MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 886
Kutokana na Serikali kuwadharau Walimu, Kila mwalimu ajiunge na sera inayoitwa FUKAMA yani FUNDISHA KULINGANA NA MALIPO, mda unaobaki kafanye shughuli zako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana
Kutokana na Serikali kuwadharau Walimu, Kila mwalimu ajiunge na sera inayoitwa FUKAMA yani FUNDISHA KULINGANA NA MALIPO, mda unaobaki kafanye shughuli zako.
Ila kwa kweli mtu akiniita mwalimu aisee hata mie naona kanitusi kabisa aisee...maana hii professional kila mtu anaidharau sijui kwa nini.........
walimu wa kulazimishwa kutokana na shida zao lazima wakwepe kuitwa walimu lakini ukweli ni kuwa mtu wa kwanza anaeidharau fani hii ni mwalimu mwenyewe hebu ona wale mawaziri ambao ni walimu kwa asili badala ya kusaidia kuboresha ualimu ndio wameenda kuharibu kabisa pale wizarani!amua sasa kuwa mwalimu kamili utaona kama utadharaulika!
Mimi huwa naamini ukijitahidi kuwa mwalimu wa kweli ndio unavyojizidisha dharau...
sidhani kama utendaji bora hudhoofisha sifa kazini labda kama tunatofautiana kwenye matumizi ya neno dharau!
ni kweli serikali imeendelea kuwafukarisha walimu na wa tanzania kwa ujumla wake na hili linajenga dharau pana si kwa walimu tu bali Taifa kwa ujumla wake!dharau tunayoiongelea hapa ni ya kipato na umasikini wa waalimu...jamii na serikali yako imewafanya kuwa watu masikini sana na kipato kidogo....
ni kweli serikali imeendelea kuwafukarisha walimu na wa tanzania kwa ujumla wake na hili linajenga dharau pana si kwa walimu tu bali Taifa kwa ujumla wake!
Na taifa likidharaulika mwl ana nafasi kubwa ya kulitoa taifa hapo na kwa hilo walimu wanatakiwa kukazana nalo kupitia elimu waitoayo ili wazalishe wakombozi wa kweli na kwa kufanya hivyo dharau hiyo itatokomezwa!
huyo anatakiwa akauje madeni yake baclays,vinginevyo atafungwaNimekuta mwalimu amekopa NMB, Bayport, Faidika, Blue financial na Pletinum Credit. Take home yake ni 00. Salary slip yake nimechukua nikiweza nitaiscan niiweke hapa ila jina nitalifuta. Kweli ualimu ni bonge la chaka.