Ukitoka nyumbani?! Ushatoa 70k then ukitoka nyumbani unafanyaje? Majirani inategemea ndugu yangu. Halafu wanaolalamika ni wale wa bundle za 3000 zimekuwa 10,000/- sasa mtu kama huyu umwambie atoe 70k?
Nafikiri umuhumu, use case na bajeti zinakuwa tofauti kwa watu tofauti
Hii set up ndiyo ipo kwa watu wengi naona huku Marekani, na watu wanajaribu kuileta Tanzania. Na si lazima kila mtu aitumie, kwa sababu bajeti za watu zinatofautiana.Malengo ya watu ni tofauti. Wengine wanataka kuangalia internet mara moja kwa siku jioni wakiwa nyumbani, wengine wanataka kila dakika wawe na internet.
Hii setup kwa maelezo ya juu nilivyoielewa
1. Ukiwa nyumbani, unatumia hiyo internet ya waya iliyounganishwa nyumbani. Hata kwenye simu hutumii bando, kwa sababu utaweza kuunganisha wireless router na kutumia Wifi. Maana yake hiyo 70,000 kwa mwezi ita save sana bando lako ukiwa nyumbani. Haponm utadownload vitu vingi sana bila kuhofia bando. Youtube, movies etc.
Sasa 70,000, kwa mujibu wa bajeti za watu tofauti, na use cases, inaweza kuwa hela nyingi sana au kidogo sana.
2. Ukiwa njiani, huko utatumia bando la kampuni ya simu.
Kama unaweza ku afford hivyo na upo nyumbani at least kuanzia jioni utapata the most cost effective internet.
Kama hiyo setup ni gharama sana, unaweza ku afford kulipia internet mara moja tu, either ya simu au hii nyumbani, of course ya simu inakupa mobility zaidi, lakini inaweza kuwa na gharama zaidi per MB.