Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Aaah mazoez ya push up bwana!
Nilianzaga nikiwa bordin hapo ndo nikawa nafanya kila siku yaan tukiacha class tu muda wa michezo ni mimi na push ups kuja kustuka jimwili likubwa juu alafu vitako vidooogo......

NILIACHA!
 
Natamani sana hizo,ndio zilikuwa zangu. Home kwangu nimetenga room kabisa. Ilikuwa kila asubuhi,saa moja na nusu namalizia hapo. Naanza na kuruka kamba na kichura hiyo dk 30 nakata. Nakuja push up zile za two nakoz tu,mkupuo wa 30,30 mara 5. Nakuja unashika mikono kwa nyuma kwenye kama mwamba wa kitanda,yaani unaukigeukia huo mwamba unashuka chini na kupanda. Mikono tu na visigino ndio vinakuwa vimeubeba mwili. Hayo mazoezi nimeanza nayo miaka 20 iliyopita. Sasa kilichokuwa kinanitokea kila nikikomaa mayo sana ilikuwa napata bawasiri, yaani kama vidude vinatokea sehemu ya haja kubwa,kama tuvidole tudogo hivi. Wakati wa haja,nikimaliza ile mishipa ya ndani inauma. Ikawa hiyo inakuja na kupotea nikawa naendelea na mazoezi huku nikitafuta tiba. Nimehangaika sana na tiba. Hivi ninavyoongea nimeacha mazoezi kabisa,kwa sababu sasa nikifanya tu kidogo napata maumivu makali balaa. Bado nahangaikia tiba,tiba ni adimu sana. Inaniuma sana nikikumbuka mazoezi,natamani mno

Sent using Jamii Forums mobile app
pole sana kaka
jitahidi kula maembe, nanasi na matunda mengineyo yenye nyuzinyuzi.
pia jitahidi kunywa maji na juice marakwamara na baada ya kila mlo.
punguza vyakula vigumu kama ugali na makande.
nasisitiza maji na matunda
 
Sio kweli mkuu. Samahani kukubishia lakini. Mimi kwa siku nakunywa maji si chini ya lita 3 kwa siku. Maximum lita 4 kila siku mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila samahani Mkuu! Mm nishawahi kuugua hivyo nikagoogle ndo nikaona maji yanasaidia kweli mm sina tabia ya kunywa maji mengi ila nilipoanza kunywa ilipotea tu ghafla nikapona ikawa historia ila kuna ndugu yangu yeye naye ilimpata ilikuwa serious sana akafanyiwa mpaka operation ndo akapona na haikujirudia tena! Sasa itabidi tushirikiane kuipata dawa ngoja niendelee kuuliza watu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Asante sana mkuu kwa wema wako. Hivi nafikiria kesho niwaone doctor's wataalam wa upasuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkuu kwa wema wako. Hivi nafikiria kesho niwaone doctor's wataalam wa upasuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app

Waone Mkuu halafu operation yake haiko complicated sana ni wanakikata tu hako kanyama halafu wanakupa na dawa za maumivu basi baada ya siku mbili tatu unapona

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Waone Mkuu halafu operation yake haiko complicated sana ni wanakikata tu hako kanyama halafu wanakupa na dawa za maumivu basi baada ya siku mbili tatu unapona

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kweli eeeh...! Kama mara mbili nimetoroka hosp. Mwezi wa 9 mwaka jana doctor mmoja baada ya kuniona akasema tena kwa mkazo,bro subiri oparation,nikamwacha anandaa vifaa. Kingine kilichofanya nitie mpira kwapani,tuko pale akasema hii ni mara ya anakuja. Anafanyiwa vinarudi baada ya miaka mi3. Mimi nafikiri bado hawajagundulia dawa sawa sawa. Huu ugonjwa nafikiri unakuwa umejijenga ndani tumboni. Wanatoa vya nje bila kutoa tiba kuua vimelea vyote vya ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waone Mkuu halafu operation yake haiko complicated sana ni wanakikata tu hako kanyama halafu wanakupa na dawa za maumivu basi baada ya siku mbili tatu unapona

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kweli eeeh...! Kama mara mbili nimetoroka hosp. Mwezi wa 9 mwaka jana doctor mmoja baada ya kuniona akasema tena kwa mkazo,bro subiri oparation,nikamwacha anandaa vifaa. Kingine kilichofanya nitie mpira kwapani,tuko pale akaja jamaa mmoja anasema hii ni mara ya 3 anakuja. Anafanyiwa vinarudi baada ya mwaka au miaka mi3 au mi3. Mimi nafikiri bado hawajagundulia dawa sawa sawa. Huu ugonjwa nafikiri unakuwa umejijenga ndani tumboni. Wanatoa vya nje bila kutoa tiba kuua vimelea vyote vya ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua napiga push up za kawaida napiga 50 lakini niakona kazi bure,
Maana kuna jamaa alinipa demo nipige push up 10 za kibana mikono (mikono unaikutanisha unatengeneza kopa) nilipiga nne tu nikashindwa kuendelea maana ukibana mikoni unakosa balance kurudi ukishuka.
Nikaona hizi ndio zenyewe ukipiga kumi tu zinatosha
Sasa kila siku nikitaka kuoga nazipiga 25(hapa nimekubuhu ndo maana napiga nyingi ivi) saivi kifua kimekua kama The Rock.
 
