Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

Poleni sana ila hii ni wake up call tuache utegemezi, na huku US napo ni msiba tuu maana tariffs, artificial intelligence na siasa za Trump, hakuna ajuaye kesho, hata federal government employees ambao kazi zao kihistoria ndio the most secured, ndio wameanza nao na mpaka sasa maelfu wako nyumbani na 5000 FBI employees waliohusika na uchunguzi wa Jan 6 wanaweza kuingia jela, wananchi fight imeanza my hope damage haitakuwa kubwa
 
Kwani hawalipwi chochote baada ya kusitishiwa mikataba?Kama huna biashara ya maana mjini ni bora kurudi mkoani kujipanga kwanza!
 
Unamwachia nan? Mm nilichukua yote hata 0 haikubak yaan yote mwanzon nilijua watanipa kwa asilimia 33 ila nikawa smart nikabeba yote...pambana uchukue ufanye mambo yako

Kama ulitumia cheti cha form six unapewa hela yote,
Iko hivi kuna professional na non professional
Non professional ni zile kazi za form six kushuka chini,
Hao wanachukua hela yote,
Na professional ni zile kazi kuanzia diploma hao wanapewa asilimia.
 

Siku zote kazi ya kuajiriwa ni ya mda tu, kuna siku mambo yatabadilika
 
Ndio manake angalau uende makao makuu ya wilaya. Toka kipato cha zaidi ya milioni 2 kwa mwezi mpaka laki 3?Huoni kama hujawekeza mjini itakuwa ni tatizo kubwa KuCoup?
Ni kweli, ila ni mtazamo, ukikaza hata hapa hapa mjini unatoboa
 
Hiyo ya kulipwa na NSSF kila mwezi inategemea na umri wako, kama una less than 55 unakua huna sifa but again inategemea kama michango haijafilisha miezi 180 hata kama una 55 and above bado huna sifa, is either utafute kazi ili uunge hiyo michango hadi ifikishe 180 or else utapewa mzigo kamili uende ukafe na shida/raha zako
 
Ni kweli, ila ni mtazamo, ukikaza hata hapa hapa mjini unatoboa
Itahitajika discipline ya kiwango cha PhD.Kwanza unaweza kuanza kupata pressure toka kwa marafiki,mwenza na hata watoto baada ya kipato kushuka.Hiyo inaweza kukutoa kwenye mstari wa malengo yako.Mkoani hakuna matumizi makubwa kuliko Dar.Mfano Unaweza kutumia gari mara chache kuliko Dar.Vyakula ni bei rahisi zaidi n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…