Kwa wale waliowahi kutunza siri nzito kwa muda mrefu tukutane hapa

ngoja watu waje kubashiri.....

Hapo hakuna kitu mkubwa, nnavyosema namaanisha hakuna mtu anaejua kama najua. Kuna nilivyofanya, nilivyoona, achilia mbali nilivyosimuliwa.

kadri unavyojua mambo mengi zaidi ya watu ndio unavyozidi kujihatarishia maisha yako.
 
Kuna vitu sitakuja kuvisema hadi nazikwa, iwe kwa anaenifahamu au asiyenifaham. Iwe ni kwa kuandika au kwa kuongea. Sitakuja kusema.
Hiyo ndio inaitwa siri! Maana hata kama hujulikani na ukaisema, hiyo si siri tena!
 
Daaahh Nina siri ya uchaguzi 2015..Yaaani hawa jamaa nawatunzia siri zao mpaka sasa halafu wamenitupa kama hawajui Nina siri nzito.Kama mheshimiwa unapita humu tafadhali nikumbuke ktk ufalme wako.Mzee wangu Jo unakumbuka sikuwa nikilala,usiku na mchana tunahangaika,Leo mumenitupa jamanii.
 
Mfalme alikuwa na kinyozi maalumu wa kumtunzia siri ya kipembe kichwani. Kinyozi alikwenda porini akachimba shimo, akainama na kutamka 'mfalme ana pembe' na kisha kufukia shimo. Siri ni ngumu kutunza.
 
Nmecheka sana hiii.. Huyo Mecky balaa
 
Hahahahahaaaaa uncle mecky nouma
 
Mimi siri yangu ambayo iko moyoni na inanitesa ni kumla mke wa jirani yangu na kumpa mimba(Zamani lakini) mpaka leo nikimwona jamaa huwa najutia sana, kweli kutoka moyoni najutia sana kitendo kile japo mkewe alikuwa mzuri sana
 
Kuna kitu tofauti Mungu kakiweka ndani yako/Pia mwonekano wako ndio maana wanakuja tu siyo Bahatimbaya

Mimi unakuta Mtu mzima au Hata wazee anakuja kuomba Ushauri au analalamika kwangu na anafunguka kweli,Maskini wa Mungu sina Elimu kubwa wala Maendeleo/Mali nyingi na wengine Wananiogopa ata namna ya kuanza kuongea nami Bc nikijiangalia najishangaa Najitafakari sina lolote wala Chochete.
 
Nilimaliza shule ya msingi jijini DSM , kutoka shule ile tulichaguliwa watu 10 kujiunga na sekondary ( kumbuka enzi zile haikuwa rahisi watu kujiunga na secondary za umma wadada 4 wakaka 6 ) , japo baadaye nilikuja kuhama shule za umma , kuelekea shule ya sekondari niliyopelekwa tuliotoka shule 1 ya msingi tulichaguliwa wawili tu na tulipangwa pamoja form 1 Q , kiukweli nilishangaa mtu niliyejiunga naye form 1 si yule niliyefanya naye mtihani wa kumaliza darasa la 7 , sikuwahi kumuuliza yeye binafsi wala sikuwahi kumuambia mtu yeyote kuhusu jambo lile hadi leo , japo yeye alionekana kudokezwa kuhusu mimi na aliniheshimu kwa miaka miwili niliyosoma naye
 
Kuna siri mwanaume unazikwa nazo, yaani hata ukuta hauuambii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…