Salaam, Shalom.
Kwa mara ya kwanza, Nchi yetu ilipokea Rasmi Chanjo ya CORONA virus Kutoka nje aina ya Johnson Johnson mnamo July 24, 2021.
Hadi sasa imebaki miezi 4 kukamilisha miaka mitatu tangu kuingia Chanjo nchini na kuanza zoezi Hilo la Chanjo nchini.
Asilimia kubwa ya walipinga Chanjo hizo walidai kuwa,madhara ya Chanjo hizo yataanza kuonekana dhahiri baada ya miaka mitatu tangu kupata Chanjo hizo.
Ni ombi LANGU, Kwa wote mliopata Chanjo hizo, piteni hapa na Kutoa uzoefu wa MAISHA kabla ya Chanjo na maisha baada ya Chanjo ya CORONA.
Tusaidieni kujibu maswali yafuatayo;
1. Ulichanja Chanjo ya coronavirus?
2. Je, AFYA zenu na za ndugu zenu zimeimarika zaidi na kuepuka kuugua kama zamani kabla ya Kupata Chanjo?
3. Changamoto mlizozipata ndani ya muda wa Chanjo Kwa miaka hii karibia mitatu ni zipi?
4. Faida mlizopata baada ya kuchanja kiafya ni zipi kulinganisha na kabla ya kuchanja?
Karibuni 🙏