Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
Sasa wazazi wepi tena si ndo ao ao au?
 
Maisha haya kila mtu ana Siri zake nilishawahi kwenda mdogo wangu alikuwa Mgonjwa hospitality wenyewe walishauri tuanfalie njia nyingine. Ndiyo tulienda huko
 
Niliwakuta wanafanya mazingaombwe mara wakatupaka dawa ili tuone miujiza yao. Hapo niko kidato cha tatu.
Hawakufanya tuone kitu badala yake wakasema kila aliyepakwa dawa awafuate au wakivimba mikono baadae wasijelaumu.
Mie huyoo nikaunga tela kuwafuata huko uchochoroni ngarenaro hadi walipokuwa wana 'ofisi' yao.

Kuna dada akaingia nikasikia analalamika yeye ni housegirl na bosi anamnyanyasa hivyo anaomba bosi atengenezwe.

Kuna mzee akaingia nikasikia analalamika amezulumiwa shamba hivyo waliomzulumu watengenezwe.

Wakaendelea watu wengi mie bado naogopa.

Ikafika ndo nimebaki wa mwisho nikaingia. Nikakuta jamaa amekaa kitandani kumejaa maburungutu ya hela na matungyli na hirizi kadhaa. Akaniuliza nataka nini nikamwambia sina shida yeyote ila kwa kuwa wamesema aliyepakwa dawa aende na mie ndo nimefika.

Akanihoji endapo ningetaka fedha kwa ajili ya shule. Nikamwambia sihitaji maana sitakuwa na jibu la kuwapa wazazi kuhusu nilipotoa. Akaniambia niweke sikio kwenye moja ya tunguli nisikilize mizimu inasemaje. Nikatega sikio huku kichwa kimemuelekea yeye hivyo siwezi kumuona. Mara nikasikia sauti zisizoeleweka nikataka kutoa sikio akanishikilia kichwa. Nikawa nahojiwa na mizimu kama inisaidie kufaulu n.k kisha nikasikia kama inasema niweke hela niliyo nayo pale. Nikageuka kwa kasi nikakuta jamaa ana microphone mdomoni ikabidi niipotezre kama sijaona kitu maana kwa watu pale. Ikabidi niseme sina hela isipokuwa mia mbili tuu. Basi nikaiweka hiyo miambili na kusepa.

Hadi leo siamini katika uganga.
GOOD!
 
Nimewahi Kwenda kwa Mchanga kwa matatizo mawili matatu ya kimaisha ila kila nikienda kwa mganga usiku lazima nimuone anakuja kuniloga namtoa nduki mwisho nikaamua kuacha Kwenda maana nilijiona mie ndio mganga hata mganga mwenyewe haniwezi
 
Kila mtu huwa ana imani yake

Kila mtu ana mbinu zake za kutatua matatizo yake.

Wapo ambao wakipata shida kidogo tu ni kwa babu sangoma wanakimbilia.

Tujuzane, vipi gharama huko? Shida zinatatulika? Permanently or temporarily?

Na pia nasikia every dark magic comes with a price, ni kweli..? Ni price zipi mnalipa kupata magic nyeusi hizo

Tujuzane

Binafsi mimi sijawahi kukanyaga kwa sangoma na sitakaa nikanyage huko
Rekebisha maelezo yako sasa kama hujawahi kwanini useme tulio wahi! Sema mliowahi kwenda kwa waganga njooni hapa. Inavyoonesha wewe ni mmoja wao wa kwa hizo imani ila umeamua ujitoe bila kujijua ukakosea kuandika.
 
Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
Sasa si bora huyo Sangoma niliwahi kwenda kwa mchungaji fulani tegeta ni mama hivi katika mazungumzo yetu aliniambia eti matatizo yangu yanatokana na jina langu Hahahaha nilicheka sana kimoyomoyo mchungaji anatoa ushauri wa kigangaganga Hahahaha akaniombea pale wapjii
 
Back
Top Bottom