Kunakiipind nilitaka kwenda kwa waganga kumrudisha mpenzi wangu akiyekuwa akisumbuliwa na mapepo. Ni kuwa alianza nichukia bila sababu lakini ilikuwa ni influence ya mapepo. Mwishoni alikuwa akija kwangu lazima mapepo yampande so akaacha hata kuja kwangu na kuanza nichukia.
Nilimconvice nimpeleke kanisani aombewe kumbe ndyo ikawa nachocheea moto. Nikazidi chukiwa mpaka akasema tuachane kabisa. Allipokuwa akiniona tu anaugua ghafla.
Kwa upendo niliokuwanao niliumia sana. Nilifanya njia nyingi ili nimsaidie ikashindikana.
Rafki yangu akanishaur niende kwa mganga ili nitumie dawa za mvuto nimrudishe then anisikilize kila nachotaka ili iwe rahisi kumpeleka kwenye maombi aombewe.
Sikuwahi kwenda kwa mganga na sufikirii kufanya ivyo maisha yangu yote. Nilishauriana na Rafiki yangu yeye aende anilitee iyo dawa kwa gharama zangu.
So aliniletea dawa unaweka kwenye kibatari kinawaka siku 3 unakuwa unaongeza tu dawa kwenye mafuta huku unanuwia. Nilifanya ivyo kwa siku 2 ya tatu ikanshinda. Chumba changu kilijaa mosh mweusi nkakata tamaa.
(Hii ni story ndefu nakatisha tu baadhi ya matukio. )
Nilikata tamaa na nikarudi kwa Mungu kufanya Maombi. Nilifunga na kumuombea mungu amtibu mapepo yake. Ila alizidi kunichukia mpaka tukaacha kuongeleshana kabisa.
Nikaamua kwenda kuombewa mimi mwenyewe maana mambo yangu yalikuwa yamekwama toka nianze kudate naye. Biashara zangu zilikuwa napata hasara tu. Na mpaka nilikoswakoswa kufa kwenye ajari kubwa. 2017.
Nilipofika kwa bwana wa maombi akaniombea na kuniambia kuwa niliingilia ndoa ya watu. Yani yule dada alikuwa kama kaolewa na Jini. Na kama anajini mahaba. ( actually yule mtoto alikuwa anapenda ngono sanaa sijawai ona) So alichonishauri ni kuachana naye kabisa la sivyo nitapotezwa kwenye ramani ya dunia. Nilimsisitiza anisaidie amtolee mapepo niweze ludiana naye ila alinijibu kwa kusema. " kama imepangwa kuwa ndye atakuwa mke wako utakuwa naye ila kama sivyo hata usijisumbue."
Kweli nikafata ushauri na kuanza maisha mapya. Nikapta GF mwingine mpaka tukafunga ndoa. Biashara yangu na maendeleo yangu yaliludi katika mstari kwa kasi ya ajabu.
Sent using
Jamii Forums mobile app