Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Hizo nyumba kwa nje zimechoka sn Lkn ndani wanatoka viumbe warembo vibaya wakinyamwezi!

Siku ya jtano usiku bendi ya tabora jazz ilikua inatoa burudani pale unyanyembe social hall karibu na soko kuu mida ya saa nne usiku utasikia ukiw mitaa ya Chemchem near Kwa wanaume Milambo School nyimbo zinasikika "Ooooh najuta ....nifanye nini sasa....pole kaka mimi ni bado msichana....!"

Kulikua na mabasi ya kwenda Urambo yana carrier juu, road ikiwa ni vumbi nasikia siku hizi ni lami enz hizo stend mpya haijafunguliwa na mh Ben Mkapa aliyekuja kuifungua baadae sna akiwa anatembelea mkongojo kipindi hicho.

Redio za FM ilikua hakuna had baadae sana ikaja RFA na hizi za CG FM na VOT, voice of Tabora zikafuata.

Ukitembea njiani unaangukiwa na maembe aliyoacha Mwarabu ile njia ya karibu na NMB kwa nyuma imejaa miembe njiani
 
Disco la mwanaisungu, tabora hotel.
Basketball kwenye grounds za uhazili.
Nani alisoma mwenge, kipindi cha mwalimu chiboni?
enzi za akina ADAM mabreka
enzi za babu JEFF MIHAYO SEC.na mihogo ya ya kukaanga
enzi za kina silencer na ubabe wa mjini polisi hawamtishi.
enzi za baiskeli za cheng zcheng kila mwenye nayo ujue ni mwanajeshi.
enzi ya team ya TINDO ya watoto wa mjini.
 
Disco la mwanaisungu, tabora hotel.
Basketball kwenye grounds za uhazili.
Nani alisoma mwenge, kipindi cha mwalimu chiboni?
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.

Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?
 
Duu sitasahau ugomvi wa Tabora boys na milambo wakigombea mademu wa kazima Enzi hizo kazima kulikuwa
na warembo....mwenye no ya evelini kisenge tafadhali....fungulia dog ya mwanaisungu club.tuliopo Dar tutafutane jamani
 
Mimi zaidi Tabora naikumbuka timu ya Milambo enzi hizo mwanzoni mwa miaka ya tisini inapanda daraja na kuingia ligi kuu kwa kishindo.

Kupitia juhudi za mkuu wa mkoa wa wakati huo Marehemu Laurence Gama na Mfadhili wa timu, Muasia mmoja aliyefahamika kwa jina la Kanji, Milambo ilikuwa na wachezaji kama Godwin Mashoto, Job Ayubu, Ferez Teru, Mikidadi Jumanne(Bubu), Mrisho Moshi, Ali Manyanya nk.
Nilikuwa sikosi mechi uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kama siku sina pesa basi ilibidi 'Fungulia Mbwa' itumike!!
 
Kuna mchizi mmoja alikuwa anaitwa teacher ! Au kwa jina jingine Matola alikuwa anapendelea sana kukaa pale stendi ya basi na kwa mayor hoteli
Au wakati mwingine unamkuta mitaa ya bachu! Mnamkunbuka??
Na mwingine Ali tola!

Teh teh teh
Cc mtemi usike Mboka Manyema
 
Last edited by a moderator:
nilisoma boizia 95_97, njia yetu kwenda mjin kwa kumuogopa MADAFU ilikuwa chocho za Rufita_National_Kitete_then Kanyenye, tulikuwa tunakula bakora za maafande hasa afande CHACHA_kumamamamake. mahasimu wetu MIRAMBO kwa ajili ya geloz na wote tulikuwa ni mapenz ya barua tu yaan hata mkikutana huwez kumwambia_unapiga story nyingine halaf mwishon unatupia letter akasomee chumban
 
Tabora bazar na vitumbua vya mzee simba pale diamond talks wakti wa magharibi na kombe la maziwa moto!!
Usinifanye nikaanza kulia saa hii!
Na wakunibembeleza yuko safari.


Rafiki Yangu kahtaan bora tupige story tukumbushane mambo ya nyuma kuliko mijadala ya Imani kule!

Mwanangu umemtaja Yule Mwehu Teacher umenikumbusha mbali sn! Nakupa majina ya wehu wengine! Malingumu na mwingine Roshi, na Aziza Moka na Yule Muhindi Wa kwa Athumani Store na Amani Mwehu, Mwajuma Ringa?


Vp wawakumbuka wale Mbuzi waliokua wanajichunga wenyewe?

Wayakumbuka mabasi ya Mpalaye?

Mboka Manyema ni balaaaa Mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Tabora bazar na vitumbua vya mzee simba pale diamond talks wakti wa magharibi na kombe la maziwa moto!!
Usinifanye nikaanza kulia saa hii!
Na wakunibembeleza yuko safari.

tulikuwa tukienda kusali ijumaa na tukiwa na hela tunapita hapo Diamond Talkies tunagonga mtind na madiko diko then tunaanza safar ya kurud boizia_lile jengo liliharibiwa kwel maana baadae liligeuzwa booking office na store ya Mohammed Trans, siku hiz mpaka Usoke ni lami na muda si mrefu mpaka URAMBO kwa PATEL itakuwa Lami, TAMUSA TBR _hatareeee
 
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.
Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.


Umesahau mengine yanaitwa Mfulu Na Magongoti!
 
Back
Top Bottom