Ndoa haina formula unaweza ukaiga za wenzio kumbe ndo unajimaliza kabisa, ingia ndani ya basi hata kama limejaa hata pa kuweka mguu hakuna we ingia tu likianza kumove utapa pa kuweka mguu. Usiogope karibu kwenye chama.
habari za hapa wanajamii...?? nigependa nipate ushauri kwa walio ndani yandoa tu, maana mii natarajia kiungia ndani ya ndoa !.. hasa wale ambao ndoa zao zinaumri wa miaka 10 na zaidi. ni kitu gani kimewasaidia kudumisha ndoa zao...? na niyapi yakuzingatia ukiwa ndani ya ndoa..? nawakaribisheni sana...!!
pia nawakaribisha wanajamii wote tarehe 18-08-2012 walio zanzibar karibuni hata wolio nje ya hapa. nilie mpata kupitia jukwaa hili namvisha kizibiti wendo yani (pete) ya uchumba.
Umesema vizuri kuwa unatarajia kuingia kwenye ndoa.
Swali:- Umeshawahi kugombana na mwenzako huyo, na baadaye mkapatana kwa dhati (mkasameheana na uhusiano kuendelea)? Kama bado basi kuna mtihani hapo. Kwasababu inawezekana kabisa katika maisha yenu ya ndoa mkatofautiana, au kugombana, au kupingana katika jambo fulani. hapo kama kila mmoja hana 'uwezo' wa kusamehe na kusonga mbele basi hamna ndoa.
Muhimu:- Kila mmoja wenu anatakiwa kuwa tayari 'kushuka', au kujishusha mbele ya mwenzake. Yaani kukubali kushindwa kwenye jambo fulani ambalo halina muafaka kati yenu. maana kila mtu 'akipanda' na kujiona kuwa ana haki sana au kuwa anaonewa, basi hamna ndoa.
Hongera, ulimpata humu, so nice I hope ndoa yenu itadumu. Mungu awatangulie.
Uongo japo kidogo lazima usimwe ndani ya ndoa.
Ndoaaaaaa....... Ndoanaaaaaaaa....
pia nawakaribisha wanajamii wote tarehe 18-08-2012 walio zanzibar karibuni hata wolio nje ya hapa. nilie mpata kupitia jukwaa hili namvisha kizibiti wendo yani (pete) ya uchumba.
mtangulize Mungu kwa kila jambo katika ndoa yako