Habari wana jamvi,wajuzi wa mambo.
Nije katika makusudio ya uzi huu.UCHAWI,UPO,NA WAGANGA WA KWELI WAPO UTAKI ENDELEA KUBISHA,UONE KAMA UTAPATA FAIDA YOYOTE.
Kiukweli maisha yanaweza kukutuma kufanya chochote ili kupata unafuu wa mambo yanayo kuzonga.ima maisha,maradhi,mapenzi nk.binafsi ninekwenda kwa sagoma kwa sababu kuu moja.
Kuna jirani yangu nimepakana nae mpaka wa shamba, kiukweli huyu jirani ni mrafi wa ardhi sijapata kuona.anavyo igombania kana kwamba akifa anaichukua hiyo ardhi, baada ya kugombana kwa mda mrefu niliamua kumuachia, ili amani idumu. ila kwa masharti aniambie, anataka ukubwa upi na sitotaka tena majadiliano nayeye kuhusu mipaka tena.alijubali na nikaenda nae kwa mjumbe wa shina, tukakubariana vizuri.
Baada kukaa kwa mda kidogo nikaenda kwa babu mmoja bungu kwa ndani uko.nilipo fika nikamueleza mzee kua nimedhurumiwa eneo langu na jirani yangu.nikaulizwa utanaje?nikasema mi nataka eneo langu lirudi kwa amani,na basina majadiliano. Basi kazi ikafanywa, nikombwa nikannue baazi ya vitu,nikatekeleza. Aisee sikuamini kilicho tokea baada ya zile siku7 nilizo pewa na babu. Alikuja mwenyewe nyumbani akiwa na mjumbe yuleyule, na makaratasi tulio kubaliana, na kuongea mbele ya mjumbe kua kuazie leo eneo nalirudisha mikononi mwako, na kuniomba msamaha wa kufa mtu tena uku akitokwa na machozi, kana kwamba anaumia kiasi kikuvwa mno.
Nikamuuliza kwa nini umeamua kurudi tena? Akasema kaka,roho yangu inauma kwa kutenda uhovu huu,nimejifikiria na kutafakari nimeona sina sababu ya kufanya hivyo.ok!mjumbe unamsikia jirani yangu? Je, ushauri wako? Akasema kubari lirudi mikononi mwako kwa ahadi isiyo jirudi tena swala hili.ok sawa tukaa chini na kuyamaliza.
TOKEA APO NIMEAMINI DAWA ZIPO NA ZINAFANYA KAZI.
JE, WEWE UMEKUTANA NA KISANGA GANI KATIKA MAISHA NA SAGOMA?