Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?

Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?

Redpanther

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
2,823
Reaction score
3,816
Habari za wakati huu ndugu zangu na wanajamvi la Hoja mchanganyiko? Nitaomba radhi kwa yule nitamkwaza ila acha niliweke hili swala hapa jukwaani tulijadili.

Mimi nimebahatika kulelewa na wazazi wote wawili mpaka nimekuwa mtu mzima. Kufika kwangu hapa ni Juhudi za bila kuchoka za Mama na Baba kwa Msaada ya Muumbaji. Kama kijana niliyelelewa maisha hayo, naweza nisijue namna gani ilivyo kulelewa na mzazi mmoja, zile hustle zilipaswa zifanywe na wqzazi wote wawili zinafanywa na mzazi mmoja, are you thinking what am thinking [emoji848]

Daaah kwanza salute sana Kwenu single mothers, Mnapambana na muendelee kupambana ila tu msituchukie wanaume.

Mzazi mmoja anapiga kazi ya watu wawili, daah, Hat off to all of respective and hard working single mothers out there. Najatibu kuwaza mambo ambayo baadhi ya wadada ambayo nimetokea kuwa na urafiki nao,kiukweli vita wanavipiga.

Unajua kuna muda anaenda kudanga ili tu apate pesa ya kuwalisha, kuwasomesha watoto. Mtoto wa single mother anakuwa kwa uwezo wa Mungu kupitia akili janja ya mwanamke.

Wakati nakua nimekua nikiona vile mama zangu wadogo wanavyopambana kulea familia zao. Na wengine waliobahitka kupata mabwana walipata support kubwa kutoka kwa hawa wanaume na watoto waliwalea mpka leo wamekua. Lakini kundi hili la single mothers wanaolea watoto wao kwa kutumia mfuko au Pochi ya Madanga ni wengi sana, almost 90%. Na haka kakundi ndio nataka tukajadili hapa leo hii.

Kuna vijana wa kiume ambao leo hii, Boastfully, wanasema mimi sitakuja kuoa mwanamke aliye mtoto tayari. Mimi hii naiona sio sahihi, hawa ndio walipaswa wawe wakwanza kuwaoa hawa single mother as the payback. Kama vile nyinyi mlivyolelewa yawapasa mlipe shukrani kwa mwenyezi kwa kuwafuta machozi hawa wanawake walio na watoto na hawana Wanaume.

Kama vile nyinyi mlilelewa kwa shida mnajua vile mama anahangaika sana kuendesha familia anapokuwa pekee yake, mnapaswa mrudishe shukrani kwa mwenyezi kwa kwenda kuwalea hao watoto ambao Baba zao wapo au hawapo duniani.

Niwaombe sana sana vijana wenzangua wa kume mliolelewa na Mama mmoja, nendeni mkaoe single mother muwafute machozi kama vile mama zenu walivyofutwa machozi na Baba zenu wa kufikia.

Sio uongo na nyinyi mnajua, wale Baba wa kufikia walikuwaga wanawapeni vipesa vya kujikimu shule na mengineyo na hatima yake mama aliweza kuwakuza hadi mmefikia hapo.

Na nyie dada zetu mliopata watoto na hamuishi na hao Baba za watoto msijisifu sana kwa watoto eti kuwa umewalea hao watoto bila msaada wa mtu yoyote, kwelii? Hivi wale wanaowalipia ada za watoto wenu ni akina nani na wanaolipa kodi ya pango la nyumba ni akina nani?

Ifike mahala unawabia watoto wako wakiume ukweli, ili siku wakikua waweze kuwasupport akina dada au akina mama wemye watoto kama nyinyi mlivyo kuwa.

Ni hayo tu, Nakaribisha maoni na michango juu ya mafikirio yangu haya usiku huu wa manane. Naamini meseji imefika. Mnisamehe nitakaowakwaza.


MY FAVORITE COMMENT

Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?
Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?
 
IMG_0397.jpg
 
Pamoja na maelezo yako yote
Pamoja na kwamba mama yangu pia amenilea akiwa single mom
Lakini Mimi sitakuja kufanya Hilo kosa la kuoa single mom labda km na Mimi tayari Nina watoto wawili

Ila bado Sina mtoto usinizungue mabint kibaooooo wabichi wakunizalia first born
 
Nikiwa kama international step dad nasema ingia kwenye uhusiano na single parent kwakua unampenda na siyo kwakua unamuonea huruma na unafanya payback.
Kuna mzee mmoja nimewahi kukutana nae aliniambia maneno haya

"Usioe mwanamke kwa kumuonea huruma mfano umekaa nae kwa kipindi kirefu ila kama kuna vitu umeona havifai na umejitahidi aviache, na vimeshindikana basi hata iwe vipi usioe kwa huruma"
 
Its male nature. What goes against nature, goes against God, for nature is God.

In nature , dume la Simba huua vitoto vya dume mwenzake (dhaifu) ndio humpa mimba nyingine jike (yenye mbegu imara), hata siku moja halei zile mbegu dhaifu toka kwa dume dhaifu lililofukuzwa. Hii imehakikisha only the best breed inaendelezwa. Its a method of nature.
 
Back
Top Bottom