Umesema vizuri kuwa unatarajia kuingia kwenye ndoa.
Swali:- Umeshawahi kugombana na mwenzako huyo, na baadaye mkapatana kwa dhati (mkasameheana na uhusiano kuendelea)? Kama bado basi kuna mtihani hapo. Kwasababu inawezekana kabisa katika maisha yenu ya ndoa mkatofautiana, au kugombana, au kupingana katika jambo fulani. hapo kama kila mmoja hana 'uwezo' wa kusamehe na kusonga mbele basi hamna ndoa.
Muhimu:- Kila mmoja wenu anatakiwa kuwa tayari 'kushuka', au kujishusha mbele ya mwenzake. Yaani kukubali kushindwa kwenye jambo fulani ambalo halina muafaka kati yenu. maana kila mtu 'akipanda' na kujiona kuwa ana haki sana au kuwa anaonewa, basi hamna ndoa.