Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Sijui ilikuaje lakini hihabari niliishinda nadhani nikiwa kidato cha kwanza, hats hivyo niligundua teknolojia iliyonisaidia kuwa nakausha hicho kimiminika Kabla ya asubuhi, shida ilikua namna ya kuondoa ramani(mkojo ukikauka unaachaga ramani) kama siku hiyo shuka lililotumika sio la maua maua!
 
Kinachinishangaza kwanini ilikuwa lazima tuote? Yaani kama sio mgonjwa lazima uote unakojoa tu ukojoe kitandani. Watoto wote kesi hio hio unaota.

Nafikiri kizazi chetu hatutawachapa hovyo watoto wakikojoa kwasababu tunaelewa kinachowasibu.
Kwakweli sijui kuna mahusiano gani kati ya kukojoa kitandani na kuota, lazima tu uote alafu ndoto yake mkojo haukatiki alafu rahaa kukojoa.

Siwezi kumchapa mwanangu kwasababu ya kukojoa kitandani aisee.
 
Hahahaaaa! Ulikuwa unaukaushaje?
Na harufu je?
 
sasa si ungelala na kopo mkuu
 
Mama unacheka tu, hebu tupe experience yako.

MBITIYAZA na Nalendwa msijifanye hamkukojoa kitandani, hebu mkuje.
ha haha me nilikuwa nakojoa mara moja moja halafu namchukua mdogo wangu alikuwa analala sana namsukumizia kwenye mikojo yangu..akiamka analia mama anampiga ila akirudi ananidunda ,,.. tatizo lingine mimi siyo muongeaji kujitetea sana siwezi na kumpiga siwezi ila dawa yake nilikuwa nasubiria niharibu nimsogeze na sijawahi kukamatwa
 
Mi niliambiwa kila aina ya dawa mara huyu kasema sijui nipande juu ya mti nikojoe huku naruka toka kwenye tawi,mara nikakojolee mstari wa siafu wapii mara sijui kunywa maji ya mchele yale ya kuoshea wapii kila mbinu nilitumia ila bado nikawa nakojoa bado formula ni iyo iyo ya ndoto uzuri nilikua nalala peke yangu so nikilowesha hapa nahamia pale naendeleza usingizi mbinde maza akija asubui kukagua ha ha ha sometime nikijoa nawai shule kukwepa kipigo ukiludi ile unaingia getini maza anakuanzia vitasa kule kule ikafikia akataka kuja kunitangaza shule da ila akagaili ila ilikua very psychological torture mamnake watoto wengine walikua napapitishwa mtaani na kindumbwe ndumbwe chaliaaaa
 
[emoji15] [emoji15] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] hiyo ya kupanda juu ya mti unakojoa huku unaruka...

mi nliacha kukojoa nkiwa na miaka 8 tu.
nkistuka saa 10 usiku nimelimwaga kojo usingizi hauji tena mpaka kunakucha.
sasa kama ni siku ya shule hiyo ni afadhali yangu but nkiwa darasani ni mawazo tu kama bi mkubwa kagundua ule msala au nliolala nao.
nkirudi naingia kwa kunyata..
but kama ni weekend nachezea makofi na bakora hizo..hapo kindumbwe ndumbwe cha mashosti kinanisubiri nje..loh!
 
Hahahaaaa! Ulikuwa unaukaushaje?
Na harufu je?
harufu haikua kubwa sana nadhani, ilikua ni kuchukua matambala/nguo nakulalia eneo husika nahisi mikojo ilikua inafyonzwa na nguo hizo, familia haikua ikininyanyapaa, tatizo lilikuja likaisha lenyewe, personally sikuwa nasababishwa na kuota it was just happening aisee, sijui ilikua nini sababu, nilipokuja kulifutilia hili tatizo niliona sababu yake imefungamana na mambo kadhaa ya kisaikolojia wakati wa malezi/makuzi.
 
Ha ha ha, acheni kufukua makaburi.

Kilichokuwa kinanishangaza ni kwamba nikiwa ugenini likizo kwa wajomba hii kitu ilikuwa nadra sana kutokea.
 
Nyie watu nyie hebu acheni bwana!mimi nishabwanda sana tu ila nisiyo sahau ni siku nilienda kwa uncle ikawa late nikaamua ku overnight kule na nililala na suruali ile ile (enzi zile tuoipiga sana couldruoy ).
Mwanangu ugenini nikachafua ikabidi mtoko wa next day uwe shida maana cousins wangu age moja mademu (i was 10yrs or so) nikavaa ya kike moja mpaka suruali ifuliwe ikauke mpaka leo aunt nikisimanga watu wanaovaa za kike ananikumbusha hii makitu na huyo cousin wangu anasema nina bahati enzi zile foto foto ilikuwa hamna
 
Kinachonishangaza hawa wazazi hawakupitia hii stage? Kwasababu watoto wote chanzo ni ndoto wala si uzembe. Umecheza mchana kutwa unalala hoi! Na ubongo ulivyona makusudi unakuotesha ule ule mchezo uliocheza unaenda kwenye majani unakojoa kumbe uko kitandani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…