Kwa Wale Vijana Wanaopenda Kuvaa Kiatu kisichoweza Kuingia Maji Timberland Boot

Kwa Wale Vijana Wanaopenda Kuvaa Kiatu kisichoweza Kuingia Maji Timberland Boot

Mkuu Kobello Umesema maneno ya Ukweli huyu FaizaFoxy anajiropokea tu anaijuwa kweli kiatu cha Timberland thamani yake?

Nnavijuwa viatu kabla hujajuwa viatu ni nini, bado ulikuwa unapekuwa na kamasi zinakuchuruzika.

Hivyo ni viatu vya kazi usione hao mastaa wanapigwa picha wamevivaa ukaona ndio viatu vyao wanavyonunuwa, hao wapo katika kuvitangaza wanalipwa. Na mtu mshamba tu na asiyejuwa kuvaa ndio atavivaa hivyo kwa minajili yote.

Wajinga ndio waliwao.
 
Hehehe .... Sijawahi kupekua, na Timberland boots ni symbolic kwa urbanites/hiphop/east coasters. Ni fashion statement tu kama zilivyo back-packs au baseball hats. Unajichora tu, labda wadanganye wa kuja huko kariakoo. Mimi mjini ni 3rd generation, yaani babu yangu kazaliwa mtaa wa Muheza kariakoo.
Timberlands hazivaliwi na washamba. Wewe stick to "makubazi" haya mambo waachie vijana, usijichore.
 
Laki 3😕😕😕 ada hyo ya shule

Tangaza biashara yako maboyastiki yatanunua😎😎
 
Nilishawahi kuwa nazo nikazunguka navyo Tanzania, vikawa hoi. Pia kwa sisi Warefu, vinaumiza sana Mgongo.

By the way, huyu jamaa anaitwaje?
Huyu ni mmojawapo wa Mastar Holwood simjuwi kwa jina Sikonge Mkuu Viatu hivyo hapo kwetu watu hawawezi kuvinunuwa vinavaliwa na Ma-Star wa Hollwood mötu masikini hawezi eti atowe Shillingi laki 3 na elfu 50 anunuwe Kiatu cha Timberland wakati kwake anakula ugali kama huyu bibie FaizaFoxy hana pesa ya kununuwa kiatu kam hicho wakati anashindia kula ugali na kauzu.:A S wink:
 
Last edited by a moderator:
Timz na CAT sio label ya yeyote jamani tukubali tu kuna classes na choice pia! !!
Hivyo ni viatu vya mkataba haswa kwa watu wa kazi!!
kobelo kasema pia hiyo ni symbol kwa watu fulani yaani hata ukisafiri ukamkuta mtu kavaa hiyo basi tayari hamkosi la kuzungumza sababu kama nilivyosema hivyo sio viatu vya kila mtu tu!!

Lakini mi nilipenda zaid HAWKEYE sababu ya uzito, wao wanatumia non rubber sole inakuwa kama sponge ngumu sana hii kwa urban-hip hop-hustlers-hangouts inakuwa more comfy kutembea nayo!!!
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni mmojawapo wa Mastar Holwood simjuwi kwa jina Sikonge Mkuu Viatu hivyo hapo kwetu watu hawawezi kuvinunuwa vinavaliwa na Ma-Star wa Hollwood mötu masikini hawezi eti atowe Shillingi laki 3 na elfu 50 anunuwe Kiatu cha Timberland wakati kwake anakula ugali kama huyu bibie FaizaFoxy hana pesa ya kununuwa kiatu kam hicho wakati anashindia kula ugali na kauzu.:A S wink:

Ugali na kauzu my favorite, naona una ilmu finyu sana, kuna chakula gani ambacho ni tofauti kati ya masikini na tajiri? fikiri.

Unaenda restaurant unauziwa wali uliopikwa na mchele ule ule anaokula masikini kwa bei mbaya. Lakini kwa ujinga wako unaona umekula cha maana zaidi.

Hapa unafata jina na nani kapigwa picha (kalipwa) kutangaza hivyo viatu, lakini laiti ungalijuwa mastaa wanavyovaa usingekuja na upuuzi wako hapa wa kusifia viatu vya kufanyia kazi za sulubu wewe ukaona ndio vya maana. Ni ujuha wa hali ya juu, na nna uhakika kuna majuha wenzako humu wanaokuunga mkono.

