Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Kuna aina ya push-up man, je push-up unazopiga...ni za nakoz (nuckles) mbili au zote ...na kama ni push-up za nuckles zote ni zile unakuwa kwenye flat surface au za kuweka miguu juu ya kitu kama jiwe, stuli au ukutani...150 push-ups mana ake uko fit,
na kama we unaona uko vizuri jaribu zile za vidole vitatu then uje unipe mrejesho......alafu utofautishe nuckle push-ups na palm-push-ups
Gonga TWO NUCKLES. uchane watu mashavu
IMG_20190307_090552.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani sana hizo,ndio zilikuwa zangu. Home kwangu nimetenga room kabisa. Ilikuwa kila asubuhi,saa moja na nusu namalizia hapo. Naanza na kuruka kamba na kichura hiyo dk 30 nakata. Nakuja push up zile za two nakoz tu,mkupuo wa 30,30 mara 5. Nakuja unashika mikono kwa nyuma kwenye kama mwamba wa kitanda,yaani unaukigeukia huo mwamba unashuka chini na kupanda. Mikono tu na visigino ndio vinakuwa vimeubeba mwili. Hayo mazoezi nimeanza nayo miaka 20 iliyopita. Sasa kilichokuwa kinanitokea kila nikikomaa mayo sana ilikuwa napata bawasiri, yaani kama vidude vinatokea sehemu ya haja kubwa,kama tuvidole tudogo hivi. Wakati wa haja,nikimaliza ile mishipa ya ndani inauma. Ikawa hiyo inakuja na kupotea nikawa naendelea na mazoezi huku nikitafuta tiba. Nimehangaika sana na tiba. Hivi ninavyoongea nimeacha mazoezi kabisa,kwa sababu sasa nikifanya tu kidogo napata maumivu makali balaa. Bado nahangaikia tiba,tiba ni adimu sana. Inaniuma sana nikikumbuka mazoezi,natamani mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Polee, brooo.. Nicheki tuyajenge.

Ila ulikuwa una overload mwili wako... N unatakiwa bana zaga ukiwa na mazoez magumu, n ulaji sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Push ups 150? Za uhakika mkuu? Au zile kama unacheza ndombolo. Nimepumzika kwa sasa lakn umenikumbusha leo jioni inadidi nianze. Ila sijawahi kupiga zaidi ya 30 kwa awamu.
Maamuzi na kukomaaaa.... Ishu ni kuendelea. Fanya kila siku na usi limit nguvu ya mwili wako.... Trick ur mind, the body will obey..

Anza hivi, pale unapo ona mwili unachoka, asume hiyo ndio warm up. Anza kuhesabia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi napiga zile wyf anakaa kwa juu mgongoni, napiga za kutosha.
 
Kwani kuna tofauti gani kati ya push up za ngumi na zile za kawaida?
 
Wakuu mimi naomba tips, ninaanzaje hili zoezi. Mana nikajaribu kuenda hata moja inanishinda.
Anza kuweka mikono juu ya meza na miguu chini, piga piga hizo, nyingi nyingi, halafu punguza angle taratibu.

Au piga magoti haraf anza kupiga push ups.

Ukijenga nguvu za mikono unakuw katik flat surface, ukiwa vzuri zaidi.

Unaweka miguu juu mikono chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kifupi gym nilishaacha kwenda long time nikaamua kuanza kupiga push up home tu!

Kwa kifupi huwa naenjoy sana hasa marafiki wakija kunitembelea huwa nawapa challenge ya kushindana na Mimi huwa nacheka sana baada ya push up 15 tu wanaanza kuhema kama mbwa koko!wakati Mzee mzima hapo naenda zaidi ya push up 150

Tukutane hapa wapenda mazoezi

Sent by Diaspora
Du 150? Unatisha mzew baba!

Sent using My Xiaomi Redmi 4a
 
Back
Top Bottom