Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Hahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
🤣🙌🙌🙌
 
Haiwezekani na haitakaa itokee

Jr[emoji769]
Mkuu hiyo inatokea sana huku Usukumani, unakuta Ng'wana Luhanya ameenda kuloga usiku kumbe jamaa limezindika ile nyumba, anajifalaguafalagua mpaka kunakucha yuko hapo hapo na masempele yake. Mpaka mwenye nyumba anaamka! Sasa hapo nikiamua kumfanyia mauaji?
 
Waganga wenyewe wanaogopa corona, eti uvae barakoa na uoshe mikono kilingeni..!!
 
Hahaaaaaa.....
Naji mngemrudishiaaa.
 
Mkuu tupe connection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si unaona, yaani safari moja huanzisha nyingine, huyo angekuja kupukutisha ukoo mzima halafu baadae wangemchukua na yeye akatumikie wengne

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliwahi kuelezwa na jamaa mmoja kuwa walikuwa wanachimba TANZANITE kule Mererani., mmoja wao alikwenda kwa mganga ilipate madini. Huyu jamaa alipewa masharti ya kuoga pale anapochimba madini mchana kweupe!Wale wengine walishangaa kuona jamaa anashuka ndani ya gari huku akiwa na ndoo ya maji , akaanza kuoga!
 
Allah anistiri saana nisifike huku kwa kweli! Mara zoote namuomba allah anikinge na roho ya kishirikina kwa kweli, kuingia rahisi ila kutoka huko mtihani.

Kuna mitihani mtu inakufika, unakosa pa kushika, kwangu mungu ndio kimbilio pekee, najua katika huo mtihani pia kuna mtihani wa subira upo juu yake, lazima niwe na subira, nikijiuliza kwa mema gani hasa ninayofanya kiasi anijibu haraka haraka hivyo huwa sioni, hivyo nakuwa mpole nikijibidiisha kumuomba anivue hayo majanga.
Najua kila jambo ni mtihani lazima nifaulu ama nifeli(yaani nishukuru ama nikufuru) so huwa natembea humu.

Sisemi mie mwema saana ama sikosei, kuna yangu mabovu nayabananga(namuomba allah anistiri nadhani nikipata mke nitakuwa nimeanikiwa kwa kiasi kikubwa kuepukana na majanga yangu), ila hili la shiriki najitahidi zaidi nisiyabanange. Nimeona watu wangu kadhaa waliolowea katika mambo haya, ushirikina miyeyusho.
 
We jamaaa duuh usije ukawa umemfunga kizazi dada wa watu

l love you mamy .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…