Nakumbuka kauli alioitoa Edward Lowasa mwaka 1994 nikuwa chuo cha ualimu Monduli akimtetea mkuu wa chuo wakati huo (Def) Kuwa "if you are looking for the green pasture then you are in wrong way".Sakata lenyewe lilikuwa linahusiana na kula ugali mfululizo wakati fedha za kununulia mchele zikiwa zimefisadiwa.
Sasa hilo linadhihirika waalimu wakiwa wanataabika na familia zao,wanadharaulika na jamii ambayo wanatarajia watoto wao watafundishwa na walimu hao hao.
Na wasihi walimu wajiendeleze na fani zingine bila kusahau ujasiria mali ambao utawatoa kimaisha na waache kukopakopa ovyo kwenye vyombo vya fedha vya mafisadi kule unapokopa 1million na unalipa 4million.Na kule tunapoacha kadi za benki rehani.
Tuwasaidie watoto wa wakulima maana hao wanao tufanyia ufisadi watoto wao wanasoma shule za bei mbaya na pengine nje ya nchi,hivyo wanaweza wasiathirike na "FUKAMA" ikawa ni sawa na unajipiga na bastola kwenye mguu wako mwenyewe.
Tushirikiane kudai haki zetu kila moja kwa nafasi yake,wilayani ofisi za elimu ndo usiseme Mafisadi wa kutupwa,miungu watu,wana wahujumu walimu wenzao.