Kwa wale waliosoma Seminari za Katoliki

Kipindi hicho mlikuwa watata. Enzi zetu za miaka ya juzijuzi ukiongea kidogo tu unaweza kukaribia kuondoka.
 

Pia ninakumbuka kuna siku ilikuwa birthday ya baba Gombera ila cha ajabu siku hiyo hawakuleta mbege ila soda peke yake....
Nakumbuka siku hiyo hapakukalika kwani watu tuliungana tukagomea sherehe hadi mbege iletwe... maFr walifanya kazi ya ziada kutushawishi tunywe tu soda.
Pia nilikuwa mtaalamu wa kuwapa wengine majina ila bahati nzuri hakuna aliyethubutu kunipa jina la utan. Maisha yalikuwa mazuri kuliko kipindi kingine chochote.
 
Mi pia nimesoma seminary.
Basi unaambiwa tulikua tunasoma darasa moja na masista wawili wakaliii enzi hizo.
Mapadri waliokuwa walezi wetu na pia maticha, walikua wanawagombania hao watoto mpaka zikawa zinapigwa.
Ilibidi wale masista wahamishwe na tokea mwaka huo masista hawapelekwi kusoma iyo seminari.
 
Kipindi hicho mlikuwa watata. Enzi zetu za miaka ya juzijuzi ukiongea kidogo tu unaweza kukaribia kuondoka.

Si kwamba tulikuwa watata bali tulikuwa tukifanya plan za uhakika bila kabla ya kufanya jambo... Always nilikuwa na Plan B na C...
Kuna siku tumetoroka wanne kwenda st. Magreth kuna jamaa wa darasa la mbele walinipatia hela kidogo kwa lengo la kuwafanyia mpango wa kwenda St.Magreth. Kidume nikaandaa mipango na baada ya muda wa masifu ya jioni tukaanza safari. (kipindi hicho simu zilikuwa adimu sana).
Kwenye plan ilikuwa imeshatumwa barua kwa wale viwavi watusubiri kwenye uzio wa shule yao...bila kujua kuwa wale viwavi wameshakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku wakitusubiri.
Wanaume tukafika na kupenya kwenye tundu nililokuwa nikilitumia kuingia huko. Ile anamaliza wa mwisho tukasikia "chini ya ulinzi" ...kutahamaki pale pembeni kuna mlinzi na gobore lake.
Niliwaza kwa kasi kuwa pale ni kufukuzwa tu shule kwani Gombera alishasema nikamatwe red handed anihukumu. Pia nilijiona ninafukuzwa shule huku hakuna hata kiwavi niliyemfuata ila kwa kuwa tu master mind wa mkakati.
Nyumbani kuna gobore hivyo najua ili upige risasi unahitaji zaidi ya sekunde 5.Kwa wakati ule nilihitaji sekunde 2 tu kujinusuru. Mithili ya umeme nilichomoka kwa kasi na kuruka uzio ule wa wavu kabla ya mlinzi kujua cha kufanya.
Sikusimama popote nilikimbia kwa kasi niwezavyo (bahati njema nilikuwa mchezaji na kipindi cha likizo nilikuwa nikishiriki riadha mtaani)... Nilikatiza kule mtoni kama vile hakuna mabonde.
Kama nilivyosema simu zilikuwa adimu hivyo nilijua wazi kuwa mlinzi hakuwa na simu hivyo kutoa taarifa ni lazima awadhibiti mayeka wake kisha ndio apeleke taarifa kwa uongozi wa shule kisha nao watoe taarifa SAJASE. Nilikadiria watahitaji dakika 20 hivi na mimi sikuhitaji muda wote huo.
Nilifika shule nikaingilia upande wa uwanjani kwa juu. Nikakatiza uwanja wa basket kisha nikaingia majuu na kutulia huku ninacheki usalama halafu bila kupoteza muda nikaingia chumbani...(kile chumba pembeni ya ofisi ya nidhamu)....
Sikuweza hata kuvua viatu nikapanda kitandani navyo na kujifunika. Wakati huo transfoma ilikuwa imeungua na tulikuwa tumemaliza mitihani hivyo jenereta liliwashwa kwa muda tu kisha tukaenda kulala.
Huku nyuma wenzangu waliokamatwa walihojiwa na wakanitaja.( my rule no 1: die alone...hakuna kutajana) kisha simu ikapigwa SAJASE kisha nikaanza kutafutwa.... Kwa mawazo yao ni kuwa kwa muda ule nisingeweza kufika shuleni kwa vyovyote. Kunitafuta ilikuwa ni sehemu ya kujenga ushahidi kwamba sikuwepo shuleni. Mwisho walikuja chumbani kwetu na kuja hadi kitandani kwangu (enzi hizo majina na namba ya kitanda yanawekwa mlangoni). Hawakuamini macho yao waliponikuta nimelala na waliponiamsha nikaamka kwa hasira kwani walinimulika na tochi. Ilibidi wapige simu tena kuuliza jina kama wamekosea (wangenifunua wangegundua nimevaa viatu bado)....
Ilibidi waniacha hadi asubuhi wale wengine walipoletwa shule kisha wakanitaja....kumbuka wamevunja sheria ya mastermind hivyo ni kuwakana tu! Niliitwa kuhojiwa na yule mlinzi alipoletwa anitambue alishindwa kabisa...mie nikamwambia mwalimu wa nidhamu kuwa "wewe unajua uhasama unaokuwepo kati ya madarasa yetu...inawezekana vipi nikashirikiana nao? Hakika hawakuwa na mimi na ninyi walimu ni mashahidi mliniamsha jana usiku..."
Jumatatu inayofuata wale jamaa walifukuzwa shule ika kama kawaida Makusaro hakuacha kunipa onyo...." Isaac jiangali, jiangalie wakati mwingine nitakufukuza, nitakufukuza,,,nssssssh nssssh"
Ilikuwa mara yangu ya mwisho kutoroka usiku....
 

