Kwa waliochanja Chanjo ya CORONA Njoni mtoe uzoefu Ili tupime ufanisi.

Kuna magonjwa yanayohitaji dawa za kiroho na mengine yanahitaji dawa za kawaida. Pale msalabani Yesu aliona kiu. Je ilikua kiu ya kawiada au ya kiroho?. Tunaishi kwenye ulimwengu mbili tofauti. Unatakiwa ujue ni wakati gani wa kuishi kwenye ulimwengu wa mwili na wakati gani ni wa kiroho
 
Sijapata madhara yyte sanasana trending yangu ya kupata maambukizi ya mafua imepungua before ilikuwa kila mwaka angalau mara mbili nitapata mafua ila sasa ni mara moja tu..na wala hayakai sana siku nne kwisha.
Nguvu zako za mwili ziko sawa kabisa?

Hupati wenge sometimes?
 
Sijawahi kupata madhara nilipata changamoto siku ya kwanza ila siku zilizofata nilikuwa fresh tu na nilikuwa mtu wa safari za congo mixed paris
 
Mimi nilipata chanjo na haikuniletea shida yoyote!
Siku za nyuma Kabla ya chanjo ya korona mafua yalikuwa yananisumbua sana ikitokea nimeyapa ila baada ya chanjo mpaka leo naenda mwaka wa pili nimesahau habari ya mafua kunisumbua.

Nyumbani wataumwa wote ila sio mimi wakati zamani wakiumwa walihakikisha mimi siambukizwi kwa sababu yakuwa yananileta homa na hata kulala kabisa.
 
Huoni kuwa kutopata mafua kutokana na vumbi lililopo na mabadiliko ya hewa ni tatizo pia?

Vumbi linaloingia mwilini kupitia pua linatokaje ikiwa hupati mafua Wala chafya?
 
Nilichanja pfizer sindano mbili..niko fresh sina tatizo lolote..
Kwahiyo huna tofauti na wasiochanja?

AFYA na kinga Yako imeimarika zaidi au imebaki pale pale?

Nikisema Chanjo kwako haikusaidia chochote nitakuwa sawa?
 
Kwahiyo huna tofauti na wasiochanja?

AFYA na kinga Yako imeimarika zaidi au imebaki pale pale?

Nikisema Chanjo kwako haikusaidia chochote nitakuwa sawa?
Kwahyo uko hapa kuwafariji wasiochanja?
 
Huoni kuwa kutopata mafua kutokana na vumbi lililopo na mabadiliko ya hewa ni tatizo pia?

Vumbi linaloingia mwilini kupitia pua linatokaje ikiwa hupati mafua Wala chafya?
Mafua ya vumbi yanaambukiza? Kwani chanjo ya korona inazuia kupiga chafya?
 
Hayati aliharibu sana akili za Watanzania. Hivi kweli mzungu atake kumuangamiza muafrica ni lazima atumie njano ya Corona?
Watengeza Chanjo wenyewe waliokiri kuwa Chanjo huambatana na kuganda Damu Kwa baadhi ya watu,

Hukusikia Hilo?
 
Mafua ya vumbi yanaambukiza? Kwani chanjo ya korona inazuia kupiga chafya?
Fafanua kidogo,

Umesema kuwa baada ya kuchanja, una zaidi ya miaka miwili hupati homa na mafua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…