Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Ah ah ah ah ah pole
 
Nakumbuka siku ya kwanza kazini, nilipangwa mkoa wa Mara, nikaenda na nguo zangu na vitu vyangu vya maana, kutokana na kule ninapokwenda kuwa kijijini nikaomba hifadhi kwa wenyeji...

Wenyeji wakaniambia kuwa huwa wanaogopa kutoka nje usiku kwa sababu kuna wanga wengi hivyo huwa wanajisaidia kwenye makopo..

Nikalala, nikashtuka usiku mikojo imenibana, nikaenda kwenye kopo nikakuta linakaribia kujaa pia sikupenda kujisaidia mle kwa sababu za kiafya

Hivyo nikaona nivumilie tu hakutakawia kucha, ile baridi sikujua mkojo umetoka saa ngapi, nikajikuta asubuhi kwenye bahari ya sham!

Ilibidi nitoe nguo zangu zote nikaushie mikojo ili wenyeji wasishtuke! Hadi leo nashindwa kuwauliza kama siku ile waligundua kuwa nililowanisha godoro!
 
Nlishawahi lowanisha kitanda shuleni nlikuwa form 2 nlikuwa naota nimetoka dining baada ya msosi wa jion nimeenda toilet nipunguze maji niingie prepo ile nafika toilet kengele ya prepo imelia afu mkojo ka haushi vile naongeza spidi haukati mpaka nkaanza kusema isije ikawa naota nkawa najistua stua niamke kama naota na kweli kumbe nlikuwa naota hase nakumbuka nlilala na nguo za darasani zililowa vibaya yaani na sikuwa na mpango wakufua kabisa pia ilikuwa usiku sa tisa nliboeka usingizi ulikata nkaenda kupiga msuli usiku huo kwa hasira
 
Kwakweli sijui kuna mahusiano gani kati ya kukojoa kitandani na kuota, lazima tu uote alafu ndoto yake mkojo haukatiki alafu rahaa kukojoa.

Siwezi kumchapa mwanangu kwasababu ya kukojoa kitandani aisee.
Mchape hase maana wengine hufanya makusudi
 
Raha ya ngozi unageuzia upande wa pili uzingizi unaendelea ila godoro ukiharibu ni mwisho wa usingizi
 

Nimecheka sana mkuu, nimekuvutia picha ukiwasalimia wapita njia huku ukimwaga vitu...
 
Sijaelewa maana ya "upenuni" na "chandim"...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…