Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?

Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?

Nikiwa kama international step dad nasema ingia kwenye uhusiano na single parent kwakua unampenda na siyo kwakua unamuonea huruma na unafanya payback.

Ni sawa Mkuu, kwahiyo unataka kunambia kwa idadi ya single mothers waliopo atakosa kweli wa kumpenda ? Watakuwepo Mkuu ila sema mtizamo hasi juu ya wenzetu hawa. Tuwapende na tuwaoe kama ikitokea umepata mmoja akaonyesha utayari
 
Habari za wakati huu ndugu zangu na wanajamvi la Hoja mchanganyiko? Nitaomba radhi kwa yule nitamkwaza ila acha niliweke hili swala hapa jukwaani tulijadili.
Mimi nimebahatika kulelewa na wazazi wote wawili mpaka nimekuwa mtu mzima. Kufika kwangu hapa ni Juhudi za bila kuchoka za Mama na Baba kwa Msaada ya Muumbaji. Kama kijana niliyelelewa maisha hayo, naweza nisijue namna gani ilivyo kulelewa na mzazi mmoja, zile hustle zilipaswa zifanywe na wqzazi wote wawili zinafanywa na mzazi mmoja, are you thinking what am thinking [emoji848] … Daaah kwanza salute sana Kwenu single mothers, Mnapambana na muendelee kupambana ila tu msituchukie wanaume.
Mzazi mmoja anapiga kazi ya watu wawili, daah, Hat off to all of respective and hard working single mothers out there. Najatibu kuwaza mambo ambayo baadhi ya wadada ambayo nimetokea kuwa na urafiki nao,kiukweli vita wanavipiga. Unajua kuna muda anaenda kudanga ili tu apate pesa ya kuwalisha, kuwasomesha watoto. Mtoto wa single mother anakuwa kwa uwezo wa Mungu kupitia akili janja ya mwanamke.
Wakati nakua nimekua nikiona vile mama zangu wadogo wanavyopambana kulea familia zao. Na wengine waliobahitka kupata mabwana walipata support kubwa kutoka kwa hawa wanaume na watoto waliwalea mpka leo wamekua. Lakini kundi hili la single mothers wanaolea watoto wao kwa kutumia mfuko au Pochi ya Madanga ni wengi sana, almost 90%. Na haka kakundi ndio nataka tukajadili hapa leo hii.
Kuna vijana wa kiume ambao leo hii, Boastfully, wanasema mimi sitakuja kuoa mwanamke aliye mtoto tayari. Mimi hii naiona sio sahihi, hawa ndio walipaswa wawe wakwanza kuwaoa hawa single mother as the payback. Kama vile nyinyi mlivyolelewa yawapasa mlipe shukrani kwa mwenyezi kwa kuwafuta machozi hawa wanawake walio na watoto na hawana Wanaume. Kama vile nyinyi mlilelewa kwa shida mnajua vile mama anahangaika sana kuendesha familia anapokuwa pekee yake, mnapaswa mrudishe shukrani kwa mwenyezi kwa kwenda kuwalea hao watoto ambao Baba zao wapo au hawapo duniani.
Niwaombe sana sana vijana wenzangua wa kume mliolelewa na Mama mmoja, nendeni mkaoe single mother muwafute machozi kama vile mama zenu walivyofutwa machozi na Baba zenu wa kufikia. Sio uongo na nyinyi mnajua, wale Baba wa kufikia walikuwaga wanawapeni vipesa vya kujikimu shule na mengineyo na hatima yake mama aliweza kuwakuza hadi mmefikia hapo.
Na nyie dada zetu mliopata watoto na hamuishi na hao Baba za watoto msijisifu sana kwa watoto eti kuwa umewalea hao watoto bila msaada wa mtu yoyote , kwelii ?? Hivi wale wanaowalipia ada za watoto wenu ni akina nani na wanaolipa kodi ya pango la nyumba ni akina nani ??
Ifike mahala unawabia watoto wako wakiume ukweli, ili siku wakikua waweze kuwasupport akina dada au akina mama wemye watoto kama nyinyi mlivyo kuwa.
Ni hayo tu, Nakaribisha maoni na michango juu ya mafikirio yangu haya usiku huu wa manane. Naamini meseji imefika. Mnisamehe nitakaowakwaza.
Wee jamaa bwana yaani kisa mama zetu walifanya umalaya na kuzalishwa na kuachwa ndio na sie tukafanye ujinga wakuoa single maza?

