Mambo yanasonga na dunia inabadilika.
Kama tuliweza kukaa na kujadili tunafanyeje kuhusu masuala ya ndoa na ubatizo wa watu wale, basi tunaweza kukaa na kujadili kuboresha mambo mbalimbali.
Siamini kama maelekezo yote yanatoka top down tu. Naamini yanaweza pia kutoka down up. Maji yakapanda mlima!!
Na kutokana na viongozi wakubwa kwa baadhi ya dini kutokuoa basi ni muhimu zaidi kusikiliza mapendekezo toka kwa walio field mojakwa moja. Kama jeshini tu.
Oneni. Katika kiapo kilichopo, kinachovuma makanisani kina mapungufu. Ukitulia ukachunguza unaona ni kama kujinenea laana iliyofichwa katika baraka za hapa na pale.
1. Tunapaswa kuamua kuwa tunachotaka katika ndoa yetu sio shida na raha (sa ndo nn) bali tunaitaka furaha tunapopitia yote ya maishani
2. Tunapaswa kuamua kujiombea maisha ya milele na sio kukipa promo kifo, ati kitutenganishe. Unajuaje kama hakuna uwezekano tukawa mabest hata huko mbinguni.
3. Umaskini na utajiri kwanza hata haimake sense.
4. Tuitake afya na tuwe na shukrani maana hata magonjwa mengi ni matokeo ya kuwa na afya. Hivyo tukubaliane kuitunza zaidi. You are never a sick person trying to regain health. You are a healthy person keeping it that way and fighting diseases (Imetoholewa toka kwa Mazed Charahani)
Ebu soma kwa utulivu hiki kiapo:
View attachment 2835614
Sie waamini, wenye imani. Ni kwa nini tusijinenee mema kila wakati. Tunaweza kuiacha kusema waziwazi. Tukaziacha imejificha hizo laana za kifo, shida, magonjwa na umasikini. Tukasisitiza zaidi katika baraka za
furaha, afya na utajiri🤔
Nisiwachoshe sana pendekezo lenyewe hili hapa:
View attachment 2835616
Ps: Kwa makanisa ya kiroho, ya manabii na mitume ambao ndio maaskofu haohao naomba mlitafakari halafu muwe wa kwanza kuifanya hiyo reform. Hamnaga bureaucracy nnajua. Roho wa Bwana akaseme nanyi🙏
Muwe na siku njema