St. James' Seminary nakumbuka tulikuwa na upinzani wa jadi na Maua seminary.....
Siku moja wakaja kwenye match pale "uarabuni" tikawapiga 4 na wakaanzisha fujo...sie tukafungua stoo ya slesha naamini siku hiyo wanaMaua wengi walifika kwao kwa miguu maana walitawanyika sana.
Tulipoenda kwao waliogopa kufanya fujo ila nao wakatuiga 4. Enzi hizo kikosi kina watu kama Aron Mwaituka, Mdee, Peter Imani (golie), Aristariki Mwenyeheri a.k.a Beki..huyu wengi walikuwa hawamjui jina hata baadhi ya walimu walimuita BEKI. Jamaa alikuwa na bifu na viatu uwanjani na siku aliyovaa viatu muda mrefu uwanjani ni dakika 7 kwenye match kule Chanjale sem. Tatizo lilikuwa kwenye kumpita. Pia kulikuwa na wachezaji kama vile Sadiki Mwamlima ( aliwaui kuichezea Tukuyu stars kabla ya kuja SAJASE) , Mponzi, Aristablas Macha....na mimi mwenyewe.
Namkumbuka Father Landelin Makiluli alipokuja akiwa Frater...alikuwa anadokoa makwenzi hasa..
Fr Maramba.... Fr Mavumilio....Fr Ruwaichi a.ka. KP... Fr Kenyange....sister Anna (nadhani walienda kuanzisha Anwarite Girls)...Sister Edith...Sister Epimark.... mzee Gabriel....Fr Negro....Fr Kajetan Kazi (huyu sijui kama zilikuwa zinamtosha) Fr Nderumaki....Fr A. Makusaro ( nilibahatika kumuona mwaka jana ile TZC yake bado anayo)
Nilikuwa mtaalamu wa kula VENJA na nilikuwa na MIGODI kadhaa ya MBUNENE na ndizi kule pg project.
Sitasahau siku Ruwaichi alipovizia mgodini na kutukamata mbaya zaidi nikisema " tufanye fasta KP asitukamate" hakuwa na makuu zaidi ya kunitaka nimuambie tu maana ya KP...akili ilifanya kazi ya ziada nikamuambia maana yake ni Kenyan Police....akauliza kwa nini tunamuita vile? Nikaanza kummwagia sifa na kumuambia " hivi Fr ulishaenda jeshi....tunakuita Kenya Polisi maana uko sharp kama wao...ona hata hapa ulivyotukamata kama kuku" alivyopenda kusifiwa akatuambia malizeni kula mkaendelee na kazi.
Next time aliponikamata na miwa mie na group yangu hakutuelewa bali alitufunga mashati na kutuzungusha shule nzima tumebeba miwa yetu huku tunaimba " sisi ni wezi" . Hakika hadi leo sithubutu kuiba chochote.
Nakumbuka pia siku niliyododge kazi kwa saa 1 tu wakati Fr Negro akiwa anasimamia kazi.. wakati huo nilikuwa nafanya kule Phyisics Lab. Negro alinitafuta na nilipopatikana jioni alifanya calculations za muda wa watu wote niliopoteza na ikatakiwa niwalipe...mwisho wa hesabu ikaonekana ninatakiwa kufanya kazi saa 8 kwa siku kwa muda wa siku 36.... kwa sasa huwa ninapata zawadi za mfanyakazi bora ofisini.
Siwezi kusahau tukio la kufariki kwa mwenzetu Gilbert Riziki a.k.a Njuka (R.I.P) wakati tunatoka shambani Masaera. Huyu jamaa wakati huo alikuwa i/c wangu kule Box room na kwa mbwa.
Nakumbuka ratiba ilivyokuwa tight hadi watu walikuwa wakilala na uniform.
Nakumbuka ujanja wa kusaka "VIWAVI" kule Mandaka na wakati mwingine kuvuka mto hadi St. Magreth.
Hakika nikisahau wema wa St. James mkono wangu wa kuume na unyauke.
Baadae nilikuja kwenda Usa Seminary (FREEDOM SQUARE) kwa A-level.