Tupia picha mkuu
 
Mkuu dawa ya bawasiri ni kunywa maji mengi ukiwa una tabia ya kunywa maji mengi huwezi kupata bawasiri

Sent from my iPhone using JamiiForums
Maji + Matunda + Mboga Mboga kwa wingi
Kawaida Bawasili ni tokeo la kutomeng'enywa chakula vizuri hivyo ku force mishipa iliyopo karibu na kinyeo kufanya kazi ya ziada kusukuma haja kubwa hatimae kupasuka kwa hiyo mishipa/veins

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka December 2018 nilikuwa napiga 10 nikajipa nikianza January 2019 nitakuwa kila mwezi naongezi 5 yaani mpaka December 2019 napiga 70
Hii sasa March nilitakiwa niwe napiga 25 lakini napiga 35 non stop
All in all mazoezi ni kama chakula ukizoea cha aina moja tu you get bored. Nimejaribu Kuruka Kamba 100 lakini nimeona pumzi inabana sana nashindwa kuendelea na Push Ups
Nimeamua kwanza mpaka nifike 50 ndio niongeze na kamba. Actually Kamba ndio lilikuwa zoezi langu hapo zamani nilikuwa napiga Kamba mpaka 350-400 na zilikuwa zile kamba nzito kabisa sijui nini hasa kimetokea nikiruka 100 tu nahema utafikiri nimerun 50kms
Nikienda Gym kabla ya kushiriki zoezi lolote kwanza huwa najiwekea malengo ya kukimbia kwanza 30 minutes non stop na hii yaweza nichukua miezi 2. Hapo hapo Gym unakuta mtu ana attend zaidi ya mwaka 1 lakini kukimbia 15 minutes hawezi, na akikuona unakimbia 30-40 minutes non stop anashangaa
Nikiweza ruka kamba 250 na kufanya quality push ups 50 zinanitosha saana
Maji + Matunda + Mboga Mboga muhimu saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpk sasa ssijamuona GUAM Ktk huu Uzi!
 
Wakuu mie huwa napiga 70, kwa mkupuo, kisha naanza kushuka hadi 20. Nimeanza kupiga toka 2003.
Ila kuna kipindi niliacha km miez sita, nilipokuja kuanza kupiga push up. Sikuweza kufikisha 70 kwa mara moja.
Ila nimekomaa hadi nimeanza kuweza.

Tatizo uzito umeongezeka toka 82kg hadi 89.
Na urefu wangu ni cm 178. Kimsingi huwa napiga zoez ili kilo.zipungue. kwan nataka niwe na 75-80. Ila shida, navyozidi kupiga push up uzito unaongeza sana. Na bado najitahidi niwe nakula sana mchana tu, asubuhi sili, usiku ni matunda tu au karanga.

Je nifanye ili uzito upungue na usiathiri routine yangu?

Kaka hakuna kitu kibaya kama ku skip Breakfast au kula kidogo
Muulize mtaalamu yoyote duniani wa mambo ya health and nutrition atakwambia kuna kanuni kubwa 1 ya kupangilia quantity ya chakula nayo ni "Take your breakfast like a KING, take your lunch like a PRINCE and take your dinner like a BEGGAR" Ingawa ni kinyume cha uhalisia wetu wabongo lakini ndio kanuni nayo ni hivi
1. Asubuhi inabidi tule chakula kingi kama vile tufanyavyo kwenye Lunch. Hapa ikiwezekana ugali na ndondo uliwe

2. Mchana inabidi tupunguze iwe kama mazoea yetu yalivyo kwenye Breakfast. Hapa kikombe cha Chai na Bites kidogo sio mbaya.

3. Wataalamu wanasema hapa bilauri ya maziwa au vipande kadhaa vya matunda au Salad vinatosha.

Kiakili ya kawaida ukichunguza sana inakubalika. Ikumbukwe energy kubwa mwili + akili hutumika kati ya saa 1 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi hivyo chakula chote kinachotumiwa wakati huo humeng'enywa vizuri muda huo. Kuanzia saa 6 kuendelea kazi huanza kupungua mwili hauitaji energy nyingi na mida hii ukila chakula kingi kama tunavyofanya unaanza kusikia mwili umechoka kausingizi kanaita, lakini kama utapiga kakombe ka chai na bites ule mzigo wa asubuhi unaendelea kumeng'enywa vizuri na mwili bado unaendelea kuwa mwepesi.

Tatizo zaidi linakuja kwenye dinner kwa sababu mida hiyo ndio tunakuwa home, na wapenzi wetu ndio wanapata nafasi ya kutupikia tukipendacho, na inawezekana kabisa milo mingine tuka skip lakini sio dinner maana kesi yake kwenye ndoa inabidi ipelekwe The Hague. Hapa ndio tunapofakamia chakula kingi na mafuta mengi ambacho hakitumiki kabisa kwa sababu baada ya muda huenda kulala. Na si aghlabu ukakuta tunatumia chakula kama appetizer ya usingizi. Inatakiwa gap ya dinner na kulala isiwe chini ya masaa manne ikipungua hapo chakula choote (hasa wanga na protein) hushindwa kumeng'enywa na hupelekwa ktk group la cholesterol au unconverted fats. Hizi unconverted fats ndio hii hujitokeza kama vitambi, makalio makubwa, na manyama uzembe ya mbavuni
Hizi unconverted fats ndio sababu kubwa ya Kisukari, Pressure, Cancer na Figo kuathirika

Hivyo ndugu usipunguze au kuruka Breakfast bali ongeza na punguza hiyo milo mingine

Wakati unakula kumbuka portion 4 za tumbo lako 1/2 chakula + 1/4 maji + 1/4 emptiness au hewa

Kumbuka mboga mboga na matunda kwenye mlo wako navyo ni muhimu

Vile vile usisahau tunakula ili tuishi, hatuli ili tufurahi au turidhike(to enjoy). Na ndio maana vyakula vingi ambavyo vinaupa mwili nguvu, nuru na uhai ladha yake mdomoni imekuwa sio maridhawa sana mdomoni ukilinganisha na mapocho pocho na mahanjumati yanayoharibu miili yetu

Wakatabahu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom