Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwaio unatushaurije tulio kinyume na imani za kishirikina....tukubali kushindwa au?
 
Zamani ulikuwa genius sasa umekengeuka na kwenda kutafuta hekima kwa hao vinyago hapo. Naomba Yesu Kristo akurudishe kwenye hekima na maarifa yake kwani hakuna linaloshindikana kwa Yesu Kristo. Safari yako ya kurudi kwa Yesu inaanza sasa.
 
Siku nikienda nitaleta mrejesho ila kitakachonipeleka moja ni kufanya utafiti kwamba je,hivi ni kweli hizo tunguli zina effect kwenye maisha..?
Na la pili nadhani itakuwa mapenzi😅
Kama sio hilo basi nawania kiti Cha ikulu full stop😅
 
Waganga anakupa solution fasta...ila maombi sometimes watu wanavunja au wanapiga vitu wasivyojua vimetegewa wapi..wachawi Wana formula...Sasa we unaoomba kitu ambacho hujui kilitegwa vipi..ilo Ni tatizo...pia walokole wengi Hawajui jinsi ya kuita malaika wa kuwasaidia..hawajui majina ya MUNGU yenye nguvu ambayo ukitaja lazima kitu kiwe..ila wachawi wanajua kukusanya roho..pepo na jinni na kuyatuma watakavyo.......Sasa bora niende zangu kwa mganga aniambie fasta na kusolve tatizo bila kupoteza muda
 
Mimi sina imani na waganga Ila ilitokea kasumba flani ilinibidi niende sio MTU wa dini deep yaani nafika taja shida zangu akachukua na maelezo alikuwa ni shekhe flani anatumia ubani na tuvitu twa harufu marashi pia akaanza kuniganga Mimi nam enjoy naona anachora matairi ya gari kwenye liungo lake duh since naingia nilikuwa sina imani kabisa kufupisha alinigonga hela akataka nirudi sijui awasiliane na jini gani nirudi after two day na pesa iliyonona kidogo majibu yake ya awali kwenye tatizo langu hayakuwa na muelekeo sikurudi na paka Leo wengi makanjanja.
Tubaki njia kuu Mungu yupo tummwamini na kumuomba
 
warumi umeshawai kupewa masharti magumu na mganga hadi yakakuogopesha endapo utayashindwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…