Kwa wale wote wafanyabiashara ya mazao njooni Mpanda kapanga (Mwese)

Kwa wale wote wafanyabiashara ya mazao njooni Mpanda kapanga (Mwese)

Wakuu Sina muda wa kuandika thread ndefu sana.

Lakini kwa ufupi sana kama wewe ni mfanya biashara wa mazao especially mahindi na mpunga njoo Mpanda -kapanga kama unaenda mwese.

Mahindi yanauzwa kwa bei ya 45-50k gunia. Ukikusanya mwenyewe kwa watu ni 30k kwa gunia maeneo ambayo utaweza kuyapata kwa wingi ni
Kasunga
Kasilipu
Manyoni
Kapanga
Katende (hapa mchele ni 1300 kg1)
Na vijiji vyote.

Kama uko seriously Fanya hivyo mahindi yapo kwa wingi mno mno.

Hapo kapanga ndo senta kubwa Kuna semi 🚛 na fuso nyingi mno mno zinasomba mazao usiku na mchana.

NB: WAKUU SITATOA NO MTONYO NILIO WATONYA UNATOSHA SANA.

Picha zina load sana nimefuta mtandao upo wa shida mno huku.(Vodacom)
Ubarikiwe Sana, na Mungu akubariki, vijana wa JF tupewe ni zaidi?
 
Hizi bei za nafaka zitaendelea kushuka mpaka August.
Kuna maeneo gunia la mahindi linauzwa Tsh 35000 na kilo ya mchele super itashuka hadi Tsh 1000 make wakulima bado wanavuna.

Wenye mitaji mikubwa changamkieni mwaka huu ni mwendo wa kupiga mbesa!
Usisahu wese limepanda pia, usafirishaji ni gharama kubwa
 
Usisahu wese limepanda pia, usafirishaji ni gharama kubwa
Ndo maana nawashauri wasikurupuke kwenda kuchukulia mzigo mikoa ya mbali.
Nafaka kama mchele na mahindi hata mkoa wa Morogoro utapata kwa wingi tu na bei ni sawa na ya huko mpanda. So why uhangaike kwenda mbali?
 
Moro Mchele haujawahi kiwanja bei nafuu huu mkoa Una shida
 
Moro Mchele haujawahi kiwanja bei nafuu huu mkoa Una shida
Sio kwa mwaka huu mkuu. Mpanga ni mwingi sana.
Nimetoka juzi Turiani. Mchele mashineni ni sh 1500 super na bado wakulima wanavuna. Shamba ngunia la debe 8.5 sh 60k super. So why uende Mpanda au Malinyi huko mbali na mbali.
Mahindi huko kilindi na kiteto yatakosa wanunuzi coz ni mengi na ndo kwanza wanaanza kuvuna.
 
Pamoja mkuu. Na maharage nilisahau kuongezwa hapo debe Lina 25k tu
Natarajia kupata pesa mwezi July Kati Kati sijui kama Msimu utanisuburj
Sio kwa mwaka huu mkuu. Mpanga ni mwingi sana.
Nimetoka juzi Turiani. Mchele mashineni ni sh 1500 super na bado wakulima wanavuna. Shamba ngunia la debe 8.5 sh 60k super. So why uende Mpanda au Malinyi huko mbali na mbali.
Mahindi huko kilindi na kiteto yatakosa wanunuzi coz ni mengi na ndo kwanza wanaanza kuvuna.
Huu mwaka Mvua ilinyesha vizuri Nchi nzima
 
Vipi kwa Mkoa wa Songwe ,nimekaa hapo Mlowo ,kuna biashara kubwa Sana ya Nafaka hasa Mchele na Mahindi sijui kwa sasa hali iko vipi ?
 
Panafikika kwa gari dogo kutokea Mpanda mjini kwa kiangazi?
 
Back
Top Bottom