Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Hili kitu nimelimwaga aisee.Lilikata std 5 eebana naanza form one likarudi walah niliteseka ule mwaka.Niliomba Mungu juu chini.ila baadae ikakata ndio ikawa mwisho wa fedheha ile.
Ila watu waliokojoa sana wengi ni smart sana kwa akili za darasani.tunahitaji research hapa.
Ah ah ah ah ah pole
 
Nakumbuka siku ya kwanza kazini, nilipangwa mkoa wa Mara, nikaenda na nguo zangu na vitu vyangu vya maana, kutokana na kule ninapokwenda kuwa kijijini nikaomba hifadhi kwa wenyeji...

Wenyeji wakaniambia kuwa huwa wanaogopa kutoka nje usiku kwa sababu kuna wanga wengi hivyo huwa wanajisaidia kwenye makopo..

Nikalala, nikashtuka usiku mikojo imenibana, nikaenda kwenye kopo nikakuta linakaribia kujaa pia sikupenda kujisaidia mle kwa sababu za kiafya

Hivyo nikaona nivumilie tu hakutakawia kucha, ile baridi sikujua mkojo umetoka saa ngapi, nikajikuta asubuhi kwenye bahari ya sham!

Ilibidi nitoe nguo zangu zote nikaushie mikojo ili wenyeji wasishtuke! Hadi leo nashindwa kuwauliza kama siku ile waligundua kuwa nililowanisha godoro!
 
Nlishawahi lowanisha kitanda shuleni nlikuwa form 2 nlikuwa naota nimetoka dining baada ya msosi wa jion nimeenda toilet nipunguze maji niingie prepo ile nafika toilet kengele ya prepo imelia afu mkojo ka haushi vile naongeza spidi haukati mpaka nkaanza kusema isije ikawa naota nkawa najistua stua niamke kama naota na kweli kumbe nlikuwa naota hase nakumbuka nlilala na nguo za darasani zililowa vibaya yaani na sikuwa na mpango wakufua kabisa pia ilikuwa usiku sa tisa nliboeka usingizi ulikata nkaenda kupiga msuli usiku huo kwa hasira
 
Kwakweli sijui kuna mahusiano gani kati ya kukojoa kitandani na kuota, lazima tu uote alafu ndoto yake mkojo haukatiki alafu rahaa kukojoa.

Siwezi kumchapa mwanangu kwasababu ya kukojoa kitandani aisee.
Mchape hase maana wengine hufanya makusudi
 
Mimi mwenyewe hapa niko hoi nikifikiria, nimebaki kucheka za wengine wanaopiga magodoro pasi kuzima msala.

Ngozi ni zaidi ya mwavuli, unajikuta uko swimming pool huna la kusema.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Raha ya ngozi unageuzia upande wa pili uzingizi unaendelea ila godoro ukiharibu ni mwisho wa usingizi
 
Duh nakumbuka mara ya kwnza kukojoa kitandani nikiwa najitambua ilikua nipo darasa la nne, niliota tumeenda kucheza chandim sasa kabla mechi kuanza nikawaambia jamaa wanisubirie nitoe chururu basi nikaenda pembeni ya goli nkaanza kukojoa duh yani nlikua najiskia raha ajabu afu kojo haliishi yani kama robo saa hv minakojoa mdogo mdogo yani mpaka watuwazima wanapita mi nawasalimia huku nakojoa uleutamu haukua wakawaida ghafla nikanza kuhisi joto lenyeunyevu hapo ndipo nlipo gundua ulikua mtego na maumivu ya kibofu yalikua makali kiasi chakukatisha usingizi, ikabidi nitoke kwenye ndoto fasta nikawahi toi then nikachange nguo nikachukua na nguo chafu nikagandamizia pale palipo lowa bahati nzuri palikua hapajaloa sana sasa kazi asubuhi ikiwa kulinda lileeneo madogo wasijue kama bro niliharibu mambo usiku # good old days

Nimecheka sana mkuu, nimekuvutia picha ukiwasalimia wapita njia huku ukimwaga vitu...
 
Duh nakumbuka mara ya kwnza kukojoa kitandani nikiwa najitambua ilikua nipo darasa la nne, niliota tumeenda kucheza chandim sasa kabla mechi kuanza nikawaambia jamaa wanisubirie nitoe chururu basi nikaenda pembeni ya goli nkaanza kukojoa duh yani nlikua najiskia raha ajabu afu kojo haliishi yani kama robo saa hv minakojoa mdogo mdogo yani mpaka watuwazima wanapita mi nawasalimia huku nakojoa uleutamu haukua wakawaida ghafla nikanza kuhisi joto lenyeunyevu hapo ndipo nlipo gundua ulikua mtego na maumivu ya kibofu yalikua makali kiasi chakukatisha usingizi, ikabidi nitoke kwenye ndoto fasta nikawahi toi then nikachange nguo nikachukua na nguo chafu nikagandamizia pale palipo lowa bahati nzuri palikua hapajaloa sana sasa kazi asubuhi ikiwa kulinda lileeneo madogo wasijue kama bro niliharibu mambo usiku # good old days
Sijaelewa maana ya "upenuni" na "chandim"...
 
Back
Top Bottom