KWA WAHENGA TU: Mara ya kwanza kuona TV/ Video/ Sinema ilikuwa mwaka gani na ulijisikiaje?

Mimi acha nisimulie mkasa wa rafiki yangu ingawa yeye issue yake ni tofauti, yeye alipanda gari mara ya kwanza akiwa tayari anajitambua kabla ya hapo hajawahi ona hata gari inatembeaje aisee.

Kwanza kabisa alipokuwa ndani ya gari yeye aliona gari huwa inateleza tu kwa jinsi miti na vitu vinaonekana ukiwa ndani ya gari..

Alipofika nyumbani alishindwa kulala kabisa aliona kama kitanda kinaleteleza(kinatembea kama gari) na akikaa kwenye kiti anaona hivyohivyo..
 
Mimi cinema ya kwanza kuona ni ya Yesu niliona ni true kabisa hata alivyouwa na watu walilia sana tuliokuwa uwanjani niliona waroma siyo watu
 
Sijui mara ya kwanza ila nakumbuka kitaa tv zilikuwa kibao yaani maana tulikuwa na wazee wa bandari wanakaa mitaa iyo Tanga mjini hyo

Kwingine uwanja wa mzalendo hapo vipaji vyote ya Tanga wasanii wacheza mpira ndo maskini yao na kwetu ilikuwa kama km moja na Miata kadhaa palikuwa raha ya matukio makubwa kama ngumi na kifo cha nyerere yanaonyeshwa hapo sometime pakuja band wakina luiza mbutu enzi izo zamani kidogo ili Tanga ni uwanja wa burudani

Baada ya kuondoka nikaja sikia meya sijui kisauji kauza uwanja kwa mashia wanaugeuza sehemu ya kuzikia

Kwingine ukumbuki mkubwa ulikuwa Africa mashariki pale karibu na old Tanga kitambo sana yaani
 
Hiyo inaitwa nyakati, watoto wetu na wao watakuja kushangaza kwamba baba zao kwa mara ya kwanza walishika smartphone wakiwa na miaka 20
 
Nilikuw napend san matangaz ya zamani

Achen tu 🤣
 
Kwa mimi mara ya kwanza sikuona Tv kwa macho, bali niliipapasa kwa mkono kupitia tundu la kwenye box lake. Ilikuwa ni Hitachi inch 20 ya mwaka 2000. Hii ilitokana mshua alinunua huko mjini akaiagizia ije nyumbani apo ndo ikakutana na mimi. Jamani niliipapasa sana kama masaa manne hivi.

Na pia nilikuwa nainusaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…