Kwa wale waliosoma Seminari za Katoliki

Mi nimesoma pale allahu Akbar catholic seminary.....niliiifunza mengi km mnavoona Tabia zetu na misimamo yeti tuliopita hapo
 
nyie waseminary wa kikatoliki wengi wenu ni wajinga na wapumbavu kabisa, huku chuoni ndio mnongoza kwa ufuska, hamsali tena eti mshasali sana, waoga kumkiri kristo hata wengine hamtaki kujiita wakristo, huu ni unafiki na uzandiki, kanisa limewapa elimu bora badala ya kuitumia kulisaidia kanisa na taifa mmekengeuka, badilishen njia zenu na muungame mmurudie kristo, anaebisha juu ua haya tafadhali awaangalie WENGI wa waseminary waluoko vyuoni ni aibu kubea kwa kanisa katoliki.
 
mtu yeyote aliyepita seminari na akashindwa kujengeka huko huyo hafai kabisa. Pale ni sehemu kujenga watu si mchezo
 
Unanikumbusha Uru Seminari enzi za rector Pepe na msaidizi wake Cha Umeme. Dah, shule ilikuwa kama jeshi vile. Ole wako ukutwe na kosa. Na kama kawaida, maisha ya ndani kwa ndani na changamoto zake. Ukiona mdada kapita, unatoa macho kama kinyonga, si ukame! Hadi mtoke out Jumapili moja ya mwezi, kazi ipo. Ni maisha fulani hivi ya nidhamu, chezea upandere wewe?
 

Nilikuwa na mawazo kama hayo kabla sijatoka seminarini hizo nilikuwa nazisikia sana lakini nilipotoka nikajua kwanini wengi wenu ambao hamkuwahi kuwa waseminari mmejipa kazi ya Mungu, mmekuwa dart throwers. Siwatetei waseminari lakini naamini wanafanya vizuri naamini wangekuwa mafuska kama unavosema wengi wangekuwa hawajafanikiwa kabisa kimaisha lakini wengi wamefanikiwa na wapo sehemu nzuri tu.

Ushauri wangu msijifanye mnawajudge wengine wakati nyie wenyewe hampo perfect,hoja unayosema kumkiri kristo nadhani wewe unafanya kama vile mafarisayo yaani unataka uonekane mbele za watu ndio uonekane kuwa unamjua Mungu na unaishi kadiri Mungu atakavyo
 
St joseph or kaengesa seminary...dah enzi za mzee matipa na sangu mkubwa kama lector...issue za kuchoma mahindi msituni....issue za kukata mkia form one...tarehe tisa mwizi wa tisa saa tisa usiku....

Rector sio lector
 
Mbona St.MAJUSE VISIGA SEMINARY siwaoni humu
 
hongereni wandugu mliolelewa kifikra zaidi,kimaadili zaidi na kiimani huko st.....ila komboeni hiki kizazi cha digitali.
 
Binafsi ni tunda la Makoko Seminary pale Musoma miaka ya Recta, Fumakule aka Dudu (RIP). Nathubutu kusema hakuna maisha magumu kama maisha ya seminary na hakuna maisha mazuri kama ya seminary. Mtu aliyesoma seminary anaweza kufit sehemu yoyote hata pawe vipi, hata jeshini hata tetereka, mifano ipo.

Maisha yale humbadilisha mtu kisaikolojia na kumfanya awe tofauti kabisa na watu wengine. Awe mpole popote, anakuwa muoga, mkimya, mcha Mungu, mwelewa na asiyependa malumbano. Na amini usiamini mseminary huwa mwoga wa kutenda dhambi hasa uzinzi awapo bado seminary. Tatizo linakuja pale anapomaliza ama kwenda shule hizo za mchanganyiko, ni kama mbwa kafunguliwa... hutembeza dudu balaaa. Ushahidi upo.

Kingine ambacho hutukumba waseminary wengi ni kutokuwa na ham tena ya kusali ama kujishughulisha na mambo ya imani. Wengi huwa wapinzani wa imani na kuona kwamba kila kitu ni kawaida. Nadhani hii inachangiwa na mambo ya kule seminarini, maana kule ni kusali full, yani kila siku, mara novena, mara rosari, mara mifungo, mara joint mass.

Lakini tathmini inaonesha waseminary ni watu wa maadili popote walipo na hufanya vizuri makazini na popote huwa viongozi.

Nami pia useminary umenisaidia hadi hapa nilipo.

Nawamis sana maclassmate wangu, Max Pole, Deo Shija, Muhija, Blaz Ndege, Manoja, Lusajo Baraka, Deo Bwire, Kamese, Cistantin Mnaku n.k.
 
St joseph or kaengesa seminary...dah enzi za mzee matipa na sangu mkubwa kama lector...issue za kuchoma mahindi msituni....issue za kukata mkia form one...tarehe tisa mwizi wa tisa saa tisa usiku....
Ni Rector.....Sio Lector....

Kwa Kiswahili anaitwa Gombera....

Mlikuwa mnawakata mikia 'wafollow' eeeh!....

Vp kuhusu 'kuchinja mbuzi'......Teh teh.....
 

Shule za mchangani hizi hatutaki majadiliano yenu wezi wa mitihani
 
seminary sio me naona walinihalibu tu, kufungiwa ndani sana, pale nilipokuwa kwenye makundi ya watu wengi walinitambua ni product ya seminary bila hata kuuliza.. Nakumbuka nilipokuwa form one vijana wa form four walitimuliwa wote bila hata huruma, basi mwaka huo hapakuwa na form four wahitimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…