Uongo katika mzungumzo ni sifa mojawapo ya alama ya unafiki, hivyo inabidi tung’ang’ane ili tuondoe sifa hiyo katika maisha yetu. Allaah Aliyetukuka Amehimiza sana sifa hiyo pale Aliposema: “Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli” (9: 119). Hii ni sifa ambayo inamwingizaa sahibu wake Peponi: “…na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli…Allaah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa” (33: 35).
Hadithi hizi mbili muhimu toka kwa mjumbe wa mwenyezi mungu
1.Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Bila shaka, ukweli ni wema, na wema unampeleka (mtu) Peponi. Hakika uongo ni uovu, na uovu unampeleka (mtu) motoni”
2.Amesema tena:
“chungeni sana kuhusu ukweli na ikhlasi, kwani ukweli na ikhlasi inaongoza kwenye wema, na wema unaongoza Peponi”