Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Urudi na ushuhuda kabisa.Huu Uzi umenikumbusha mbali Sana..nitarudi.
Sawa kaka akeUrudi na ushuhuda kabisa.
Zamani ulikuwa genius sasa umekengeuka na kwenda kutafuta hekima kwa hao vinyago hapo. Naomba Yesu Kristo akurudishe kwenye hekima na maarifa yake kwani hakuna linaloshindikana kwa Yesu Kristo. Safari yako ya kurudi kwa Yesu inaanza sasa.Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.
Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.
Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.
Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .
Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.
Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.
Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.
Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.
Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.
Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hahahahahah weee mtu umenifurahisha huyu cha moto atakiona waganga siku hizi wana smart😛😛😛😛mkuu umempiga picha mganga ukamsambaza?
Keisha habari yako.
Ukitaka kurud niambie nitume nauliHuu Uzi umenikumbusha mbali Sana..nitarudi.
Toen nuks hapa[emoji16][emoji16]Waganga tuna tunaruhusiwa ku komenti?
SawaUkitaka kurud niambie nitume nauli
stidy