu binadamu hatufanani kama vidole vya mkono.Sawa mkuu ila swali langu ni kwa nn hao watu wenye roho nzuri na kujitolea huwa wengi wao wanamaisha magumu au ya kawaida tena wengine wanafirisika kwa kusaidia?Je wanavyotoa huwa hawapati baraka za kubadilisha maisha yao?
Ni kweli dunia ina mitihani mengi. Kuna nyakati bila kushikwa mkono maisha yanakua machungu sana.Ebu fanya utafiti wako vizuri maana kuna wengi tu wenye mioyo ya kusaidia na wamefanikiwa na bado wanasaidia wengine.
Mimi ni mfano mzuri wa mmoja wapo wenye moyo ya kusaidia na pia nimefanikiwa.
Sidhani kama ukiwa na roho ngumu ya kuto kusaidia watu ndiyo utafanikiwa. Pengine uwenda hizo pesa unazo save na kuacha kusaidia watu ukatumia pabaya zaidi labda kunywa pombe au starehe zingine lakini kama ni uwekezaji basi ntasema iyo myth iko sahisi kwa mantikiya kubana pesa na kuwekeza.
Nawasihi wahenga tusaidiane jamani hapa duniani tunapita tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vyema ndgKweli tenda wema nenda zako.
Kama ukiwa unataka return kwa ulio watendea basi wewe ukuwa unasaidia ulikuwa una wekeza.
Mara nyingi au zote ulio wasaidia siyo wao watakao kuja kukusaidia watakao kusaidi ni wengine tofauti.
Kwahiyo ukiwa na shida usi walilie wale ulio wahi kuwasaidia tafuta mtu tofauti kabisa na atakupa msaada.
Mdau mimi naamini hivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini ndugu hata dini inatushauri tuwekeze kwa Mungu kupitia sadaka na matendo mema.Sikumbuki ni injili ipi ila kuna mstari YeNsu anasema palipo hazina yako ndipo roho yako itakua tena tuweke akiba zetu kwa Mungu ambapo nondo na wezi hawafiki?Sasa kwa nn unasema kumsaidia mtu sio kuwekeza?waswahili wanasema wema hauozi maana yake nn?Natoa wito wale mliosaidiwa mnawajibu wa kimaadili kuwakumbuka waliowasaidia
Kwenye dini kuna mawili kwa watu wenye taswira ya watoaji wa sampuli uliyotolea mfano.Nimekupata mkuu!Ila nilitaka kujua kwa kadiri ya mafundisho ya Dini na kijamii tunafundishwa unaposaidia ndo unapata baraka nyingi ila naona watoaji wengi maisha yao yapo kawaida tu nikadhani wale wenye uwezo wasiotoa watapata laana wafilisike wawe maskini lakini kadiri wanabyokuwa wabahili na roho mbaya ndo Mali zao zinaongezeka!
Mwenye roho mbaya anafanya lolote ili afanikiwe, mcha Mungu hathubutuHili jambo nimekua nikilifikiria kwa miaka mingi bila majibu.Hata wewe hapo ulipo jaribu kuangalia katika familia au ukoo wenu. Unaweza kuta katika ukoo au familia ndugu yenu mwenye roho mbaya ndiye mwenye uwezo kifedha kuliko nyie wenye moyo wa kutoa. Katika jamii tunazoishi yaani wale watu wenye huruma na moyo wa kujitolea kwenye matatizo ya wenzao huwa na maisha magumu au ya kawaida sana.
Labda ungetegemea kwa kadiri mtu anavyosaidia wenzake ndo na yeye mambo yake yanyooke lakini inakua tofauti.Wapo watu wengi waliofirisika kwa kusaidia ndugu au marafiki mwisho wa siku wakajikuta wameishiwa kabisa. Mbaya zaidi wale waliosaidiwa huanza kuwacheka na kuwakejeli. Nimeona mfano huo kwa baba yangu. Tangu tukiwa wadogo ndugu wengi walikuwa wakija pale nyumbani na kusaidiwa hadi ada za shule kwa wale waliokua wanasoma. Sasa imepita miaka mingi maisha yake ni yaleyale, wale waliosaidiwa wengi wapo kimya tena baadhi wako ulaya lakini hata kupiga simu kutoa salamu ni mtihani.
Upande wa pili ukiangalia watu wenye roho mbaya na wabinafsi huwa wanafanikiwa sana pamoja na roho zao mbaya. Hawa ni wale watu ambao hawatoi msaada hata kama mtu anaumwa labda kwenye msiba ndo utawaona wanatoa misaada ya sifa.Kwa nini iko hivyo wakati tunaambiwa kwenye dini kadri unavyotoa ndivyo unapata zaidi? Kwa nini mwenye roho ngumu ndo afanikiwe kuliko mwenye roho nzuri? Majibu yenu tafadhali. Pascal Mayalla, Mshana Jr na wahenga wengine, nahitaji busara zenu huku.
Unaposaidia lengo ni kuondoa kizingiti kinachomzuia mtu kufikia sehemu fulani, ni kumuwezesha pasipo kutaraji malipo.Lakini ndugu hata dini inatushauri tuwekeze kwa Mungu kupitia sadaka na matendo mema.Sikumbuki ni injili ipi ila kuna mstari YeNsu anasema palipo hazina yako ndipo roho yako itakua tena tuweke akiba zetu kwa Mungu ambapo nondo na wezi hawafiki?Sasa kwa nn unasema kumsaidia mtu sio kuwekeza?waswahili wanasema wema hauozi maana yake nn?Natoa wito wale mliosaidiwa mnawajibu wa kimaadili kuwakumbuka waliowasaidia
Umenena vyemaaaYesu alivyosema ni Rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuona ufalme wa Mungu Ulielewaje mkuu?
Kula kongole. Nimekupenda bureeeeeh. Chukua kinywaji nakuja kulipia.Japo sijatajwa kwenye uhenga hapo acha nijipendekeze tu.
Mwenye roho nzuri ni sawa na tenga la nyanya hata ulipeleke baharini au ziwani kuchotea maji haliwezi kujaa. Roho nzuri yao inawadidimiza hawaweki akiba.
Mwenye roho mbaya mbinafsi ni sawa na ndoo ukikinga maji yanajaa. Hawa mara nyingi wana uwezo mkubwa wa kuweka akiba. Wahenga walishasema akiba haiozi.