Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Ila naomba maelekezo unaishije nae kijanja...Mimi nashindwa kabisa kujizuia najikuta sitaki kabisa mawasiliano yoyote na yeye...ebu nifundishe unavyo ishi na mzazi wako
Mimi huwa nawasiliana nae kunapotokea ulazima kabisa wa kufanya hivyo. Pia nina msimamo kwamba nitakusadia ninavyoweza ila sitaki shinikizo wala ushawishi. Kama ni YES ni YES na kama ni NO ni NO. Mwanzoni ilikuwa utata ila baadae wakaelewa kwasababu pia huwa ikiwa YES huwa sipindishi natimiza. Unajua shida kubwa sana kwa wengi wetu ni ukorofi wa wazazi uliokutana na hali duni (umaskini)... wazazi wengi wana hasira sana kwamba hawasaidiwi na watoto wao huku wakijisahaulisha kuwa kila mwanaume/mwanamke ataachana na wazazi wake na kuambatana na mkewe/mumewe.
 
Mimi mzazi wangu Bado ni mtumishi...juzi TU hapo amepandishwa tena cheo japo muda wa kustaafu kwake umekaribia...ila kiukweli Mimi Bado najitafuta kimaisha sijawahi kumlilia shida akanisaidia Hadi Huwa najiuliza pengine sio mzazi wangu...nilipo gundua kuwa Hana msaada na Mimi...niliamua kufocus na maisha yangu japo Bado sijayapatia ila ni kitambo sana sijamlilia shida...last time nilikuwa Nina shida ya laki 3 mfukoni nilikuwa na kama 220k nikamwambia mzee Nina shida ila Bado kama elfu 80 hivi....alicho nijibu kilinitoa machozi harafu ilikuwa ni shida muhimu sana maana wife alilazwa hivyo ilikuwa ni bill ya hospital...baba alikataa katakata kunisaidia...nikaamua kuachana nae...hivi sasa Nina mawazo ya kuhama nchi Mimi na watoto wangu...ili niepukane na huyu mzee kwani Najua TU baada ya yeye kustaafu atataabika TU...Hilo lipo wazi wastaafu Huwa wanaponda raha miaka mitatu TU...
 
Kama umelelewa vizuri huwezi elewa vile watu wanapitia. Nimesoma visa vingi hapa nikamshukuru Mungu kwamba sikuwahi pitia waliyoyapitia. Familia yetu haina ugomvi hata chembe tunaishi peace sana.
Pole kwa wate wanaopitia changamoto na wazazi wao.
Hongera sana, Lucky you
 
Kusaidiana bado haifukii dhana ya mfumo dume. Mwanaume hataki kutumia anachokipata na familia, anataka mke aendelee kumnyenyekea aombe kila shillingi inapelekea watoto kutokusomeshwa shule kwa amani maana ada hazilipwi, so mke anapoamua kupambana ili aje asomeshe wanae mwenyewe mwanaume anaibus sasa kwamba yeye ni mwanaume ila mwanamke anataka kumpanda kichwani. Anashindwa kusema kwamba kwanini atafte kazi nzuri inanishushia uanaume wangu. Wewe kama hayajakukuta usikatae nnachokusimulia. Kama hukielewi
Bora ukatulia maana wanaume mnateteanaga ila wake zenu wanakufa na vitanzi vya kila aina
 
Hongera kwa ujasiri
 
Sidhani kama core point ya mada yangu ilikua mzazi kumtegemea mtoto
Hii inafanana na story ya maisha yangu. Mama yangu alikuwa hanipendi tangu nikiwa mtoto. Na hadi nilijua na marehemu bibi yangu ambaye alinipenda sana kuna kipindi aliwahi sema sijui kwanini mama yako hakupendi na mimi wala siwezi sema chochote hii kauli inatembea sana masikioni mwangu kila wakati.

Wakati nakua mama aliwapenda na hata sasa anawapenda sana wadogo zangu kuliko mie, anawashirikisha zaidi wao kuliko mie. Na hata kuna kipindi aliugua sana karibu kufa akagawa mali kwa wadogo zangu wote kasoro mie. Mama yangu yeye ukiona anakuwa karibu na wewe kipindi hicho kuna kitu anataka kwako akishakamilisha anakutakana. Imekuwa hivyo kwenye life langu. Nimekuwa nikijishusha lakini wapi. Ananiombea mabaya wakati wote, sema huwa nasema Mungu siyo mzungu, anapima kila jambo. Right laana zingekuwa rahisi basi ningekuwa Nisha kufa muda mrefu. Nimejitajidi sana kuwa beba wadogo zangu nawasomesha lakini hata Sipati reward. Anawatumia wadogo zangu hao hao kunihujumu.

Kwa kweli imefika mahali nimeamua kunyamaza coz naona naumia bure mahali ambapo sipendwi. Si kwamba huduma sita peleka nitaendelea kutuma huduma kama kawaida. Lakini kuwa karibu kabisa kwa kweli hapana. Nimeamua hata nyumbani kwa sasa sitakanyaga.

Mama ni mtu anataka kukuendesha, right ningekuwa namsikiliza ndoa yangu ingekuwa Isha kufa. Wadogo zangu ambao wanamsikiliza kila kitu ndoa zao zipo very unstable. Mimi sikutaka kumsikiliza kila kitu. Haya maisha nilichojifunza tujifunze sana kujitegemea jenga misingi mizuri ya familia yako. Wapende watoto wako, wape rewards jenga uchumi wako. Anayekupenda mpende asiye kupenda achana naye.

Mama anataka akupangie uishi na nani na usiishi na nani sasa haya maisha hayaendi hivyo.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Duuu mzeee mbona huyu unamzungumzia bi mkubwa wangu kabisa.
 
It's Official. We won't be on the same page, never ever.
 

Aiseeee [emoji119][emoji119][emoji119]
 
Tuko pamoja mimi nina 3miaka hadi ifike 5 ndio niende nifike jioni niondoke asubuhi

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Bahati mbaya siwezi share nini shida. Ila ndio hivyo itakavyobakia. Mawasiliano yatabakia kumpa shikamoo tu
Dah...! I feel what you are through. What if ukisikia kafariki? Utaumia mno au utaona normal tu? Unaonekana humpendi sana baba/mama yako. Dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…