Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Nakumbuka mwaka 1971 nilikuwa chuo cha watumishi wa serekali pale magogoni. Niliishi hostel pale kituo kinaitwa akiba. Basi la chuo likitoka kurasini branch ya secretarial course( sasa chuo cha uhasibu) linatupitia nakutuchukua kwenda chuoni magogoni wakati huo mkuu wa Chuo mzee Lukanga mzee wa kibondei. Karibu nyuma kidogo ya hostel kuelekea Upanga kulikuwa na vijumba vya dada poa toka mkoa maarufu kwa dada wa kazi hiyo enzi hizo. Mitaa ya jiji ilikuwa anafagiliwa kuanzia saa nne usiku barabara zikiwa na magari machache mno. Ilala, Magomeni, Temeke quarters nyumba zilikuwa zimepangika na barabara safi za lami. Watu hawakuwwa zaidi ya milioni katika jiji.
 
Mji ukikua msafi ulipokua chini ya wavaa vikofia...[emoji16][emoji33]
 
Mie sina la kusema, nimezaliwa 1980, hapahapa dar. Nikaenda kijijini na bibi yangu mzaa baba, nimekujarudi dar, 1998. Kwa hiyo sikumbuki chochote ila nawashukuruni sana kwa kutupa historia ya dar es salaam.
 
SAA NYINGNE NAOMBA TUWE NA AKILI SASA SISIS TUNAJADILI MAMBO YA MAENDELEO MTU MWINGNE ANALETA HOJA ZA NYUMBA MIAKA HIYO ATA SIJAZALIWA ZINATUSAIDIA NINI...JADILINI MAMBO YA MAENDELEO NA SIYO KUDUMAZA AKILI ZENU..MAMBO MEMA KAMA KUMSIFIA MH.RAIS KUNUNUA NDEGE MPYA ,KUJENGA RELI,ELIM BURE,MIKOPO VYUONI,KUPGA VITA RUSHWA NA MENGINE LAKINI SIYO KUJADILI MAMBO YA KIJINGA KAMA HAYA
 
Duh...Mkuu, mbona unafoka kama maziwa jikoni yaliyokosa mwangalizi?
Historia ni zana nzuri na muhimu kwa maendeleo. Kama hujui ulikotoka utajuaje uendako? Fikiri..!
 
Nani alikudanganya Mwinyi na Kikwete wakuja?

Mwinyi kwao Mkuranga, Kikwete kwao Bwagamoyo, yote hiyo pamoja na Dar ilikuwa ni Coast Region enzi hizo.
Mwinyi kwao ni bumbwini unguja sio mkuranga
 
Ataje orodha ya Pan ndio utamjua. Kuna wachezaji panga pangua watakuwemo katika list. GM, CK, RM, SMC, KM, KM, SM, IK, JPM, MRA, PT, MM na wengineo.

Kwa faida ya wadau nimeona niyatoe majina kwa ukamilifu.

GM - Gordian Mapango
CK - Charles Kilinda
RM - Roma Mapunda
SMC - Salum Mwinyimkuu Carlos
JM - Jella Mtagwa
KM - Kitwana Manara (Popat)
KM - Kassim Manara
SM - Sunday Manara (Kompyuta)
IK - Ibrahim Kiswabi
JPM - Juma Pondamali Mensah
MRA -Mohammed Rishard Adolf
PT - Peter Tino
MM - Mohamed Mkweche

Kama nimesahau wengine naomba mwongezee.
 
Umekosea sana tena.

Hapo ni Kichwele kweli kwa sasa ni mtaa wa Uhuru.

Kichwele haijawahi kuitwa Indira Ghandi, Indira Ghandi ni India Street.

Hiyo mitaa yetu na si Nkurumah hapo.
Indira gandi zamani iliitwa Market Street lilikuwepo Soko na hilo Soko likaondoshwa likajengwa Jengo Bank ya NBC ikahamia hapo ikaitwa Kichwele Branch umaarufu wa Soko ukawa unapotea na Jina la Kichwele likashika kasi hadi Miaka ya 80s katikati Gari aina ya Range Rover ilikuwa ni marufuku kupaki eneo la Bank. Hivyo We mama Jitambulie Mitaa yako ya Kariakoo Street na Lumumba ndio uijuayo la sivyo ukiijua yote basi ulikuwa pashkuna.
Mtaa wa India nao Upo umeanzia Clock Tower hadi Round About ya Jerry Slaa aliyoremba vikaragosi vya madebe na vyuma. Mtaa huo ukiwa unaupita utaweza kufika Msikiti wa Ngazija,Hospital ya Hindu Mandal Usichanganye Mtaa wa India na Indira Ghandi.

Yaweza kuwa sehemu zinafanana haswa maana Nkurumah ni same japo kiasi hicho kijumba pembeni ya ile Picha kilinistua kulikoni nyumba chafu ya kiswahili kuonekana mtaa wa Nkurumah! ila kuna kamfanano.
 
