Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Kwa wale wapenda mazoezi ya 'Push up' tukutane hapa!

Wakuu mie huwa napiga 70, kwa mkupuo, kisha naanza kushuka hadi 20. Nimeanza kupiga toka 2003.
Ila kuna kipindi niliacha km miez sita, nilipokuja kuanza kupiga push up. Sikuweza kufikisha 70 kwa mara moja.
Ila nimekomaa hadi nimeanza kuweza.

Tatizo uzito umeongezeka toka 82kg hadi 89.
Na urefu wangu ni cm 178. Kimsingi huwa napiga zoez ili kilo.zipungue. kwan nataka niwe na 75-80. Ila shida, navyozidi kupiga push up uzito unaongeza sana. Na bado najitahidi niwe nakula sana mchana tu, asubuhi sili, usiku ni matunda tu au karanga.

Je nifanye ili uzito upungue na usiathiri routine yangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribu pia zoezi la kukimbia.Linakata sana uzito.Nilikuwa nina kg 92 ila ndani ya miezi sita ya kufanya jogging nikarudi kg 82.
 
soda ya kopo zikoje hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
unashika ile sehem ya kuvalia saa, then mkono mwingine unakuja ngumi....unaanza zoez la push ups, then baaada ya muda una switch mikono
 
dah ila ngumi itajaa masugu,vp tricep na bicep linajenga hilo zoezi la soda,maana pushup za ngumi sipigagi

Sent using Jamii Forums mobile app
weka two knuckles, ukiweka mkono mzima si unachafua mkono. hiz ishu wafanye wanaoanza
 
Wanasemaga et jinsi unavyopiga ndio unazid kuzoe mmmh
Mi nina mwezi sasa nilianza kupga 10-15 nikapanda 15-25 nimepanda saivi kwa mpgo mmoja bapiga 30 then namalzia 20 hoi vibaya yaniii hivi ntazoea kweli niwe siumiii hivi maana duuu mtihani huu
 
Kaka hakuna kitu kibaya kama ku skip Breakfast au kula kidogo
Muulize mtaalamu yoyote duniani wa mambo ya health and nutrition atakwambia kuna kanuni kubwa 1 ya kupangilia quantity ya chakula nayo ni "Take your breakfast like a KING, take your lunch like a PRINCE and take your dinner like a BEGGAR" Ingawa ni kinyume cha uhalisia wetu wabongo lakini ndio kanuni nayo ni hivi
1. Asubuhi inabidi tule chakula kingi kama vile tufanyavyo kwenye Lunch. Hapa ikiwezekana ugali na ndondo uliwe

2. Mchana inabidi tupunguze iwe kama mazoea yetu yalivyo kwenye Breakfast. Hapa kikombe cha Chai na Bites kidogo sio mbaya.

3. Wataalamu wanasema hapa bilauri ya maziwa au vipande kadhaa vya matunda au Salad vinatosha.

Kiakili ya kawaida ukichunguza sana inakubalika. Ikumbukwe energy kubwa mwili + akili hutumika kati ya saa 1 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi hivyo chakula chote kinachotumiwa wakati huo humeng'enywa vizuri muda huo. Kuanzia saa 6 kuendelea kazi huanza kupungua mwili hauitaji energy nyingi na mida hii ukila chakula kingi kama tunavyofanya unaanza kusikia mwili umechoka kausingizi kanaita, lakini kama utapiga kakombe ka chai na bites ule mzigo wa asubuhi unaendelea kumeng'enywa vizuri na mwili bado unaendelea kuwa mwepesi.

Tatizo zaidi linakuja kwenye dinner kwa sababu mida hiyo ndio tunakuwa home, na wapenzi wetu ndio wanapata nafasi ya kutupikia tukipendacho, na inawezekana kabisa milo mingine tuka skip lakini sio dinner maana kesi yake kwenye ndoa inabidi ipelekwe The Hague. Hapa ndio tunapofakamia chakula kingi na mafuta mengi ambacho hakitumiki kabisa kwa sababu baada ya muda huenda kulala. Na si aghlabu ukakuta tunatumia chakula kama appetizer ya usingizi. Inatakiwa gap ya dinner na kulala isiwe chini ya masaa manne ikipungua hapo chakula choote (hasa wanga na protein) hushindwa kumeng'enywa na hupelekwa ktk group la cholesterol au unconverted fats. Hizi unconverted fats ndio hii hujitokeza kama vitambi, makalio makubwa, na manyama uzembe ya mbavuni
Hizi unconverted fats ndio sababu kubwa ya Kisukari, Pressure, Cancer na Figo kuathirika

Hivyo ndugu usipunguze au kuruka Breakfast bali ongeza na punguza hiyo milo mingine

Wakati unakula kumbuka portion 4 za tumbo lako 1/2 chakula + 1/4 maji + 1/4 emptiness au hewa

Kumbuka mboga mboga na matunda kwenye mlo wako navyo ni muhimu

Vile vile usisahau tunakula ili tuishi, hatuli ili tufurahi au turidhike(to enjoy). Na ndio maana vyakula vingi ambavyo vinaupa mwili nguvu, nuru na uhai ladha yake mdomoni imekuwa sio maridhawa sana mdomoni ukilinganisha na mapocho pocho na mahanjumati yanayoharibu miili yetu

Wakatabahu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umenipa shule kubwa sana, nafurahi kukutakana jamvini na watu makini kiasi hiki.
Nimeanza kunywa chai, japo bado sifunguki km mchana. Pia njaa inaanza kuniuma kuanzia saa 4-5 hivi, lkn napambana hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom