Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Wewe hutojibiwa maana hakika mzizima huifahamu na wala hujui nini maana ya maeneo ya pwani au watu wa pwani
Sitojibiwa na nani sasa? Una uhakika gani mimi siijuhi Mzizima?
 
Sitojibiwa na nani sasa? Una uhakika gani mimi siijuhi Mzizima?
Wanaoijua mzizimahawawezi kuandika "siijuhi"wakikusudia siijui ,wanaoijua mzizima hawawezi kumnasibisha mkazi yeyote wa pwani kuwa wakuja!
Hitimisho-huijui mzizima period!
 
Wanaoijua mzizimz hawawezi kuandika "siijuhi"wakikusudia siijui ,wanaoijua mzizima hawawezi kumnasibisha mkazi yeyote wa pwani kuwa wakuja!
Hitimisho-huijui mzizima period!
Sawa wakuja, mkishafika Mjini kuuza kahawa na kukaa vijiweni basi moja kwa moja unajiona wa Mzizima,
 
Sawa wakuja, mkishafika Mjini kuuza kahawa na kukaa vijiweni basi moja kwa moja unajiona wa Mzizima,
Mkuu sio mimi tu hadi babu yangu ni wa mzizima na ndio watu waliomshika mkono J.Nyerere na kumtembeza mjini na hata alipikufa marais wote wa nchi hii walihudhuria msiba wake mwenyekiti- wa wazee mkoa wa dar unanisoma? Sasa tafuta wenyeviti wote marhum mmoja babu yangu na kwa taarifa tu katika hotuba za jk nyerere pale anaposema alipelekwa zanzibar bagamoyo babu yangu alikuwepo katika msafara na watu wa mwanzo kuacha utumishi wa mkoloni ili kudai uhuru babu yangu alikuwepo !
 

Hata mimi Babu yangu alishiriki sana harakati za uhuru hapa Dar es salaaam, japo hakuwa Mzaramo, Mndengereko au Mmanyema

Kuna kitu huwa mnakosea sana, Mtu kama Kunambi, Rupia, Pombeah, Cecil Matola, Kyaruzi ect hawakuwa wazawa wa Dar, lakini huwezi kusema ni wa kuja huku ukifanya watu kama Fundikira (Tabora) Sykes family (Zululand) na wengine wanaofanana na hao kuwa sio wakuja,
 
Sina cha kukupinga hapo na ukweli utabaki kuwa hao uliwataja ni wakuja walioshirikiana na wajanja wao ila vizazi vyao vilivofuata si wakuja ! Hoja ya hapa ni hawa wakuja sasa ambao hawaijui hata kwa kuhadithiwa hii darul salaam!
 
Kumbe Mkisi alikuwa mkuu wa shule, mimi alikuwa alikuwa afande wangu JKT
 
Nakumbuka manzese kabla ya daraja kulikuwepo msufi almaarufu manzese msufini. Maeneo ya posta mpya opposition kulikuwepo jumba LA empire cinema,ah mambo mengi sana
 
124
Mjomba umekumbuka Biriani la Shesh Mahal hii ilikuwa karibu ya Hindu Mandal Hosp. Kaka Jumbe Cap (Baharia wa zamani) kuna wakati alikuwa maneja hapo.
 
Wanaoijua mzizimahawawezi kuandika "siijuhi"wakikusudia siijui ,wanaoijua mzizima hawawezi kumnasibisha mkazi yeyote wa pwani kuwa wakuja!
Hitimisho-huijui mzizima period!
Tawile tawile tawile...
 
Snow cream ndiyo hii iliyopo karibia na ofisi za Chanel 10 ?
 
Yaap kwa Mzee kassim baba Mariam. Kwa marehemu mzee Kenge kwenye kachori na bajia ahahha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…