Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na kukataa dini yake je , uovu na shari mnatambuaje ?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja ...

Kuna kundi la watu kubwa wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu ila wanasema dini ni utapeli wakimaanisha hizi dini mbili maarufu Uislamu na Ukristo na kwamba Mungu yupo kweli ila hakuketa dini, vitabu , miongozo wala kutuma wajumbe (Manabii na Mitume )

Nauliza je , inawezekana Mwenyewe Mungu atuumbe tu Kisha asiweke miongozo na utaratibu kwa viumbe wake kuishi ? kama hata familia ,shule , taasisi , nchi nk Kuna miongozo na kanuni vipi kwa wanadamu tuliumbwa na kuachwa bure ?

Je , unatambua vipi kuwa jambo hili zuri au baya na kwa kutumia vigezo vipi ?

Tukisema kwa kutumia akili na utashi wa kawaida je , utashi wa mtu ukaaamua ni ruhusa mtu kumuoa na kumuingilia mwanae au mtoto wake tunaweza vipi kumkubalia au kumkatalia ?

Utashi na akili ishafeli binadamu kukubaliana kwenye uovu na shari ndio maana unakuta Sheria mbalimbali zinabadilika kutokana na wakati au mahali . Mfano baadhi ya sehemu kujiua ni ruhusa ipo kisheria , baadhi ya sehemu ni makosa , nyakati za zamani biashara ya utumwa ilikuwa inaonekana ni jambo la kawaida sasa haionekani hivyo .

Hata Jf waliounda hawakuiacha bure waliweka Sheria , miongozo na mipaka katika majadiliano . Hii simu ninayotumia sasa nilikuta Manual guide ya jinsi ya kutumia pomoja na precautions wakati nanunua .

Je , wewe unayeamini katika Mungu na kukataa kuwa hakuacha miongozo ya dini kwa wanadamu unatumia nini kupima Shari na Uovu .

Kama Kuna aliyemuumba Mwanadamu ambaye ni Mungu je ,inawezekana kumuacha bure tu bila muongozo juu ya namna gani aishi ?

#Uzi Tayari

046e3dba4a32729d174f87f25744c395.jpg
 
View attachment 3687696
Mkuu, mimi naamini Mungu yupo na siamini kwamba alituumba bila kutupa mwongozo. Akili ya binadamu ina mipaka na dhamiri za watu hutofautiana.

Swali langu ni hili: kama kila mtu akiamua mwenyewe jema na baya, tutapataje kipimo cha haki kinachovuka matakwa ya mtu binafsi? Kwangu, kuamini Mungu ni hatua moja, kutafuta ukweli kuhusu mwongozo wake ni hatua nyingine.
 
Fafanua hiyo 'objective morality ' mkuu wamatumbi tuelewe .
msaada wa AI, Objective morality is the philosophical idea that moral truths (what is right or wrong) exist independently of human opinions, feelings, or cultural beliefs.

hua inakuaga debate kali sana, kwa kifupi ni mtanange
 
Evolution ndio inakufanya usimtamani kingono mtoto wako, dada yako, kaka yako, mdogo, wazazi wako na ndugu wengine wa karibu, sio dini.

Dini inazuia kucheza kamari lakini watu wanachezea kamari, inazuia pombe lakini watu wanakunywa pombe, wanaiba, wanadhulumu, wanafanya ngono nje ya ndoa n.k
 
Evolution ndio inakufanya usimtamani kingono mtoto wako, dada yako, kaka yako, mdogo, wazazi wako na ndugu wengine wa karibu, sio dini.
Mbona wapo ambao wamefanya hayo kulala watu wa familia ?

Je , vipi kuhusu wanaume kulana mbona wanakulana sana tu hiyo evolution inafanyaje kazi ?
 
Mkuu wengi wanachokikataa sio uwepo wa miongozo.
Shida inakuja Mungu mmoja lengo lile lile juu ya viumbe wake kwanini Miongozo itofautiane nakati Mungu ni mmoja?
Mfano
Mungu mmoja alieleta miongozo kupitia manabii kwanini sasa mfano biblia na Qur an zitofautiane katika miongozo kama vile namna ya kuswali/kusali..
Kwanini sasa Mungu mmoja karibu kila jamii iletewe mwenyekuwakilisha miongozo yake Mungu halafu jamii zingine zisiletewe?mfano kwanini Mungu hakuleta sheria kwa waafrika kupitia nabii wa kiafrika?
 