Kosa ni kosa tuu ata kama kafanya mama yako au baba yako. Mambo ya kusema watoto wanalelewa na nguvu za mungu huo ni ujinga tuu maana kwanza huyo mungu mwenye ulisha mkosea kwa kuzaa nje ya ndoa.

Last but not least usingo maza mwingi ni kiherehere chao na umalaya wao. Wacha wabebe majuto ya dhambi zao.
 
Pamoja na maelezo yako yote
Pamoja na kwamba mama yangu pia amenilea akiwa single mom
Lakini Mimi sitakuja kufanya Hilo kosa la kuoa single mom labda km na Mimi tayari Nina watoto wawili


Ila bado Sina mtoto usinizungue mabint kibaooooo wabichi wakunizalia first born

Kwani huyu aliye na mtoto mmoja hawezi kukupatia first born ? Pamoja na kwamba kwake anaweza asiwe first born lakini utamuvwa kumwita first born wako bado upo .
 
Wanawake hawana shukrani ata umfanyie lipi utakuja kuishia kudharaulika tu

Single mother hatuoi hawa ni laana sababu huwa wanalinga sana kipindi wapo mabinti dharau nyingi anaweza akamkataa jamaa mwenye nia ya kuoa kisa anadate na Mme wa mtu

Single mothers sio laana Mkuu, hawa watu ni wasikivu sana na wametulia asikuambie mtu. Tuliza akili utapata mtoto mzuri kabisa, kuna watu mimba zimeingia kibahati mbaya kama vile tu mnavyowapelekea mioto hawa ambao hawajao na wao ilitokea hiyo ishu sidhani kama walitaka.
Lakini kingine ndugu yangu, Single mothers unakuwa unahakika wa kuwa na mtoto maana tayari amesha ichallenge uterine yake. Single mother are very beautiful and nice women than the way we know em, let’s do something special for our girl.
 
Wanawake hawana shukrani ata umfanyie lipi utakuja kuishia kudharaulika tu

Single mother hatuoi hawa ni laana sababu huwa wanalinga sana kipindi wapo mabinti dharau nyingi anaweza akamkataa jamaa mwenye nia ya kuoa kisa anadate na Mme wa mtu

Sio wote walikuwa wanadate na married men Mkuu, angalia kwa jicho jingine utaona uzuri wa hawa viumbe . Kuna wengine humu wameshazalisha mtoto wa mtu still mtu anakua na guts za kusema maneno hayo, sio poa wakuu.
 
Wangekuwa ni single maza wale wa enzi zile za mama zetu sawa ila hawa wa twenti senchuali my dear brother utapata heart attack ambayo hujawai ipata tangu uzaliwe

[emoji28][emoji28][emoji28]Kwanini Mkuu ??
 
Kama umepata mwanamke anamtoto muache bro. Acha kujifariji ujinga. Mechi ianze bilabila

Sijapenda Mkuu, ila nimeliona hili suala vile ambavyo sisi wa kiume tumekuwa tukiwawanyooshea kidole sana hawa dada zetu. Alfu kingine, Mechi ya kuanza bila bila hainogi sana eti mpaka useme ni Muhimu sana. Kwanza ukiangalia single mothers wenyewe ndio sisi wenyewe humu humu tumewapiga mimba na wamejifungua ila hatuwataki tena, that isn’t fair at all.
 
Ni sawa Mkuu, kwahiyo unataka kunambia kwa idadi ya single mothers waliopo atakosa kweli wa kumpenda ? Watakuwepo Mkuu ila sema mtizamo hasi juu ya wenzetu hawa. Tuwapende na tuwaoe kama ikitokea umepata mmoja akaonyesha utayari
Sina tatizo na kuoana na single parent isipokua msingi wa ndoa usiwe kuoneana huruma
 
Kama umepata mwanamke anamtoto muache bro. Acha kujifariji ujinga. Mechi ianze bilabila
Na ww usijifariji na kuanza bila bila halafu mechi inaisha na magoli matano wakati umefunga moja, nne zote si zako. Malaya ni malaya tu hata mpira ukianzia kwako.
 
Back
Top Bottom