Isitoshe, kwa umwanjo-mwanjo wako umeona kiatu cha dollar 200 ndiyo ghali sana, amma kweli wewe ni mwanjo-mwanjo. Unajuwa viatu wewe? ngoja tukupe darsa la viatu:

Nna uhakika hujawahi kuyasikia wala kuyaona haya majina, hivi ndivyo viatu ghali, si hivyo viatu vya blue collar:

Miu Miu, Stuart Weitzman, Brian Atwood, Walter Steiger, Christian Loboutin, Jimmy Choo, Manolo Blahnik, Louis Vuitton.

Hayo ndio majina ya viatu unayoweza kusema ghali, Louis Vuitton vya bei ya chini ni around $10,000/= Ukija kwa Jimmy Choo unaongelea kwa uchache uwe na $ 3,500/=

Unajuwa viatu wewe? uvijulie wapi mwanjo mwanjo wa Bagamoyo wewe, nakwambia wewe ni kama kipofu uliyeona punda huko Uturuki, hujijui hujitambui. Weka kiatu cha Manolo Blahnik, ambacho kwa kukujuza tu, nimeshakifuma kwa muuza mtumba Tanzzania kwa TZS 15,000/= na hicho ukiingia dukani nnakuhakikishia ni mshahara wako huko Uturuki wa miaka mitatu au mitano , kwanza duka linavyouzwa hivyo huingii.

Ushasikia viatu vya Jason Arashaben wewe? pair moja ya hicho kiatu ni bajet ya kwenu Bagamoyo ya miaka miwili.

Mwanjomwanjo wahed.
 
Hahahahaaa, nilitaka kujua kama wewe ni Mpenzi wa film ya The Lord Of The Rings.......

Anaitwa Orlando Bloom au jina alilotumia kwenye film hiyo juu anaitwa Legolas......

images

Achana na huyo Kungwi FF. Alisoma na Warioba na hajafanikiwa maishani kuweka historia Tanzania.

Huyu ni mmojawapo wa Mastar Holwood simjuwi kwa jina Sikonge Mkuu Viatu hivyo hapo kwetu watu hawawezi kuvinunuwa vinavaliwa na Ma-Star wa Hollwood mötu masikini hawezi eti atowe Shillingi laki 3 na elfu 50 anunuwe Kiatu cha Timberland wakati kwake anakula ugali kama huyu bibie FaizaFoxy hana pesa ya kununuwa kiatu kam hicho wakati anashindia kula ugali na kauzu.:A S wink:
 
MAVIATU makubwa makubwa mpaka leo kuna watu wanavaa,uzito wote huu,nikikutana na mtu amevaa namuonaga mshamba

Halafu cha kushangaza MTU anavaa hajui ni kiatu cha kupandia mlima, au wakati wa winter, hivi Dar na joto hilo mmmh strange but true...
 
Hahahahaaa, nilitaka kujua kama wewe ni Mpenzi wa film ya The Lord Of The Rings.......

Anaitwa Orlando Bloom au jina alilotumia kwenye film hiyo juu anaitwa Legolas......

images

Achana na huyo Kungwi FF. Alisoma na Warioba na hajafanikiwa maishani kuweka historia Tanzania.

Hawezi kusoma na mtu mweledi kama Warioba...
 
Kwa Wale waaotaka Kiatu kisicho ingia Maji hicho hapo Timberland Boot Dollar 200. Ukikitaka nione mimi.

Timberland Helcor ndiyo kiatu cha maana kama unataka waterproof, fireproof, scratchproof na boot imara.
 
Last edited by a moderator:
Haha hivi Viatu kwa Hali ya Hewaya Kibongo bongo ..............
 
Attachments

  • tim-29597-1.jpg
    tim-29597-1.jpg
    53.8 KB · Views: 131
  • mberland-Stivali-Estivi-Sandybrown-JX_itely-261_LRG_03.jpg
    mberland-Stivali-Estivi-Sandybrown-JX_itely-261_LRG_03.jpg
    51.7 KB · Views: 126
  • LTD-collection.jpg
    LTD-collection.jpg
    52.3 KB · Views: 123
  • discount-timberland-mens-boots-81378.jpg
    discount-timberland-mens-boots-81378.jpg
    27.1 KB · Views: 159
  • colette-timberland-summer-2010-front.jpg
    colette-timberland-summer-2010-front.jpg
    21.9 KB · Views: 141
  • TIMBERLAND UOMO - 4.jpg
    TIMBERLAND UOMO - 4.jpg
    39.9 KB · Views: 189
  • summer.jpg
    summer.jpg
    23.2 KB · Views: 153
  • summer timber land.jpg
    summer timber land.jpg
    46.1 KB · Views: 142
  • timberland-6615rw-1.jpg
    timberland-6615rw-1.jpg
    30.9 KB · Views: 143
Back
Top Bottom