Moja kwa moja ...

Kuna kundi la watu kubwa wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu ila wanasema dini ni utapeli wakimaanisha hizi dini mbili maarufu Uislamu na Ukristo na kwamba Mungu yupo kweli ila hakuketa dini, vitabu , miongozo wala kutuma wajumbe (Manabii na Mitume )

Nauliza je , inawezekana Mwenyewe Mungu atuumbe tu Kisha asiweke miongozo na utaratibu kwa viumbe wake kuishi ? kama hata familia ,shule , taasisi , nchi nk Kuna miongozo na kanuni vipi kwa wanadamu tuliumbwa na kuachwa bure ?

Je , unatambua vipi kuwa jambo hili zuri au baya na kwa kutumia vigezo vipi ?

Tukisema kwa kutumia akili na utashi wa kawaida je , utashi wa mtu ukaaamua ni ruhusa mtu kumuoa na kumuingilia mwanae au mtoto wake tunaweza vipi kumkubalia au kumkatalia ?

Utashi na akili ishafeli binadamu kukubaliana kwenye uovu na shari ndio maana unakuta Sheria mbalimbali zinabadilika kutokana na wakati au mahali . Mfano baadhi ya sehemu kujiua ni ruhusa ipo kisheria , baadhi ya sehemu ni makosa , nyakati za zamani biashara ya utumwa ilikuwa inaonekana ni jambo la kawaida sasa haionekani hivyo .

Hata Jf waliounda hawakuiacha bure waliweka Sheria , miongozo na mipaka katika majadiliano . Hii simu ninayotumia sasa nilikuta Manual guide ya jinsi ya kutumia pomoja na precautions wakati nanunua .

Je , wewe unayeamini katika Mungu na kukataa kuwa hakuacha miongozo ya dini kwa wanadamu unatumia nini kupima Shari na Uovu .

Kama Kuna aliyemuumba Mwanadamu ambaye ni Mungu je ,inawezekana kumuacha bure tu bila muongozo juu ya namna gani aishi ?

#Uzi Tayari

View attachment 3687696
Dini hazikukataza utumwa,
Dini ya WaIsrael iliwaagiza waue wafilisti, Waameleki na mataifa wengine,
Muhammad alioa mtoto wa miaka 6,
Muhammad aliruhusu wanawake mateka wa vita watumike kingono,
Muhammad aliwatoza wasio Waislamu tozo ili kuishi chini ya himaya ya Uislamu,
Quran inaagiza kuwaua wasioamini,
Kuna vita za kidini

Maadili yako wapi katika haya yote ??
 
Muhammad aliwatoza wasio Wakristo tozo ili kuishi chini ya himaya ya Uislamu,
Quran inaagiza kuwaua wasioamini,
Kuna vita za kidini

Maadili yako wapi katika haya yote ??
Sijasema Dini inakataza utumwa , nimezungumzia jamii ya kipindi hiko na ya sasa
 
Hapo nimekuonyesha maadili hayatokani na dini, kwa sababu kama maadili yanatokana na dini basi utumwa ungeandikwa kama mojawapo ya dhambi kuu kwenye Biblia na Quran.
 
Dini hazikukataza utumwa,
Dini ya WaIsrael iliwaagiza waue wafilisti, Waameleki na mataifa wengine,
Muhammad alioa mtoto wa miaka 6,
Muhammad aliruhusu wanawake mateka wa vita watumike kingono,
Muhammad aliwatoza wasio Waislamu tozo ili kuishi chini ya himaya ya Uislamu,
Quran inaagiza kuwaua wasioamini,
Kuna vita za kidini

Maadili yako wapi katika haya yote ??
Hayo ni matokeo ya kufuata Uislamu kwa propaganda na mitandaoni bila kutumia akili na kusoma .

Kuoa Binti ya miaka 6 , Uislamu unaruhusu lakini kuwa make rasmi kutumikia ndoa mpaka mtu afikie umri wa kubaleghe kama Mwanamke avunje ungo na aridhie , sasa ubaya uko wapi mtu akishakomaa kwa ajili ya ndoa kuolewa ?