Mkuu mimi sio wa kuchemsha kuijua Dar-es-salaam,kwanza kichwele hupajui hebu kaulize tena kwa aliyekutajia hilo jina,kichwele ipo wapi? Pili hii picha ya 404 peugeot hapo siyo Nkurumah,hapo ni mtaa wa uhuru kona na Nyamwezi hiyo petrol station na jengo linalofatia kushoto bado yapo mpaka leo,upande wa kulia hiyo nyumba ndogo imevunjwa kuna Bank M, ukiangalia mbele unaona kuna Basi linatoka mnazi mmoja la kampuni ya DMT sina hakika kama uliwahi kupanda, basi lipo kona ya mtaa wa swahili na hilo ghorofa la kona ya swahili kulia bado lipo na kuna kituo cha taxi.
Mkuu Dar-es-salaam ya wakati huo na viunga vyake vipo kichwani mwangu picha haijafutika. Nakupa changa moto pita Nkurumah na mtaa uhuru utajifunza kuangalia picha.Hiyo picha imepigwa kona ya mtaa Nyamwezi kuangalia mnazi mmoja.
Hayo ya wizi sii kweli kulikuwa hakuna ujinga huo,wote tulikuwa tunajuwana utamwibia nani?
Kariakoo ilikuwa eneo la waungwana wa mji huu.
Mkuu sina haja ya kumuuliza mtu sababu nimeishi huko. So Jina la Kichwele kwa mara yangu ya Kwanza kulisikia ni pale ilipokuwa Bank ya NBC Indira Gandhi Street na Umaarufu wa Huo Mtaa ulioitwa Market ulifutwa na kupewa Jina la Wziri Mkuu wa India Alipoitembelea Tanzania. Sasa hivi hiyo Bank ya NBC ilihamisha tawi lake hapo na na kulipeleka Mtaa wa Jamhuri na Wameondoka na Jina lao la Kichwele.

Actuary huyo kichwele sielewi ni Mtu au kiumba gani.

Hayo Maeneo mimi kwangu yapo kichwani na jinsi nilivyosema ndio kichwani picha ipo hivyo eneo hilo Nenda pale Mnara wa Saa ingia Nkurumah Ukaribie National Tyre utaelewa. But picha yako muelekeo wake ni kutoka msimbazi kuelekea Mnazi mmoja ndio Sababu yangu kufananisha haswa. Any way Hongera umenipata kwa Hilo.
 
Mkuu nimekuelewa ulichosema ila kuuliza si ujinga kaulize kwa wanaoijua Dar watakwambia kichwele ni wapi.
Kuhusu picha ya Nkurumah na uhuru hebu angalia hizi picha nimezipiga leo na simu yangu ya kitochi kisha utaelewa nilichokielezea toka day one kuhusu ile picha

68197afb6aa42f70ca2a22610c3d0fdc.jpg

picha ya tarehe 27/02/2017 mtaa wa Uhuru[emoji115]
640c6fc22ba9ce7e727a9a5d0ef1211d.jpg

picha ya zamani[emoji115]
5f749b2f4f4371cb74cee86dea0c47b0.jpg

picha ya 2017 Chox[emoji115]
 
Mkuu nimekuelewa ulichosema ila kuuliza si ujinga kaulize kwa
5f749b2f4f4371cb74cee86dea0c47b0.jpg

picha ya 2017 Chox[emoji115]
Mkuu Hii Picha kaipige ukiwa unatokea Mnara wa Saa kijengo cha National Tyre kionekane na hiyo Petrol Station ikiwa inachungulia.

Total Ndie Mkongwe aliyebakia katika Makampuni ya Mafuta.

Shell ilipotea,ESSO,Agip,Cartex na BP nayo ikasepa Kabakia Total pekee.
 
Mkuu Hii Picha kaipige ukiwa unatokea Mnara wa Saa kijengo cha National Tyre kionekane na hiyo Petrol Station ikiwa inachungulia.

Total Ndie Mkongwe aliyebakia katika Makampuni ya Mafuta.

Shell ilipotea,ESSO,Agip,Cartex na BP nayo ikasepa Kabakia Total pekee
Mkuu ukipiga kutokea mnara wa saa linaonekana jengo la chox kulia kwako hapo ndiyo kwenye tofauti.
 
Hayo Mabasi sikuyapanda ila Uda na Kamata Niliyapanda. Nilisikia kulikuwa na Bus la Gholofa liendalo Ilala kutokea Nadhani Mnazi.

But pale UDSM kulikuwa na Bus moja la Gholofa pia japo sikuliona likitembea
 
Mkuu ukipiga kutokea mnara wa saa linaonekana jengo la chox kulia kwako hapo ndiyo kwenye tofauti.
Hiyo View ya left side ukiipata muonekano ndio unakuwa kama huo kwenye picha ya kale
 
Back
Top Bottom