Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

bwana mdogo kumbe umesoma juzi enzi ya martin mkisi,haya nw yupo meja kessy!
 
Hiyo View ya left side ukiipata muonekano ndio unakuwa kama huo kwenye picha ya kale
Mkuu upo Dar? Kama upo Dar pita hilo eneo mchana wa kesho piga picha kisha ilete hapa hiyo view ya kutokea mnara wa saa kulia mwa picha hayo majengo ni tofauti na picha ya kale.
Hebu tazama hii picha nyingine ya jana



Angalia mpaka nguzo za umeme bado ni zilezile za kale [emoji15] [emoji15]
 
Hapa 1960's na VW na Morris zinazuguuka sanamu ya Bismini & Haji brother ilikuwa maarufu kwa kuuza saa za mkononi siku hizi hilo duka kuna Benki ya Posta.
jengo hilo linabomolewa hivi sasa tunavyookomenti humu, buriani kwake
 
Hapa 1960's na VW na Morris zinazuguuka sanamu ya Bismini & Haji brother ilikuwa maarufu kwa kuuza saa za mkononi siku hizi hilo duka kuna Benki ya Posta.
Hapo Hsjji Brothers kwa sasa panavunjwa kunapangwa kujengwa ghorofa moja matata sana litakaloitwa Gumzo la Jiji. Subira yavuta kheri.
 
ndio tunaambiwaga zamani dili lilikuwa kwenda ulaya na wazee wetu, kumbe kweli
 

Duh ZZ naona stori za 60s na 70s zimemvuta kaka Mtebetini.Mzizi Mkavu Ubarikiwe Mkuu
Miaka ya 70s nilikuwa nakuja Dar Toka Dom
Na reli,mabasi ya Kamata Na mabasi ya railways wakati huo Shaban Robert secondary ilikuwa secondary kweli
 
aisee kuna taa naiona kunbe imekula chumvi nyingi
 
hasaa
 
Wakuu Mtebetini,FaizaFoxy,Mzizi mkavu na wakongwe wengine, kati ya mwaka 1967 hadi 1968 nikiwa na babayangu mkubwa tulipita sehemu fulani tukaona samaki (perege) wapo chini yaani kuna bwawa chini ya ardhi , ila mdomo wa hilo bwawa ni kadri ya kipimo cha mita moja kwa mita moja. Hilo bwawa ni la simenti yaani zege kwa juu, tafadhalini nikumbusheni ni wapi palikuwa? Ni mnazi mmoja au wapi?
 

Hapo ndiyo pale sasa wanafanya sherehe za mashujaa, opposite na Cooperative Building, Kidongo Chekundu. Maarufu "Garden".
 
Hongereni sana kumbe tumetoka mbali eeeh lakini mbona kama tunarudi nyuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…