Kwa waliochanja Chanjo ya CORONA Njoni mtoe uzoefu Ili tupime ufanisi.

Kwa waliochanja Chanjo ya CORONA Njoni mtoe uzoefu Ili tupime ufanisi.

Kuna mmja alikuwa analalamika kuumwa umwa ila still yupo hai
 
Hayo yalikuwa ni maneno ya waswahili tu kama kawaida yao
Wape kichwa cha habari na wao watamaliza kila kitu
Nilichanja AstraZeneca chanjo 2 ila ya Tatu niliacha tu nikaona iliyowapitia imewapitia acha nitulie na hizo 2
Sina tatizo lolote na mwisho kwenda kupima kila kitu mpaka cancer na kisukari, pressure na tezi dume ni mwezi uliopita
Namshukuru Mungu hata kikohoo sina na ni mwaka wa 3 huu tangu chanjo
 
Japo ni kawaida.
Nakumbuka miaka ya nyuma kuna wahubiri wapingana na matumizi ya computer kuwa zinahusiana na mpinga Kristo lakini leo hakuna dhehebu ambalo hakuna muamini hata mmoja ambae haitumii hiyo computer au smartphone
Ujinga ni mzigo mzito sana, na wahubiri wengi wajinga huwa wana kelele kupitiliza.
 
Kwen
Una huo ushahidi wa rate ya Mtu 1 Kwa 1,000,000?

Ninakoishi case za kuganda Damu na kufariki tulizika watu wawili.

Wewe una data?
Kwenye industry ya medicine hiyo inatokea sana. Ndio maana watu wenye shida na sulphur wawashauriwi kutumia dawa za malaria zenye viambata vya sulphur na wengi ambao wazitumia bila kujua walipata shida.

Shida hii ilitumika kukosoa watumizi ya teknolojia hii bila kuwa na mashiko.
 
Hayo yalikuwa ni maneno ya waswahili tu kama kawaida yao
Wape kichwa cha habari na wao watamaliza kila kitu
Nilichanja AstraZeneca chanjo 2 ila ya Tatu niliacha tu nikaona iliyowapitia imewapitia acha nitulie na hizo 2
Sina tatizo lolote na mwisho kwenda kupima kila kitu mpaka cancer na kisukari, pressure na tezi dume ni mwezi uliopita
Namshukuru Mungu hata kikohoo sina na ni mwaka wa 3 huu tangu chanjo
1. Kama una miaka mitatu hata kikohozi huna, vumbi linaloingia mwilini kupitia pua na hewa linatokaje?

2 . Kwanini hukuchanja Chanjo ya 3?

Kwanini hukufuata maelekezo ya madaktari?

3. Tofauti Yako wewe uliyechanja na sie au nduguzo wasiochanja ni ipi?
 
Nilichanja, sikumbuki ni lini niliugua mafua zaidi ya hivi vimafua vya kutumia Viagra!!!

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
Kuna Viagra ya kutibu mafua?

Vumbi la hapa nchini, linaloingia Kila kukicha, unalitoaje ndani ya MWILI kama hukohoi na kupata mafua?
 
Una huo ushahidi wa rate ya Mtu 1 Kwa 1,000,000?

Ninakoishi case za kuganda Damu na kufariki tulizika watu wawili.

Wewe una data?
Kwanza elewa maana ya risk na unakoishi wangapi walichoma chanjo ya J&J?

Halafu zingekuwepo hizo kesi wapotoshaji wa chanjo si mngewapeleka hadi BBC, Aljazeera hadi CNN kuhakikisha hiyo habari inafika kila kona ya dunia.
 
Madhara hayawezi kuonekana mapema hivyo.

Hao J&J wana poda yao ya watoto imedumu sokoni miongo kadhaa hadi kugundulika ina sababisha saratani.
 
Kwen

Kwenye industry ya medicine hiyo inatokea sana. Ndio maana watu wenye shida na sulphur wawashauriwi kutumia dawa za malaria zenye viambata vya sulphur na wengi ambao wazitumia bila kujua walipata shida.

Shida hii ilitumika kukosoa watumizi ya teknolojia hii bila kuwa na mashiko.
Kuna kitu mnatuficha mliochanja,

Hakuna Chanjo yoyote utachanja isiwe na side effect,

Kwann hamsemi upande wa pili?
 
1. Kama una miaka mitatu hata kikohozi huna, vumbi linaloingia mwilini kupitia pua na hewa linatokaje?

2 . Kwanini hukuchanja Chanjo ya 3?

Kwanini hukufuata maelekezo ya madaktari?

3. Tofauti Yako wewe uliyechanja na sie au nduguzo wasiochanja ni ipi?
Kikohoo cha maambukizi au hali ya hewa au virus huwa haiepukiki mkuu
Chanjo zilikuwa ni kwa kila mtu hapa nilipo walikufa watu wengi sana na umri wangu ni over 60
Niliitwa kuchanja nikaenda ya kwanza na baada ya mda nikachanja ya pili

Baada ya hapo makali ya vifo ikapungua sana na wakaanza kuruhusu safari za nje na ndege zilipoanza tu nikaja Bongo ambapo hata mask ilikuwa ni hiyari nilifurahi sana kwa hilo

Chanzo ya kwanza na ya pili walihimiza sana na wakawa mpaka wanatuma msg ila ya Tatu iliingia na watu wakawa hawafi kama mwanzo
Tofauti ya mimi na wasiochanja hakuna kwani walisema zina madhara lakini sijadhurika kwani tunakula madawa ya kila aina kila leo na yenye side effects za kila aina mpaka zinazoharibu ini au Figo ila bado watu wanakula

Nafikiri nimejaribu kujibu ulichotaka kujua
 
Kwanza elewa maana ya risk na unakoishi wangapi walichoma chanjo ya J&J?

Halafu zingekuwepo hizo kesi wapotoshaji wa chanjo si mngewapeleka hadi BBC, Aljazeera hadi CNN kuhakikisha hiyo habari inafika kila kona ya dunia.
Unanibishia Mimi niliyezika majirani wawili Mahali tunakoishi waliokuwa wamechanja na Damu kuganda baada ya muda Fulani kufariki?

Tena mmoja kati ya waliofariki,alienda kuchanja Kwakuwa Eti Alimsikia mkt wake wa chama kachanja, naye akadhani ndo msimamo wa chama, naye Akaenda kudunga.

Tulimzika japo Kwa huzuni😪
 
Hongereni mliochanja, nilijisemea kama kufa ni sawa tu ila sichanji.
 
Back
Top Bottom