- Thread starter
- #81
Kwahiyo hukupata side effect yoyote baada ya kuchanja Hadi hivi Leo?Kikohoo cha maambukizi au hali ya hewa au virus huwa haiepukiki mkuu
Chanjo zilikuwa ni kwa kila mtu hapa nilipo walikufa watu wengi sana na umri wangu ni over 60
Niliitwa kuchanja nikaenda ya kwanza na baada ya mda nikachanja ya pili
Baada ya hapo makali ya vifo ikapungua sana na wakaanza kuruhusu safari za nje na ndege zilipoanza tu nikaja Bongo ambapo hata mask ilikuwa ni hiyari nilifurahi sana kwa hilo
Chanzo ya kwanza na ya pili walihimiza sana na wakawa mpaka wanatuma msg ila ya Tatu iliingia na watu wakawa hawafi kama mwanzo
Tofauti ya mimi na wasiochanja hakuna kwani walisema zina madhara lakini sijadhurika kwani tunakula madawa ya kila aina kila leo na yenye side effects za kila aina mpaka zinazoharibu ini au Figo ila bado watu wanakula
Nafikiri nimejaribu kujibu ulichotaka kujua
Babu yangu kijijini pia alinisimulia kuwa alichanja, niliogopa sana na kumwuliza kwanini alichukua uamuzi huo,
Akajibu kuwa aliogopa kufa,
Nashukuru Mungu yupo hai Hadi sasa.