Hii inaweza kuwa maua seminary?
Huku ndio niliona masister siku moja tulipoenda kwa debate....
Pale St. James' alikuja waziri fulani akataka mwanae wa kike aje kusoma pale... Gombera Makusaro alimwambia yule waziri kuwa nafasi zipo ila inabidi aende kwanza kwa paroko wake amlete....hadi tunaondoka sikumuona yule waziri tena....
 
Kuna mtu alikuwa anaitwa Msiri. Ndiye askofu Isaack wa Jimbo la Moshi. Jamaa alikuwa mjuzi wa kukamata ila mm aligonga mwamba alipokaribia ku.nikamata nikiwa nakula venture. Ahhh Alikuwa discipline master akiwa chine ya mwingine aliitwa Field Marshal ambaye ni Fr Riziki akiwa ndiye Rector
 

ha ha ha ha mkuu umetisha sana.........yani umenifahisha mno.....mastermind rule no.1. Ukishikwa hakuna kutajana kufa mwenyewe.
 
Isaac umetisha, una historia nzuri ya kuwa na uwezo wa ku'bear' risk na kuhakikisha kwamba hudhuriki na matokeo. Ungefaa kuwa mwanausalama siku hizi. Ila I'm sure huko ulipo watu wanaenjoy umaster mind ulio nao. Sina cha kujivunia katika risk management, ila nnachokumbuka nilikuwa na uwezo mzuri wa kujenga hoja, kiasi mara nyingi nikifunguka maneno yalikuwa na impact. Niliogopeka kama mchochezi. Siku za mwisho sikumaliza kwa amani sana. Ila sajase ni baba lao.
 
hivi unawapata machalii fulani ndunguru na lyimo aisee...hivi hawa madogo wapo wapi sasa hivi mana nilikuwa nikisikia story zao.....
 
St joseph or kaengesa seminary...dah enzi za mzee matipa na sangu mkubwa kama lector...issue za kuchoma mahindi msituni....issue za kukata mkia form one...tarehe tisa mwizi wa tisa saa tisa usiku....

unamkumbuka padri nandi yule jamaa alikuwa na itikadi za kilokole
 
Sister Edith alikuwa mwl hesabu wa aina yake.

Sister Edith tumemfundisha wenyewe hesabu za kibongo. Tulikua tunamsolvia past papers za miaka ya nyuma. Sio kwamba alikua mweupe sana ila India alisoma General Maths alikua hawezi nyanga za kukomoana za NECTA.
 
Sister Edith tumemfundisha wenyewe hesabu za kibongo. Tulikua tunamsolvia past papers za miaka ya nyuma. Sio kwamba alikua mweupe sana ila India alisoma General Maths alikua hawezi nyanga za kukomoana za NECTA.

kumbe hesabu ya Tanzania na india zipo tofauti mkuu...
 
hivi unawapata machalii fulani ndunguru na lyimo aisee...hivi hawa madogo wapo wapi sasa hivi mana nilikuwa nikisikia story zao.....

Ndunguru na Lyimo walianzia f.5 hapo mi nkiwa f.3 mwaka 2008. Lyimo hakufanikiwa kumalizia hapo na hata sikujua alienda chuo gani. Ndunguru alimaliza fresh, nadhani alienda udsm. Ila nnachokumbuka wale jamaa walikuwa talented katika maswala ya social.
 

aisee hivi lyimo hakumaliza....nasikia hawa jamaa walipinda sana mkuu mana wakati wetu tulisomaga na jamaa fulani walitoka shule yao.
 
Binafsi ninaamini huwezi kufanikiwa kwenye jambo lolote kama utaogopa risk zake.....Pamoja na hayo nilikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza hata kwa maandishi. Nakumbuka tukiwa kidato cha 3 wakati huo fr Mavumilio anatufundisha Kiswahili tulikuwa tukisoma riwaya ya zawadi ya Ushindi. Kutokana na kuwa busy kuplan mambo sikuweza kukisoma ila siku ya mtihani ile tunajiandaa kuingia niliuliza majina ya wahusika na kwnye mtihani mie ndio niliweza kupata maksi zote za swali lile.
 

extraordinary mkuu...
 

ha ha ha umetisha kiongozi....mm hiyo jina unayotumia imeniacha hoi vibaya...
 

majina mnayotumia humu jf yani yananifurahisha ha ha ha ha eti kaka jambazi ha ha ha ah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…