Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

Poleni sana ila hii ni wake up call tuache utegemezi, na huku US napo ni msiba tuu maana tariffs, artificial intelligence na siasa za Trump, hakuna ajuaye kesho, hata federal government employees ambao kazi zao kihistoria ndio the most secured, ndio wameanza nao na mpaka sasa maelfu wako nyumbani na 5000 FBI employees waliohusika na uchunguzi wa Jan 6 wanaweza kuingia jela, wananchi fight imeanza my hope damage haitakuwa kubwa
 
Kwani hawalipwi chochote baada ya kusitishiwa mikataba?Kama huna biashara ya maana mjini ni bora kurudi mkoani kujipanga kwanza!
 
Unamwachia nan? Mm nilichukua yote hata 0 haikubak yaan yote mwanzon nilijua watanipa kwa asilimia 33 ila nikawa smart nikabeba yote...pambana uchukue ufanye mambo yako

Kama ulitumia cheti cha form six unapewa hela yote,
Iko hivi kuna professional na non professional
Non professional ni zile kazi za form six kushuka chini,
Hao wanachukua hela yote,
Na professional ni zile kazi kuanzia diploma hao wanapewa asilimia.
 
Poleni sana ila hii ni wake up call tuache utegemezi, na huku US napo ni msiba tuu maana tariffs, artificial intelligence na siasa za Trump, hakuna ajuaye kesho, hata federal government employees ambao kazi zao kihistoria ndio the most secured, ndio wameanza nao na mpaka sasa maelfu wako nyumbani na 5000 FBI employees waliohusika na uchunguzi wa Jan 6 wanaweza kuingia jela, wananchi fight imeanza my hope damage haitakuwa kubwa

Siku zote kazi ya kuajiriwa ni ya mda tu, kuna siku mambo yatabadilika
 
Ndio manake angalau uende makao makuu ya wilaya. Toka kipato cha zaidi ya milioni 2 kwa mwezi mpaka laki 3?Huoni kama hujawekeza mjini itakuwa ni tatizo kubwa KuCoup?
Ni kweli, ila ni mtazamo, ukikaza hata hapa hapa mjini unatoboa
 
Kusitishwa kwa shirika la USAID na serikali ya Donald Trump kkutagusa maisha ya familia nyingi sana,
Sasa kama wewe ni mwathirika usipanick relax, wewe si wa kwanza kukutwa na hali kama hiyo,
Nimejaribu kukuwekea baadhi hatua za kuchukua ili upite salama

1. FIRST THING FIRST

Ulikuwa unachangia NSSF right?

Sawa hapa ndo pakuanzia, chukua documents zako mapema na uziwasilishe kwenye ofisi za NSSF ili uanze kulipwa haraka,
Ukikamilisha kujaza form yao ndani ya ya siku 30 utaanza kulipwa 33% ya mshahara wako kwa mwezi na utalipwa kwa muda wa miezi 6,
kwa hiyo kama ulikuwa unalipwa mil 1, utalipwa laki 330,000 kwa mwezi,
Unaweza kuiona ndogo ila ni pesa inayoweza kukuweka mjini.

Jitahidi kama una familia hii pesa itatue changamoto za muhimu tu.

Katika kufanya maamuzi ya matumizi nnashauri zingatia vitu vya lazima

a. Matumizi muhimu, mfano kununua nguo mpya ni muhimu ila si lazima
b. Matumizi Lazima mfano kula ni lazima

2. EVERY CENT COUNTS

Kumbuka kuwa mshahara uliokuwa unaingia kila mwezi haupo tena, hivyo ni lazima upitie upya matumizi yako, hasa matumizi makubwa na madogo ya kila siku.
Iko hivi,

a) kodi unalipa sh ngapi? Je inaweza kupungua, jibu ni ndio kama unalipa laki 3 tabata, kwa nn usihamie majohe, kinyerezi, mpiji au Kisemvule kwa nusu ya hiyo kodi,
Kumbuka ulikuwa unakaa karibu kwa sababu ya majukumu, usisubiri kesho anza sasa

b)Matumizi madogo madogo ya kila siku
Mara nyingi hizi huwa zinaonekana ni pesa ndogo zikitolewa kila siku, imagine kila siku unatoa shilingi elfu 10,000 kila siku kwa mwezi sio chini ya laki 3

Okay twende sawa, binafsi hiyo level nilishavuka,

Huwa nnafanya manunuzi ya jumla,
mchele nunua debe 35,000
Sembe nunua kiroba 8,000
Maharage sado 12,000
Dagaa 20,000
Nyama ya 30,000
Samaki 30,000
Mafuta 27,000
Gesi 55,000

Viungo unafanya shopping mara moja kwa wiki unatunza kwenye fridge, inategemeana na idadi ya familia uliyonayo ila kwa haraka haraka baadhi ya vitu hapo vinavuka mwezi na zaidi, mfano gesi matumizi mazuri ni kuanzia miezi miwili

Ni lazima uzingatie na situation yako, huwezi kuendelea kuishi kama awali wakati maisha yamebadilika.

Mpaka hatua hii unapaswa kuwa umejituliza kwenye ile 33%, yaani hakikisha matumizi yako ya mwezi hayazidi ile hela unayoipata,
Sikia watu wanakula mboga za majani kila siku na hawafi, watu wanashindia Maharage mchana na jioni na wanadunda tu,

Laki moja inaweza kutosha familia ya watu 4 vizuri kabisa, kupanga ni kuchagua, don't stress yourself chai asubuhi haina umuhimu wowote, kwanza ni luxury😋

Je unatafuta kazi au unajiajiri?
Ndio nnajua utatafuta kazi nyingine, umetolewa kwenye ajira na ulikuwa hujajipanga it's okay,
Cha kuzingatia wakati unatafuta ajira tafuta ujuzi utakaokuwezesha kuishi mtaani, yaani vi elfu 10,000 au zaidi visikupige chenga.

Please usije jichanganya kuingia kwenye betting, au forex, crypto currency it will be your funeral, usijidanganye hizo mbanga zinahitaji kichwa kisiwe na stress ya aina yoyote.

Tafuta shughuli itakayokufanya uwe busy,
Mfano unaweza kujifunza marketing, tafuta bizaa inayouzika, nenda kwa mfanyabiasha ongea nae ufanye kazi kwa commission, hakuna biashara kwa sasa isiyohitaji mtu wa marketing, haipo,

Ongea na mkurugenzi, mwambie sitaki unilipe mshahara utanipa asilimia % ngapi kwenye kila mauzo.

Mwisho nikutakie kila la kheri, Mungu kufanyie wepesi kwenye upite salama.
Hiyo ya kulipwa na NSSF kila mwezi inategemea na umri wako, kama una less than 55 unakua huna sifa but again inategemea kama michango haijafilisha miezi 180 hata kama una 55 and above bado huna sifa, is either utafute kazi ili uunge hiyo michango hadi ifikishe 180 or else utapewa mzigo kamili uende ukafe na shida/raha zako
 
Ni kweli, ila ni mtazamo, ukikaza hata hapa hapa mjini unatoboa
Itahitajika discipline ya kiwango cha PhD.Kwanza unaweza kuanza kupata pressure toka kwa marafiki,mwenza na hata watoto baada ya kipato kushuka.Hiyo inaweza kukutoa kwenye mstari wa malengo yako.Mkoani hakuna matumizi makubwa kuliko Dar.Mfano Unaweza kutumia gari mara chache kuliko Dar.Vyakula ni bei rahisi zaidi n.k
 
Back
Top Bottom