Point nilizoweka rangi nyekundu na Nyeusi huoni kama unajiContradict mwenyewe ? ndio maana nawaambia someni na tumieni akili .

Kwenye nyeusi umesema "Muhammad aliwatoza wasio Waislamu tozo ili kuishi chini ya himaya ya Uislamu " kwenye nyekundu umesema " Qur'an imeagiza kuwa wasio amini "

Kama wasioamini wanahitajika kuuwawa unconditionally Sasa kwa nini kuwe na tozo kwa wasioamini wakati kila siku mnasema Uislamu unahimiza kuuwa Makafiri (Wasioamini ) ?
 
Ni binadamu wachache sana wanaotamani kufanya mapenzi na ndugu zao wa karibu, wengine ni maagizo ya waganga. Hata bila Sheria za dini binadamu wengi hawawezi kuwa na hamu ya ngono na watoto wao au wazazi wao.
Kwanza wewe ni Atheist au theist ?

Na nyenzo ipo bora wanadamu watumie kuJudge maadili ?
 
Hayo ni matokeo ya kufuata Uislamu kwa propaganda na mitandaoni bila kutumia akili na kusoma .

Kuoa Binti ya miaka 6 , Uislamu unaruhusu lakini kuwa make rasmi kutumikia ndoa mpaka mtu afikie umri wa kubaleghe kama Mwanamke avunje ungo na aridhie , sasa ubaya uko wapi mtu akishakomaa kwa ajili ya ndoa kuolewa ?

Point nilizoweka rangi nyekundu na Nyeusi huoni kama unajiContradict mwenyewe ? ndio maana nawaambia someni na tumieni akili .

Kwenye nyeusi umesema "Muhammad aliwatoza wasio Waislamu tozo ili kuishi chini ya himaya ya Uislamu " kwenye nyekundu umesema " Qur'an imeagiza kuwa wasio amini "

Kama wasioamini wanahitajika kuuwawa unconditionally Sasa kwa nini kuwe na tozo kwa wasioamini wakati kila siku mnasema Uislamu unahimiza kuuwa Makafiri (Wasioamini ) ?
Kuoa mtoto wa miaka 6 ni ujima na pedophilea, iwe unafanya naye ngono au hufanyi naye.

Kujichanganya (contradictions) kwa vitabu vya dini ni jambo la kawaida sana, hiyo ni dalili nyingine hivyo vinavyoitwa vitabu vya mungu viliandikwa tu na kukusanywa na watu wasio na elimu, teknolojia na maendeleo sasa hivi yanawaumbua.
 
, Gaza , Algeria masinagogi bado yapo nkKuoa mtoto wa miaka 6 ni ujima na pedophilea, iwe unafanya naye ngono au hufanyi naye.

Kujichanganya (contradictions) kwa vitabu vya dini ni jambo la kawaida sana, hiyo ni dalili nyingine hivyo vinavyoitwa vitabu vya mungu viliandikwa tu na kukusanywa na watu wasio na elimu, teknolojia na maendeleo sasa hivi yanawaumbua.
Lilikuwa jambo la kawaida sana wakati wao , hata ulimwengu wa sasa Kuna mambo ambayo miaka ya 80s , 90s yalikuwa kawaida na mtu hashangai ila sasa habari nyingine . Mfano umri wa kuanza shule na kumaliza watu walikuwa wakubwa mno tofauti kabisa na sasa .

Hakuna contradiction hiyo ni dalili kuwa nyinyi wafuata propaganda na sio wasomaji , wafuatiliaji na hamtumii akili , historically hata kwa maandiko Uislamu walikuwa na jamii za dini mbalimbali wakiwa wao watawala bila kuwauwa na waliacha mpaka nyumba zao za ibada waabudu kwa uhuru ndio maana Leo ukienda Misri unakuta makanisa ya kale
 
Unafikiri kuna wakati mungu atafanya mabadiliko katika suala la maadili kuruhusu ushoga??
Maana maadili ya mungu wako yanaenda na nyakati.
 
Maumivu na mateso.
Wajibu na Uwajibikaji.
Akija mwanao kamuelewa Mama yako ambaye Bibi yake anataka kumuoa kwa vile ni Mwanamke kama Mwanamke mwingine .

Naomba utumie hizi nyenzo kupiga au kukataa
 
Back
Top Bottom